Meya CHADEMA azikataa milioni 200 za CCM

mashakani

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2018
Posts
615
Reaction score
990
JUMAMOSI , 17TH NOV , 2018
NA MWANDISHI WETU
Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe, amefunguka kuwa amekuwa akijikuta na kesi mbalimbali mahakamani kwa kile alichokidai kuwa ni hujuma anazofanyiwa na Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa amekataa kuhamia ndani ya chama hicho.

Meya%20Iringa.jpg

Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe,.​
Mapema jana asubuhi kulianza kusambaa kwa taarifa kuwa Meya huyo wa Iringa Mjini, alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai ya kukutwa na fedha ya mtego zaidi ya shilingi milioni 2 na mzabuni Nancy Nyarusi.
Akizungumza Mjini Iringa Kimbe amesema “hii si mara ya kwanza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali na wote wanaonishtaki ni makada wa Chama Cha Mapinduzi.”
Lengo la CCM ilikuwa ni kupata Meya anayetokana na Chama Cha Mapinduzi na walipoleta hoja hiyo ikashindikana kwa sababu walikiuka kanuni, na baada ya kufeli wakaamua kuniundia tuhuma mbalimbali.” Amesema Kimbe
Wanafanya yote hayo ili nikubali milioni 200, nijiunge nao na mara ya mwisho walinifuata baadhi ya viongozi wa CCM ili wanipatie hizo fedha na wanifutie kesi, na huu msimamo wangu ndiyo chanzo kikubwa haya yote.” Ameongeza Meya huyo.

Habari zaidi, soma=>Meya wa Manispaa ya IRINGA Alex Kimbe (CHADEMA) amekamatwa na TAKUKURU - JamiiForums
 
Tuliochagua kuukataa moja kwa moja utawala huu kutokana na makandokando yake kama haya, hatujawahi kukosea na kamwe hatuna cha kujutia.

Sometimes ni bora shetani kuliko binadamu wa aina hii!!

Unajiuliza wanaofanya hujumu kama hizi wanapata wapi uhalali wa kukamata wengine kwa makosa ya rushwa na ufisadi na kamwe huwezi pata jibu.

Hizi ni siasa chafu na za hovyo zinazoweza kufanywa na watu walioshindwa ku-deliver na ambao uwezo wa kufikiri umefika mwisho.
 
Huyo atakufa maskini...na 2020 halambi udiwani wala jimbo arudi kwao akalime mihogo
 
JUMAMOSI , 17TH NOV , 2018
NA MWANDISHI WETU
Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe, amefunguka kuwa amekuwa akijikuta na kesi mbalimbali mahakamani kwa kile alichokidai kuwa ni hujuma anazofanyiwa na Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa amekataa kuhamia ndani ya chama hicho.

Meya%20Iringa.jpg

Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe,.​
Mapema jana asubuhi kulianza kusambaa kwa taarifa kuwa Meya huyo wa Iringa Mjini, alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai ya kukutwa na fedha ya mtego zaidi ya shilingi milioni 2 na mzabuni Nancy Nyarusi.
Akizungumza Mjini Iringa Kimbe amesema “hii si mara ya kwanza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali na wote wanaonishtaki ni makada wa Chama Cha Mapinduzi.”
Lengo la CCM ilikuwa ni kupata Meya anayetokana na Chama Cha Mapinduzi na walipoleta hoja hiyo ikashindikana kwa sababu walikiuka kanuni, na baada ya kufeli wakaamua kuniundia tuhuma mbalimbali.” Amesema Kimbe
Wanafanya yote hayo ili nikubali milioni 200, nijiunge nao na mara ya mwisho walinifuata baadhi ya viongozi wa CCM ili wanipatie hizo fedha na wanifutie kesi, na huu msimamo wangu ndiyo chanzo kikubwa haya yote.” Ameongeza Meya huyo.
Navalonge swela!
 
Yaani mpaka hapa inaonesha kabisa hufai kuwa kiongozi wa ngazi yoyote kwenye jamii. You can even betray your own family for money.
Watu wa namna hii hata Mungu anawanyima nafasi ambazo kupitia maamuzi yenu mtaiumiza jamii inayowazunguka. Pathetic
Huyo atakufa maskini...na 2020 halambi udiwani wala jimbo arudi kwao akalime mihogo
 
Kwa msimamo wa huyu meya nampa 5,ni wachache sana wenye msimamo kama wake dunia ya sasa.kwanza amethamini kazi aliyopewa na wanachi wake na kuwatumikia vyema siku zote giza na nuru havichangamani kamwe,vipige vita vizuri na heshima utaitunza ewe meya uliyekubali kuwatumikia wananchi kuliko kutumikia hawa viumbe wa kijani walio jaa husuda.
 
Huyo atosahau kama yuda aliweza kumsaliti yesu kwa vijisent leo mimi naanzaje kukataa 200mil tena kwa kumsaliti mbowe na nyumbu hahahha
 
Nani ana muda wa kumpa mtu milioni zote hizo
 
Back
Top Bottom