Meya wa Jiji la Dar Masaburi ajibu Mapigo ya Wabunge; Masaburi awatusi wabunge !!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya wa Jiji la Dar Masaburi ajibu Mapigo ya Wabunge; Masaburi awatusi wabunge !!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kikarara78, Aug 6, 2011.

1. Kikarara78

Kikarara78 JF-Expert Member

#1
Aug 6, 2011
Joined: Nov 18, 2010
Messages: 1,164
Likes Received: 514
Trophy Points: 280
Greetings Great Thinker,
Kila lenye Mwanzo lina Mwisho. Naona Sakata la UDA limechukua Kasi yeke baada ya Meya kuwatusi Wabunge kuwa wanatumia Makalio aka ****** kufikiri na siyo akili, amesema Mchakato wa kuuzwa UDA ulianza 2008 hata kabla hajawa Diwani.
Ukweli wa jambo hili upo wapi ??
Wahusika, wenye habari kamili tuabarisheni

MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, ambaye ametakiwa na wabunge wa jiji la Dar es Salaam kujiuzulu kupisha uchunguzi kutokana na kashfa ya uuzaji kifisadi Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), amewajibu wabunge hao na kusema kuwa kuna baadhi yao wanashindwa kufikiri kwa kutumia vichwa na badala yake wanafikiri kwa kutumia 'makalio'.
Masaburi alitoa kauli hiyo nzito jana mjini hapa alipozungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Naura Spring ambapo anahudhuria mkutano wa pamoja wa kamati za uongozi za serikali za mitaa za nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EACLAT).
Alisema wabunge katika kuchangia hoja ya suala la UDA wamegawanyika katika mafungu matatu ambao alisema katika mafungu hayo moja halijui lolote kuhusiana na sakata hilo na limedandia tu hoja na kuwataja miongoni mwao ni mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, na mbunge wa Mafia, Abdukarim Shah.
Alitaja kundi la pili kuwa ni la wabunge wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mbunge wa Ubungo, John Mnyika, na mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambao alisema wanatafuta umaarufu wa kisiasa kupitia sakata la UDA.
Alisema Mnyika aliweza kuhoji hata katika vikao rasmi, lakini Mdee hajui chochote kwa kuwa hajawahi kuhudhuria vikao vya jiji mpaka sasa.
Aidha, kundi la tatu ambalo ndilo alilituhumu zaidi kufikiri kwa kutumia makalio badala ya kichwa ni la wabunge Abasi Mtemvu (Temeke), Musa Azzan 'Zungu'(Ilala) na Makongoro Mahanga (Segerea) ambao alidai kuwa wanajua ukweli wa jambo hilo lakini wanapotosha ili kuficha madhambi yao ambayo alisema yataibuliwa muda si mrefu ya ufisadi ndani ya jiji hilo.
"Hawa wabunge ambao wana nyadhifa toka kipindi kilichopita ndio wanaohusika na kulifilisi shirika hilo na mashirika mengine ya jiji kwa kuwa mchakato wa kuuzwa kwa shirika hilo ulianza toka mwaka 2008 ambapo mimi nilikuwa hata sijawa diwani," alisema Masaburi.
Alieleza kuwa toka kipindi hicho kwa mujibu wa madokezo yaliyopo kuhusiana na uuzwaji wa shirika hilo, yanaonyesha maamuzi yalipitishwa na vikao halali hadi kuuzwa kwake mapema mwaka huu ambapo yeye hajashiriki kwa lolote mpaka wanauziana.
"Mimi ndiye niliyeibua hii tuhuma ya kuuzwa kwa UDA wakati nikihoji mali zinazomilikiwa na jiji na kuambiwa UDA imeishauzwa; nilipofuatilia nikakuta imeuzwa shilingi milioni 285! Nilipofuatilia hizo fedha kama zipo nikakuta milioni 200 zimeshaliwa; nikaamua kumsimamisha meneja wa shirika hilo na mhasibu. Sasa leo nageuziwa kibao kuwa mimi ndiye nimeuza inashangaza sana!" alisema Masaburi.
Aliendelea kusema wabunge hao wanang'ang'ania ajiuzulu kutokana na hofu iliyotanda baada ya kuanza kazi ya kuibua ufisadi ndani ya jiji hilo kwa kuanzia na UDA.
"Baada ya kuibua ufisadi UDA sasa nimepanga nihamie shirika la DDC ambako Mtemvu ni mwenyekiti wa bodi; shirika ambalo nalo kuna ufisadi mkubwa umefanyika ikiwemo kuuza mashamba ya shirika hilo na baadhi ya nyumba," alisema.
Alisema akimaliza suala hilo atahamia kuhakiki matumizi ya ujenzi wa Machinga Complex ambapo alidai inashangaza kusikia zimetumika bilioni 1.2 kujenga zile nyavu za vizimba ambavyo alifananisha na nyumba za wanyama wafugwao.
Alisema kutokana na mkakati wake huo anaomba wabunge wampe muda wa kutekeleza hayo.
Masaburi alisema hawezi kujiuzulu kwa shinikizo la mafisadi na kudai endapo akifuatilia mashirika yote hayo na kubaini yapo sahihi yuko radhi kujiuzulu kama itahitajika.
"Naomba wanipe muda kidogo nisafishe ufisadi ndani ya jiji la Dar es Salaam kutokana na mikataba ya ajabu iliyoingiwa baina ya viongozi waliokuwepo madarakani kipindi cha nyuma wakishirikiana na wabunge na kulitia umaskini jiji ili kama kuna hoja za msingi wabunge wapate hoja za kujadili bungeni," alijinasibu Masaburi.
Alifafanua kuwa kuhusu suala la malipo ya mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Iddi Simba, kutoka kwa wanunuzi wa shirika hilo yeye hatambui kwa kuwa hakuna risiti yoyote ya UDA inayoonyesha malipo hayo.
Aliongeza kuwa hata baada ya yeye kupata barua za kuwepo kwa malipo ya sh milioni 320 zilizofanywa kupitia akaunti ya Iddi Simba alimfuata mwenyekiti huyo na kuhojiana naye na alikiri kupokea malipo hayo, lakini alisema hayahusiani na mauzo ya UDA na kusema yanahusiana na biashara zao binafsi.
Alisema kutokana na majibu hayo ya Iddi Simba hakuwa na mamlaka ya kung'ang'ania kuwa malipo hayo ni sehemu ya malipo ya UDA hivyo vyombo kama Takukuru ndio nafasi yao ya kuchunguza suala hilo.
Akizungumzia tamko la Waziri Mkuu kuviagiza vyombo vya Takukuru, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ofisi ya DCI kushughulikia suala hilo, aliunga mkono uamuzi huo kwani ndio utabainisha wazi wote waliohusika katika kuliuza shirika hilo.
Sakata la kuuzwa kwa UDA lilichukua nafasi katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ambapo ilifikia wakati wabunge kutishia kutoipitisha bajeti hiyo na kutaka wote waliohusika katika uuzaji wa shirika hilo wawajibishwe ikiwemo Masaburi kwamba ajiuzulu kabla ya Waziri Mkuu kuingilia kati na kuunda tume kuchunguza suala hilo.

Source: Tanzania Daima

2. B

Bajabiri JF-Expert Member

#2
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Tangu sakata la UDA liibuke kumekuwa na majibizano ya dhahiri baina ya wabunge wa Dar es Salaam na Meya wa Jiji dr Masaburi,lakini vijembe vimejikita zaidi kati ya wabunge wa Temeke na Ilala kwa Meya,Dr masaburi nimemnukuu kwenye vyombo vya habar akisema kuwa mtemvu na Zungu nao pia ni mafisadi maana lengo lao ni kumnyamazisha tu,wana kashfa ya MACHINGA COMPLEX-ZUNGU,na ya DDC-MTemvu,masaburi anaenda mbali zaidi kwa kudai kuwa wabunge hao walishiriki kuuza shamba la jiji lililopo hiko Ruvu,lakin leo baadh ya magazeti yamemnukuu Zungu akidai atamlipua masaburi kwa Ufisad wake pale Machinga Complex,,,,,,,mabako Zungu nae anatajwa kuwa ana mkono wake pale,,,,,,
Swali la kujiuliza ni je haya yooote mbona hayakuzungumzwa huko nyuma????sisi wananch tuwaelewaje hawa watawala????masaburi anapaswa kutujibu na pia wabunge wa dar wanaosema wana ushahidi juu ya Masaburi wanapaswa kujibu hili,au ndio tuamini kuwa kuna mgongano wa kimaslahi????au tuamin kuwa hawa jamaa wamedhulumiana?????maana masaburi anadai kuwa wabunge hao wanamhofia tu,,,,,,,
NAWASILISHA

3. K

Kicheruka JF-Expert Member

#3
Aug 8, 2011
Joined: Feb 2, 2009
Messages: 791
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
Wote wezi wafikishwe mahakamani kila mmoja akatoe ushahidi wake mahakamani waache kubwabwaja kwenye TV

4. The Son of Man

The Son of Man JF-Expert Member

#4
Aug 8, 2011
Joined: Feb 9, 2010
Messages: 12,124
Likes Received: 1,707
Trophy Points: 280
Kwa state kama hii everybody claims innocence lakini ukweli waja tu!

5. B

Bajabiri JF-Expert Member

#5
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

nimejiuliza sana,yaani kwa sasa hapa Tanzania,mtu akituhumiwa nae anatuhumu,ina maana ni kusema kwamba MBONA YEYE KAIBA??KAMA MIMI MWIZI NA WEWE MWIZI,ndio mambo yanavyokwenda sasa,,,,,

6. B

Bajabiri JF-Expert Member

#6
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

utakujaje wakati huwa mambo yanaishia hivihivi???

7. K

Karry JF-Expert Member

#7
Aug 8, 2011
Joined: Mar 26, 2011
Messages: 266
Likes Received: 1
Trophy Points: 33
hahha kazi kweli kweli uko sahihi kna yeye mbona mwizi ananisema mm

8. mtu chake

mtu chake JF-Expert Member

#8
Aug 8, 2011
Joined: Aug 20, 2010
Messages: 4,090
Likes Received: 1,262
Trophy Points: 280
...vita ya panzi...furaha kwa....

9. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#9
Aug 8, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160
hapo lazima ujue kabisa kila mtu anahusika ila wao wanajifanya wajuaji na wasafi mbaya..

10. Kimilidzo

Kimilidzo JF-Expert Member

#10
Aug 8, 2011
Joined: Jan 3, 2011
Messages: 1,346
Likes Received: 38
Trophy Points: 135
Usije ukawaamini au kuwadhamini Magamba, dakika yoyote wanakuliza linapokija suala la maslahi binafsi. Wote hao mwisho wa siku utasikia kila mmoja kachukua chake siku nyingi. CCM sio watu wa kuwachezea kabisa. UDA imeishajichokea wanaigombania, wao kinachowatoa udenda ni majengo ya UDA ambayo yako katika maeneo yenye very high real estate value. Hawana nia hata moja ya kuwasafirisha watu wa dar waliozoea vipanya. Magamba kwa ufisadi oyeeeeeeee

11. N

Ndinani JF-Expert Member

#11
Aug 8, 2011
Joined: Aug 29, 2010
Messages: 5,413
Likes Received: 734
Trophy Points: 280
Mimi nchi hii inanishangaza sana hasa Rais wetu KIWETE kwani huyu Didas Masaburi anajulikana dunia nzima kuwa ni mtu mchafu[ fisadi papa] hata hivyo Rais wetu anamkumbatia kwanza akampa kuwa mbunge wa Afrika Mashariki [ ingawa sio siri kuwa aliununua ubunge ule kwa kuwahonga wabunge] na sasa amembeba mpaka amekuwa Meya wa jiji [ akigombea udiwani magogono ingawa hakai huko]. Masaburi ni mwizi na hii itadhihilika pale uchunguzi makini ukifanywa kwenye hili sakata la UDA; Masaburi amafisadi hapa na akiachiwa kuendelea kuwa Meya ataiba zaidi at the detriment ya wananchi!!

12. Limbani

Limbani JF-Expert Member

#12
Aug 8, 2011
Joined: Apr 24, 2008
Messages: 1,441
Likes Received: 91
Trophy Points: 145
Ukiwa mwana CCM ni sawa na kuwa mchawi, lazima tu utashiriki kula nyama za watu (wizi). Ndio maana kila mtu anamnyooshea kidole mwengine maana wanajuana wote, hakuna watu wasafi CCM!!

13. MAMMAMIA

MAMMAMIA JF-Expert Member

#13
Aug 8, 2011
Joined: Feb 26, 2008
Messages: 3,822
Likes Received: 23
Trophy Points: 0
...ziumiazo nyasi (lolz!)

14. B

Bajabiri JF-Expert Member

#14
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

sure,maana machinga complex ni mtaji wao,ndio maana wanaumana,ukija ddc na mashamba ya jiji,hata mi sikua najua kuwa jiji lina mashamba,sasa leo wanapotupiana vijembe thru media napata kigagaziko,inakuwaje?????nani msafi???kwanin sasa????ina maana walikuwa wakifichiana siri????za wizi???

15. B

Bajabiri JF-Expert Member

#15
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

viongoz wetu wamekuwa si watu wa kukemea hadi wanapodhulumiana,,,,,nadhan hata Zombe alipomtuhumu lema,nikajiuliza alikuwa WAPI?????

16. B

Bajabiri JF-Expert Member

#16
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

ni vigumu sana kumchongea abiria mwenzio ambae hajalipa nauli kwenye treni wakat na wewe ni miongoni mwao,la sivyo mtashushwa wote

17. Mwita25

Mwita25 JF-Expert Member

#17
Aug 8, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 3,840
Likes Received: 18
Trophy Points: 0
Kweli kabisa MB

18. Baba_Enock

Baba_Enock JF-Expert Member

#18
Aug 8, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 6,802
Likes Received: 164
Trophy Points: 160
WOTE ni Wanyang'anyi - Kama ilivyo kuanzia kwa Mkuu wa Kaya mpaka mjumbe wa mtaa!

Wa_Tanzania wote ni wezi na hamna mtu wa kumnyooshea kidole mwenzake - Taifa lililooza - SHAME!

19. Vin Diesel

Vin Diesel JF Gold Member

#19
Aug 8, 2011
Joined: Mar 1, 2011
Messages: 8,402
Likes Received: 737
Trophy Points: 280
time never lies...

20. B

Bajabiri JF-Expert Member

#20
Aug 8, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

until when Sangara?hapo ndipo napotaka kujua,maana siri ya kununua uongoz naiona hapa,Zungu ni miongon mwa wabunge wanaosifiwa kuwa wanawasaidia sana raia wake,lakin kma kashfa ndio hizi kumbe zile hela ni za wananchi,mtemvu nae ameanzisha hadi MTEMVU FOUNDATION,ipo maeneo ya KEKO,kumbe wanatuzuga????

Loading...