Nimebaini mke wangu ana laini mpya

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,485
99,223
Wakuu

Leo nikiwa bize sana dukani, nakuja kustuka Simu yangu ya private ina missedcall namba ngeni ya tigo inaishia na 900, ikabidi kuipigia haraka.

Simu imepokelewa, sauti ni ya wife, namuuliza vipi naona ulinipigia, Akasema sijakupigia. Nikamuuliza namba ya Nani Hii, mbona unatumia namba ngeni?. Akasema " sio namba ngeni, ni laini yangu ya Siku zote". Nikamwambia "sawa, nenda Kwenye point, ulikua unasemaje"

Akasema " Nlkupigia, nilitaka kukuuliza nikuhesabu chakula, utakuja kula?" Nikamuuliza "Ni lini nmewai kuja kula chakula Cha mchana nyumbani. Kwangu? Au umekosea namba?"

Akasema "nakoseaje namba yako mme wangu, kwani Kuna ubaya gani kukuuliza?" Nikamwambia "hamna ubaya, tatzo Hii namba ngeni ulonipigia, pia mazunguzo unayoleta Ni Kama hayanihusu Mimi" akahamaki.

Nikaongezea "Unanikaribishaje chakula Cha mchana na unajua kbs sijawahi kurudi mchana kula Lunch nyumbani?" Akasema "Basi yaishe, naona umekasirika mme wangu". Nikamwambia "sawa" Kisha nkakata Simu.
 
Baada ya kukata Simu,machale yakanicheza sana. Nkaamua Kwenda nyumbani MDA huo huo, nmefk namkuta wife sebleni kashika Simu akitizama tv na shemej yangu (mdg wake wa kike).

Nmemuita chumbani kaja, nmemkalisha chini nikamwamvia anikabidhi Simu yake,Kisha nkamwambia "nataka kujua khs hii laini ngeni ulonipigia leo". Akasema "sio laini yangu, Ni laini ya kijana wetu wa ng'ombe, aliazima Simu yangu kubwa mara Moja ili awapigie videocall ndugu zake,ndo kasahau kuitoa"

Nkamwambia "kwaiyo iko wapi Hii laini" akasema "nishaitoa iko kwny kava la Simu, funua utaiona" nmefunua kweli nmeikuta. Ikabd kuiweka kwenye kisimu changu Cha tochi kuikagua.

Katk kuikagua, nikakuta haina sms yyt,ila Ina majina 9 yote yameseviwa majina ya ndugu na shoga zake wife. Nkahisi huyu ananidanganya, haiwezekani laini iwe ya kijana wa ng'ombe, afu phone book iwe na majina ya ndugu zake na shoga zake wife nnaowajua mimi. Ikabd kumfata kijana nmuulize.
 
Nmetoka chumban nmeelekea Banda la uani kwa kijana na kumuuliza kijana, . "Dogo unazo laini ngapi? kuna laini ya tigo Inaishia 900 imenipigia sio mda inajitambulisha Ni wewe , Ni ya kwako? " Dogo kasema "hapana bro,hao watakua Ni matapeli, namba ninazo 2 tu Voda na Airtel, hiyo ya tigo ndo naiskia kwako. Vipi wanasemaje, wamekuomba Ela au vipi?"

Nikamwambia "ndo zao hizo,ila sjawapa pesa" Basi tukaagana nikarud kwangu,chumban na kumwambia wife kwamba "Wee Ni mwongo, Hii laini sio ya kijana,nmeuuliza kaikana, usinipotezee muda, nataka majibu yanayoeleweka Nini kinachoendelea khs hii laini"

Akaanza kulalamika inakuaje kamkana, kanambia twende wote Hadi kwa kijana, tumerud kwa kijana.
Wife anamshutumu kijana kwann kaweka laini kwny Simu yake na anaikana, anamtaka aseme ukweli kwamba aliazima akaweka lain yake na kasahau kuitoa. Nkamwmabia wife afunge mdomo, mbona kama vile anampangia Nini Cha kusema kijana.

