Methali mpya

Methali mpya

Mwendawazimu ni binadamu mwenye Uhuru bila Nidhamu, na Mtumwa ni binadamu mwenye Nidhamu bila Uhuru.
 
Tege la maskini kilema,

Tege la tajiri urembo,
 
Ukubwa wa dunia hauzidi kichwa chako -(mpya)

Tembea uone - (Ya zamani)
 
Akupendaye kakulewa -Mpya

Kunywa si kulewa - Zamani

Ulevi hauoni kasoro - Zamani

Mlevi haoni soo - Msemo wa manzese.
 
machozi yako leo, uliyapanda jana,
machozi yako ya kesho, unayapanda leo,
Apandaye anasa, atavuna machozi,
 
Asiyeweza kuongozwa hawezi kuongoza,

Asiyeweza kufundishwa hawezi kufundisha.
 
Kila nabii na majira yake, na jamii yake, na ujumbe wake,
 
Mwanamke ni mwanaume mwenye kichwa kimoja,

Mwanaume ni mwanamke mwenye tumbo moja,
 
Maskini akinenepa, amenawiri,

Tajiri akinenepa, amedhoofu.
 
Back
Top Bottom