Meya CHADEMA azikataa milioni 200 za CCM

Bora kufa masikini kuliko kuwa na utajiri wa kuwasaliti wananchi wako walio shinda kwenye foreni wakinyeshewa na mvua ili kukuchagua.

Wengine hadi sasa ni vilema wa kudumu kisa hizo chaguzi
Huyo atakufa maskini...na 2020 halambi udiwani wala jimbo arudi kwao akalime mihogo

In God we Trust
 
CCM hizi tuhuma ni nzito mno..yaani mnanunua HAKI...
Chama twawala kinanunua HAKI kweli..
 
JUMAMOSI , 17TH NOV , 2018
NA MWANDISHI WETU
Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe, amefunguka kuwa amekuwa akijikuta na kesi mbalimbali mahakamani kwa kile alichokidai kuwa ni hujuma anazofanyiwa na Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa amekataa kuhamia ndani ya chama hicho.

Meya%20Iringa.jpg

Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe,.​
Mapema jana asubuhi kulianza kusambaa kwa taarifa kuwa Meya huyo wa Iringa Mjini, alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai ya kukutwa na fedha ya mtego zaidi ya shilingi milioni 2 na mzabuni Nancy Nyarusi.
Akizungumza Mjini Iringa Kimbe amesema “hii si mara ya kwanza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali na wote wanaonishtaki ni makada wa Chama Cha Mapinduzi.”
Lengo la CCM ilikuwa ni kupata Meya anayetokana na Chama Cha Mapinduzi na walipoleta hoja hiyo ikashindikana kwa sababu walikiuka kanuni, na baada ya kufeli wakaamua kuniundia tuhuma mbalimbali.” Amesema Kimbe
Wanafanya yote hayo ili nikubali milioni 200, nijiunge nao na mara ya mwisho walinifuata baadhi ya viongozi wa CCM ili wanipatie hizo fedha na wanifutie kesi, na huu msimamo wangu ndiyo chanzo kikubwa haya yote.” Ameongeza Meya huyo.

Habari zaidi, soma=>Meya wa Manispaa ya IRINGA Alex Kimbe (CHADEMA) amekamatwa na TAKUKURU - JamiiForums
Hatari sana
 
hakuna mwanachadema kama meya mwenye uwezo kukataa milioni 200. hata 100 tu.
 
Back
Top Bottom