Meremeta & TANGOLD Revealed!

Ni taathira ya mambo
Si bishara za tambo
Kwani toka kitambo
Twalisema hili jambo


Likilia la mgambo
Jua hapo kuna jambo
Kinazama hiki chombo

Wenye mpini wa mambo
Wasema hatuna nyimbo
Haki inachapwa fimbo.

Kama watoto wa kambo
Tunaachiwa makombo
Uchumi wavushwa ng'ambo

Na: Gamba la Nyoka, a.k.a(Kombeo la Daudi)
 
Ni taathira ya mambo
Si bishara za tambo
Kwani toka kitambo
Twalisema hili jambo


Likilia la mgambo
Jua hapo kuna jambo
Kinazama hiki chombo

Wenye mpini wa mambo
Wasema hatuna nyimbo
Haki inachapwa fimbo.

Kama watoto wa kambo
Tunaachiwa makombo
Uchumi wavushwa ng'ambo

Na: Gamba la Nyoka, a.k.a(Kombeo la Daudi)

swadaktaaa!
 
Dear Sita na Pinda!

kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,
naam, viko saba vilivyo chukizo kwake

macho ya kiburi, ulimi wa uwongo,
na mikono imwagayo damu isiyo na hatia

moyo uwazao mawazo mabaya
miguu iliyomyepesi kukimbilia maovu;

Shahidi wa uwongo asemaye uongo;
naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu

Kazi kwenu!
 
na ndio maana zikawa siri na kama umefanikisha kujua Imani yangu hata wenyenazo tayari umewajua! kaza buti kumalizia
 
Jeshi hili ni la nani, mimi nauliza nini,
La nini tena kwanini, mwenye kujibu ni nani
Nauliza kwa makini, mtanipa jibu gani,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Meremeta ni ya nani, Mkuu tuelezeni,
Twataka mtangazeni, tujue wazi kwanini,
Mnachotuficha nini, mnamuogopa nani,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Mnatuzuga kwanini, kwa majibu yalo duni, (mbadala- "ya kihuni")
"Tusiseme hadharani", mwatung'akia Bungeni,
Hivi nyinyi kina nani, mnatuona wageni,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Ati wabunge "nyamazeni, serikali ni makini,
Mambo haya ya sirini, hatutawajulisheni,
Mengine yajadilini, Meremeta iacheni,"
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Si kura tuliwapeni, mtuwakilishe Bungeni,
Kimya chenu ni cha nini, mnaburuzwa na nani,
Mbona mwagwaya kwanini, vigugumizi vya nini,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Mwamunyange ndiye nani, Jeshi lake ndiyo gani,
Sumari yeye ni nani, Jeshi ni la nchi gani,
Walipa kodi ni nani, Jeshi linaitwa nini,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Walioiba kina nani, wakijificha jeshini,
Ni usalama wa nani, mbona hatuambiani,
Na usalama wa nini, nawauliza semeni,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Nasema nyinyi kubalini, Meremeta ni uhuni,
Uchafu umilikini, na bora jisafisheni,
Mtatuficha mpaka lini, hamtaweza jamani,
Siri hizi ni za nini, zanani, tena kwanini?

Kagoda nayo ninini, Dipu girini magirini,
Mwanchi goldi ya nani, Tanigolidi ya nini,
Haya yote mpaka lini, nauliza kijiweni,
Siri hizi ni za nini, zanani, tena kwa nini?

Mtakula mpaka lini, mtavimbiwa jamani,
Kula huku kula gani, ni njaa namna gani,
Bila kunawa watani, hadi ndotoni kwanini,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Watoto waje kula nini, na mnakomba chunguni,
vidole mwavilambani, njaa haiwaisheni,
Uraiani na jeshini, mwamega na kumegani,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Jembe ninaweka chini, wamenikera mtimani,
Dharau yao ya nini, mipasho nayo ya nini,
Watapeta mpaka lini, atawazuia nani,
Siri hizi ni zanini, za nani, tena kwa nini?


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Mkjj. ahsante sana kwa shairi zuri sana ambalo limegusa uozo uliojaa ndani ya bunge letu. Uozo huo ni ule unaongozwa na spika wa Bunge Sitta. Nilishawahi kusema hapa jamvini kwetu kwamba Sitta ni mtetezi mkubwa wa ufisadi na mafisadi ndani ya bunge letu uchwara hili kamwe siyo bunge tukufu maana halina utukufu wowote kwa kuficha madhambi mbali mbali yasijadiliwe na wawakilishi wetu tuliowachagua.