Nkamuuliza Kijana,
"Dogo unamiliki laini yoyoye ya tigo inayoishia na 900?" Kijana Kasema hapana. Nkamuuliza Tena kijana, "uliwai azima Simu ya MKE wangu ukawapigie video call ndugu zako?".
Kijana Kasema "niliazima kweli, ila Ni juzi sio leo".

Nkamuulza Tena, "unawafahamu flani na flani na flani (majina yaloseviwa kwny ile laini). Kijana kajibu "hapana, ndo nayaskia leo hayo majina".

Nkamwambia, "hayo majina nlokutajia yaliseviwa kwny laini inayodaiwa kua Ni yako, ndo nataka unihakikishie unayajua huyajui?" Kijana Kasema "hapana siyajui". Nkamwambia kijana Asante, Kisha Nikamwambia wife turud chumbani. Wife akapanic na kuanza kumfokea kijana. Nkawaacha nmerud zangu chumbani
 
Punde nae wife kafika chumbani kapanic,analalamika Inamaana simuamini yeye MKE wa ndoa, namwamini kijana wa ng'ombe?

Nikamwambia "sio kwamba sikwamini, unachonambia hakiingii akilini. Kuanzia namna ulvonipigia Simu, Hadi kudai laini Ni ya kijana. Yaani laini ya kijana wa ng'ombe ikaseviwe majina ya ndugu zako na shoga zako, afu uyo uyo kijana asitambue hata jina Moja kwenye laini inayodaiwa Ni ya kwake. Hapa Kuna kitu kinafichwa."

Akasema,
"Hayo majina sijayakana,Ni yangu, Simu yangu ilkua mtu akipiga haileti majina kwenye kioo, ndo nikaamua kua nayasevu kila wakipiga" nkamuuliza "umeanza kuyasevu lini hayo majina?" Akasema "leo leo wote walkua wakinipigia Simu haileti majina".

Nkarejea kwenye Simu yake kubwa na kuangalia kwenye call records kuangalia majina yote 9 kwenye ile laini ya 900 Kama kweli namba zile 9 zote zilipiga. Nkakuta tangu mwezi wa 10 hamna hata Moja ilopiga,missedcall Wala kupokelewa kupitia Simu kubwa. Nkajua uyu mwanamke ananidanganya.

Nkamwambia wazi wazi
"wee mwanamke Ni mwongo, afu ujui unamdanganya mtu namna gani, humu kwny Simu yako hamna call yyt inayohusiana na hzo namba ulizosevu humu, vinginevyo useme uwa unatumia simu tofauti kuzipigia hizo namba zako. Na nataka niione hiyo Simu Sasa hivi" Akasema Hana Simu tofauti na hiyo.

Basi nikaona ananipotezea MDA,
Nmeondoka pale na kurud kuendelea na shughuli zangu. Lakini kichwan najua Kuna kitu hakiko sawa khs MKE wangu.

Hatua nilizochukua mpk sasa,
1. Nmeanza rasmi kuzifanyia uchunguzi namba Moja baada ya nyingine zilizoseviwa kwny Hii laini.

2. Nmeangalia usajili wa laini, namba imesajiliwa jina la kiume la kiislamu, nataka nianze kumfatilia kumjua mtu huyu Ni Nani.

3. Nmemuuliza mdg wake wa kike wife khs hizo laini (baadae asije geuza kibao Akasema laini za mdg wake), keshanambia haitambui laini Kama hiyo.

4. Kiukweli iman kwa MKE wangu imepungua mno, na kwa hili ntaanza kumchunguza kimya kimya Bila kupanic.

MWENYE MAWAZO,USHAURI AU MAONI TOFAUTI NAwaKARIBISHENI.

Nawasilisha
 
Mkuu ndoa yako ina muda gan
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom