Methali mpya

Methali mpya

Upuuzi wa tajiri, ni burudani kwa maskini,

Hekima ya maskini, ni kero kwa maskini wenzake.
 
mtu akikuudhi mtemee mate ya usoni...................he! he! heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
ukitaka kumwona kinyonga mtu, mtazame mbongo wakati wa uchaguzi.
 
Methali / Nahau 20:


  • Uliza Wazimbabwe, si kila umilionea ni utajiri!
  • Katika shitaka ndilo silo, hakimu halaumiwi
  • Kwao senene-panzi, kwetu samaki uduvi- nyoka
  • Habari kuu ni mwana-habari kuminya habari
  • Usawa pia ni kutoa isivyo-sawa kwa wasio-sawa
  • Kusemwa ni sehemu za gharama za umaarufu
  • Ukitaka uchunguzi wa bure, shinda medali zao
  • Andika kwa siri, ‘marehemu mtarajiwa’, kabla ya jina la yeyote
  • Utamu wa pilipili kuwashwa (ya zamani)
  • Kwao mitala loh!, kwetu ushoga aka!
  • Mfeki hutetea cheti feki
  • Wakati wa majilio ya simba, si kila abakiaye kitako ni shujaa
  • Bendera za vyama huchipuka majira ya chaguzi
  • Raia akutwe na pingu, tujue matumizi na sheria yake
  • Asifiwe na Asi-fiwe hutamkwa tofauti kuleta maana tofauti
  • Cheza cheza kutukuza Mola, na si kulipa kisasi cha kutokwenda kwenye kumbi za starehe!
  • Urembo, somo pana na lenye ukinzani mkubwa
  • Si kila liandikwalo lina ukweli; si kila lisiloandikwa halipo
  • Hadhi ya mtu huathiri ukubalika wa ujumbewe
  • Anyaye, hukojoa
 
Back
Top Bottom