Flight_controller
JF-Expert Member
- Dec 4, 2018
- 252
- 415
=====
Fujo ZAIBUKA...Azungumza! Meya wa jiji la Dar Isaya Mwita ambaye ni pia ni diwani wa Mbweni amezuliwa na Askari Kuingia ofisi kwake alipoenda kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Halmashauri. Madiwani wote ni wajumbe wa vikao kuhusu masuala ya jiji la Dar es Salaam .
Sakata la leo limetokea mbele ya mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao Tanzania waliofika kikazi ktk eneo la ofisi za meya . Kiitifaki Meya Isaya Mwita Charles anatakiwa awapokee kwa niaba ya wananchi wa Dar es Salaam.
Sakata la meya lilianza baada ya kura za kumuondoa kisheria ya 2/3 za madiwani wote kabisa waridhie aondoke kwenye umeya kushindikana kupatikana. Sasa suala hili limekuwa la kisiasa zaidi kwa mkurugenzi wa jiji na serikali ya CCM kufanya kila linalowezekana kumzuia meya kuingia ofisini na hata kufikia kumzuia meya ambaye ni diwani kuhudhuria vikao kama diwani.
Source: Global TV online