Kama lingekuwa ni nunge tukufu basi siku zote lingeweka mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania badala yake limeweka mbele maslahi ya mapapa wa ufisadi ambao bado wamejaa ndani ya Bunge hili uchwara akina Rostam na wenziye na maslahi ya chama cha mafisadi na pia lisingezuia mijadala muhimu kama ya vitambulisho ambalo pia Sitta lizuia swala hili lisijadiliwe bungeni kwa visingizo ambavyo havina kichwa wala miguu.

Jeshi kazi yake ni kulinda mipaka ya nchi yetu kuhakikisha nchi yetu haingiliwi na adui yoyote yule ili kuleta purukushani ndani ya nchi yetu. Hata siku moja Jeshi halikupewa na wala halistahili kupewa kazi yoyote ile kuhusiana na madini yetu? Je, kulikoni mpaka jeshi likaingizwa kujihusisha na mambo ya madini? Ni nani huyo aliyeamua kwamba Jeshi letu lijishughlishe na migodi ya Buhemba na na kampuni ya Tangold? Ni fisadi Mkapa au serikali yote? Kwanini hili linafichwa kwa juhudi kubwa sana na waliomo serikalini? Wanajaribu kutuficha nini Watanzania wanaposema kwamba maswala ya Meremeta na Tangold yanagusa usalama wa Taifa, kwa nini hawasemi kweli kwamba maswala ya Meremeta na Tangold yanagusa mapapa wa ufisadi na wakiguswa nchi itawaka moto?

Kwa mara nyingine, serikali juzi ililieleza Bunge kuwa masuala yanayohusu kampuni ya Meremeta hayawezi kujadiliwa kwenye chombo hicho cha wawakilishi wa wananchi kwa kuwa yanahusu usalama wa nchi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kauli hiyo hapo juu inaonyesha dhahiri kwamba ufisadi hautakwisha Tanzania kwa sababu kuna watetezi wa nguvu wa ufisadi na si ajabu kuanzia sasa ufisadi wote utakuwa ukipitishiwa jeshini na hakuna atayefunua mdomo kutaka ufisadi huo ujadiliwe kwa kisingizio kwamba unahusu usalama wa mafisadi wenyewe wanasema unahusu usalama wa Taifa.

Hongera sana shujaa wetu Dr Slaa kwa mara nyingine kuwa sauti pekee ndani ya Bunge kutafuta haki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya ufisadi mbali mbali unaofanywa na chama cha mafisadi na wale waliomo serikali. Daima tutakumbuka juhudi zako za kuweka maslahi ya Tanzania na Watanzania mbele. Mwenyezi Mungu akupe afya njema na maisha marefu ili uendelee kuutangazia umma wa Watanzania uozo mbali mbali uliokithiri ndani ya chama cha mafisadi na serikalini.

Mungu ibariki Tanzania

Alutta Continua
 
Mimi nasema kutogusa Meremeta ni kuendekeza utawala wa kifisadi.

Date::6/23/2009
'Kutogusa Meremeta ni kukiuka utawala bora'

Na Salim Said
Mwananchi

UAMUZI wa Serikali kuzuia kujadiliwa kwa kampuni ya Meremeta Gold Mine umeelezwa kuwa ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora, wanaharakati na wanasiasa wameeleza.

Kwa mara nyingine, serikali juzi ililieleza Bunge kuwa masuala yanayohusu kampuni ya Meremeta hayawezi kujadiliwa kwenye chombo hicho cha wawakilishi wa wananchi kwa kuwa yanahusu usalama wa nchi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari alitoa tamko hilo akirejea kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa bungeni mwaka jana kuwa suala hilo haliwezi kujadiliwa na kuwataka Wabunge waheshimu kauli hiyo ya mtendaji mkuu wa serikali.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, ambaye aliuliza swali la msingi, alipotaka kueleza kuwa, anachohoji ni wizi, Spika wa Bunge, Samuel Sitta alimkatisha na kumwambia kuwa walishakubaliana katika kikao cha kamati ya maadili ya viongozi kuwa suala la Meremeta lisijadiliwe hadharani kwa sababu za kiusalama.

Jana mratibu wa masuala ya utawala bora wa Mtandao wa Mashirika ya Wanaharakati (FemAct) ambao unaunganisha taasisi 50, Buberwa Kaiza alisema jana kuwa, kitendo hicho kinajenga taswira kuwa dola inashabikia ufisadi.

Alisema katika nchi yoyote inayofuata misingi ya utawala bora, hakuna jambo linalopaswa kuendeshwa kwa usiri hasa jambo hilo linapohusu wizi wa mali ya umma na kwamba kuzuia Meremeta kujadiliwa hadharani ni kukiuka kanuni hizo.

"Katika utawala bora hakuna siri na matumizi ya fedha za umma yanapaswa kuwekwa hadharani," alisema Kaiza.

Alisema ni jambo la kushangaza kuona Bunge ambalo ni sehemu pekee ya haki ya kuzungumza na kujadili masuala ya maendeleo ya nchi, hasa matumizi ya fedha za umma linazuiwa kujadili kampuni hiyo ya Meremeta kwa kigezo cha ulinzi na usalama wa taifa.

Kaiza, ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Fordia, alisema: "Hii ni ishara ya nchi kutekwa na mafisadi kwa sababu serikali imeamua kuwatetea kwa nguvu zote watu wachache wanaotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma."

Kauli ya Buberwa iliungwa mkono na katibu mkuu wa Chama cha NCCR- Mageuzi, Samwel Ruhuza aliyetaka kampuni hiyo ijadiliwe kwa sababu imetuhumiwa kwa ufisadi ambao hauna uhusiano na usalama wa taifa.

Ruhuza alisema licha ya kuwa suala la Meremeta linalohusisha usalama wa taifa, serikali inatakiwa kutambua kuwa kampuni hiyo inahusika na ubadhirifu wa fedha za walipakodi.

"Hivi mfanyakazi wa usalama wa taifa akiiba hataulizwa wala kushtakiwa?" alihoji Ruhuza

"Suala la msingi hapa ni ubadhirifu... hayo ya usalama yasijadiliwe, lakini hili la ubadhirifu lazima liongelewe."


Kwa mujibu wa Ruhuza, inaeleweka kuwa fedha nyingi za walipakodi zilitolewa na kupelekwa Meremeta, hivyo serikali haina sababu za kuzuia suala hilo kujadiliwa hadharani kwa kuwa linawahusu wananchi.

"Mimi sina haki ya kujua kama jirani yangu anamiliki bunduki au la, lakini ikitokea mtoto wangu amekutwa ameuawa nje ya nyumba ya jirani yangu, hapo lazima niulize ili nipate ufafanuzi na maelezo sahihi juu ya kifo hicho, sasa suala hili ndio mfano halisi wa hii kampuni ya Meremeta."

Kauli hiyo ya serikali imekuja wakati Bunge likiwa limemwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), kuikagua Meremeta pamoja na Mwananchi, ambayo imeelezwa kuwa iko katika mchakato wa kufilisiwa na kwamba itajadiliwa baada ya kumalizika kwa zoezi hilo.

Inadaiwa kuwa, wanahisa wa Meremeta, ambayo ilipewa kiasi cha Sh155 bilioni na Benki Kuu (BoT) katika mazingira yanayoonyesha kuwepo kwa ufisadi na mtuhumiwa, ni kampuni ya Trienex ya Afrika Kusini ambayo inamiliki asilimia 50 na Hazina (50%).

Wanahisa wengine wa kampuni hiyo inayodaiwa kuwa ilianzishwa jijini London, ni London Law Secretary Services. Ilidaiwa Bungeni kuwa kampuni ya Tangold ndiyo iliyorithi mali za Meremeta baada ya kampuni hiyo kuwa mufilisi.

Habari hii imeandaliwa na Salim Said na Fidelis Butahe
 
Dear Sita na Pinda!

kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,
naam, viko saba vilivyo chukizo kwake

macho ya kiburi, ulimi wa uwongo,
na mikono imwagayo damu isiyo na hatia

moyo uwazao mawazo mabaya
miguu iliyomyepesi kukimbilia maovu;

Shahidi wa uwongo asemaye uongo;
naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu

Kazi kwenu!

aisee asante sana na hilo la kutoka Mithali. Ni wimbo wangu niupendao sana!
 
Mara ya mwisho niliposoma jina la Jeshi letu lilikuwa linasomeka "JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA" - na kwa kimombo "Tanzania People's Defence Force"

Sasa najiuliza:

a. Ni lini jeshi letu liliacha kuwa la Wananchi wa Tanzania na kuwa Jeshi la Serikali ya Tanzania?

Mwenye contact za Mwamunyange au au msemaji wa Jeshi hilo naomba mnipatie. Tafadhali.

Kwenye website ya serikali nadhani utapata namba hizo.
 
Siri sasa zimekuwa nyingi tena cha kusikitisha ni siri za serikali dhidi ya wananchi wake. Naona hatutaki kujifunza nini yatakuwa matokeo ya kuendelea kufanya kila kitu tulichovulunda kwa manufaa ya watu wachache serikalini kuwekwa kama ni siri. Ni kweli inaonekana safari ya mabadiliko bado ndefu. Lakini naamini tutafika tu.Dalili zinaanza kuonekana
 
:D:D:D:D:D:D Huwa nikiwaza nacheka sana. Yaani mambo ya jeshi ni siri kwetu wananchi lakini kwa walanchi na nje ya mipaka ya nchi yetu si siri hata kidogo.

Hawa hawa viongozi wetu wanapanga kununua vitu vya kijeshi kwa bei kubwa na tena vibovu. Hapo hakuna siri.

Wanaingiza jeshi kwenye ubia na kampuni za kigeni kwenye miradi ya jeshi eti ni siri? hahahahahahahahahahah uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Wanaajiri mpaka foreigners kuendesha mambo fulani fulani ya kijeshi hapa kwetu. Hapo hakuna siri. Lakini ikija kwa mtanzania mdanganyika kutaka kujua nini kinaendela, hapo ni siri kabisa. Hizi siri hizi siri zina mambo.

ngoma ivumayo ina mwisho plz.

Ama kweli usipoona ya Musa utaona ya Farao. Wabunge wetu ni vichwa wazi au wamelogwa?

Ggggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhhh
 
wanatuona wananchi wote mabwege, ipo siku.

ni kweli silaha yao ni wengi ambao hawapati taarifa sahihi ya yanayoendelea na hii yote ni kutokana na umasikini zaidi
 
Tuchunguze wenyewe. Tuyaweke wazi mambo haya. Serikali imeshasema haitayaweka wazi mambo ya Tangold, Meremeta,....Kazi kwetu wenye UCHUNGU na MALI/RASILMALI za Nchi yetu.
 
Mara ya mwisho niliposoma jina la Jeshi letu lilikuwa linasomeka "JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA" - na kwa kimombo "Tanzania People's Defence Force"

Sasa najiuliza:

a. Ni lini jeshi letu liliacha kuwa la Wananchi wa Tanzania na kuwa Jeshi la Serikali ya Tanzania?

Mwenye contact za Mwamunyange au au msemaji wa Jeshi hilo naomba mnipatie. Tafadhali.

si suala la jeshi wala usalama wa taifa!!! ukweli ni kuwa hawana majibu. kampuni inayoambiwa ni nyeti imesajiliwa nje ya nchi na kuna kampuni ya kigeni ina hisa 50%! je usalama wa taifa umebinafsishwa?
 
Mara ya mwisho niliposoma jina la Jeshi letu lilikuwa linasomeka "JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA" - na kwa kimombo "Tanzania People's Defence Force"

Sasa najiuliza:

a. Ni lini jeshi letu liliacha kuwa la Wananchi wa Tanzania na kuwa Jeshi la Serikali ya Tanzania?

Toka mawazo ya kifisadi ya kuanzisha Meremeta, Rada na Helikopta yalipokubalika na wakulu
 
It is rather ridiculous!! mtu anaulizwa ametumiaje hela ya Wananchi, jibu analotupa ati ni siri,lakini kinachoulizwa ni legitimacy ya kutumia hela na inaonekana kuna ujanja/wizi umefanyika sasa kama bunge haliwezi kuambiwa matumizi yetu yakoje ni nani mwingine anayewakilisha interest za watanzania?

Mimi naomba Spika atoe kibali bunge liende kwenye closed session kwamba sisi wengine tusijue wabunge wamekula kiapo hivi waelezwe kwa undani na umakini alafu wao watapima kama ni usalama wa nchi ulikuwa at stake or wa CCM or wa Ikulu peke yake kwa maana watu walikwiba ili ipatikane hela ya Campaign au ni wizi tu kama wa EPA lakini kusema ati tusizungumze wala kuuliza kwa sababu Pinda alisema hawezi kusema!!

Ni kutetea wizi nami siamini kama bunge zima liko pale kulinda wizi wa watu wachache.

Mungu Ibariki Tz watu wafunguke macho na haki itendeke.

Mkuu tupo pamoja. Hii siri anayeitunza ni nani na kwa faida ya nani? masikini mlipa kodi kodi yake itumike halafu akitaka kujua imetumikaje anaambiwa ni siri! iko siku nayo yaja nayo imekwisha kuwadia ambapo hao wanaoseme ni siri watakuja kusema hadharani kwamba haikuwa siri ila.....
 
Back
Top Bottom