Meya CHADEMA azikataa milioni 200 za CCM

Meya CHADEMA azikataa milioni 200 za CCM

Tuombe tu kilichoandikwa kwenye post hii kiwe cha kweli; vinginevyo amenasa na ni aibu kwa upinzani.
mkuu aliyenasa ni Ally Hapi si Meya , hili jambo Iringa nzima inamshangaa mno RC kukubali kazi aliyopewa ya kubomoa Chadema ( ambayo hataweza milele ) na kuacha majukumu yake halali na mepesi ya ukuu wa Mkoa
 
Erythro, kwa hiyo unawakaribisha wasiojulikana 'Makao Makuu' wakairipue kwa mabomu?

Imekuwa vigumu siku hizi kuchambua ukweli ni upi na nini ni gelesha tu!
Kama alichosema Erythrocite ni ukweli, unafikiri copies za hizo audio clips zitakuwa makao makuu peke yake?
 
Madai ya Mstahiki Alex Kimbe ya kutishwa na ccm kuuawa asipopokea ile mil 200 ya kuunga mkono juhudi yamefika patamu , hii ni baada ya kuwepo madai ya kurekodiwa kwa HD kwa mamluki waliotumwa kuleta hela hiyo akiwemo mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi , ambaye amebainika pia kutumia mitandao ya kijamii kumchafua meya huyo kwa kutumia majina bandia.

Hii ndio sababu ya ccm Mkoa pamoja na ofisi ndogo Lumumba kushindwa kukanusha tuhuma hizo chafu na za kufedhehesha zinazogusa moja kwa moja Mwenyekiti wa ccm Taifa , Tuhuma za rushwa ya kutengeneza inayomkabili Mh Kimbe , pamoja na mambo mengine imesababishwa na yeye kugoma kutoa flash / cd iliyotumika kurekodia watoa rushwa ya ushawishi wa mil 200 ( imehifadhiwa Chadema Makao Makuu )

Natoa wito kwa TAKUKURU Iringa kuacha kutumikishwa kwa malengo binafsi , wakuu wa mikoa wanapita tu lakini Taasisi hii ya umma itabaki , wasijiingize kwenye michezo michafu maana hawana kinga yoyote huko mbeleni .
Waweke wazi maana toka yale ya CD ya mabomu ya Arusha siwahamini
 
mkuu aliyenasa ni Ally Hapi si Meya , hili jambo Iringa nzima inamshangaa mno RC kukubali kazi aliyopewa ya kubomoa Chadema ( ambayo hataweza milele ) na kuacha majukumu yake halali na mepesi ya ukuu wa Mkoa
Erythrocyte, shida ni kwamba mahakama inaweza kusema kuwa ushahidi huo haukubaliki kwa sababu zozote zile maCCM yanaweza chochote. Binafsi nangojea huyo 'Happiness' anase nisherehekeee kunasa kwa aliyemteua!
 
Hao wanaojiita maafisa wa TAKUKURU naona akili hawana. Hukob Arusha kuna mjinga mmoja katoa rushwa ili kuwanunua madiwani,ushahidi wamepewa lkn hawakuchukua hatua yoyote zaidi ya kuongea utumbo waliousema.
Huko Iringa wanajidai kumkamata meya kwa kisa cha kupewa hongo,lkn hawamkamati aliyetoa hiyo hongo,sisi kama watanzania tunawezaje kuiamini taasisi kama hii iliyojipambanua kupambana na rushwa?
Kama hujali hata ubinadamu basi walau mtambue kwamba Mungu yupo na siku moja mtakufa na mtatoa hesabu kwa matendo yenu haya.
 
Madai ya Mstahiki Alex Kimbe ya kutishwa na ccm kuuawa asipopokea ile mil 200 ya kuunga mkono juhudi yamefika patamu , hii ni baada ya kuwepo madai ya kurekodiwa kwa HD kwa mamluki waliotumwa kuleta hela hiyo akiwemo mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi , ambaye amebainika pia kutumia mitandao ya kijamii kumchafua meya huyo kwa kutumia majina bandia.

Hii ndio sababu ya ccm Mkoa pamoja na ofisi ndogo Lumumba kushindwa kukanusha tuhuma hizo chafu na za kufedhehesha zinazogusa moja kwa moja Mwenyekiti wa ccm Taifa , Tuhuma za rushwa ya kutengeneza inayomkabili Mh Kimbe , pamoja na mambo mengine imesababishwa na yeye kugoma kutoa flash / cd iliyotumika kurekodia watoa rushwa ya ushawishi wa mil 200 ( imehifadhiwa Chadema Makao Makuu )

Natoa wito kwa TAKUKURU Iringa kuacha kutumikishwa kwa malengo binafsi , wakuu wa mikoa wanapita tu lakini Taasisi hii ya umma itabaki , wasijiingize kwenye michezo michafu maana hawana kinga yoyote huko mbeleni .
JF ina mtindo wake wa kutoa habari ambao uliipatia sifa kubwa. Kama hiyo flash/CD ipo, tunaomba iwekwe hapa ili watu tujadili. Mambo ya kusema ipo ni kama ule mchezo wa bomu lililolipuka Arusha, tukaambiwa CD ipo bila kuonekana hadi kesi yote ikapotea. Onyesheni video hiyo ili watu wapate aibu. Kwa nini maneno matupu?
 
Daah naishia kusikitika tu kwa yanayojiri kwenye nchi yangu
 
Hamna lolote walahi mijitu ya Mbagala tu hiyo walahi
Walahi!!!!walah!!!!!katika members wasio na faida humu wewe ni namba moja,pumba zimekuzidi hata hao wanaokutuma ni wajinga kama wewe?
 
Na wewe pia ni akili kubwa ndio maana umepost saa nane kasoro usiku
hivi unajua kuwa mwenzio aliyeko Mexico, Cuba, USA, Canada, etc muda wake ni tofauti na wewe uliyepo hapo Kwamtogore??
 
Yani chadema wawe na hiyo video alafu iwekwe makao makuu bila kuwekwa mitandaoni?
 
Ikibainika hivyo tunataka mamlaka ya uteuzi wa huyo RC imchukulie hatua stahiki. Nchi hii hatutaki kumwona hata mmoja wetu akionewa,akionewa mmoja tumeonewa wote na haki ni msingi wa maendeleo bila hiyo baraka hupita mbali na kusali kwetu huwa nibure kabisa
Wakati mwingine mbwa huwinda kwa ajili ya mwenye mbwa.
 
Back
Top Bottom