Meremeta & TANGOLD Revealed!

mi nafikiri hawa wapumbavu huo usalama wa taifa wanao-refer ni marungu, mawe, magobore yatakayo piga hodi hadi ikulu.wanahofia watu watawatoa macho waliofanya biashara wakiwa madarakani.. huo ndio usalama pekee wanaofikiria washenzi hawa... yaaani nina hasira kuliko maelezo.. mzee ndiyo maana sitaki siasa naweza kumtoa mtu roho.
 
Jamani ilishasema IGP Mwema kwamba:'kuna baadhi ya watu kama wataguswa/kupelekwa mahakamani,basi nchi itatikiswa' sasa which part of his statement don't we understand yet??????
You stand to be correct, wizi huu ulifanywa na Raisi Mstaafu kwa kuwashirikisha Wakuu wa Usala, kuanzia Mkuu wa Majeshi JWTZ etc, ndio huo usalama wa Taifa usioweza kujadiliwa
 
Wanabodi hivi sheria zetu zinazohusiana na Usalama wa Taifa (constitutional safeguards) zinatungwa wapi! au hatunaaa!

Kisha ningependa kuelewa zaidi huu Usalama wa Taifa unaohusiana na machimbo ya dhahabu ni Usalama gani!

Jeshi la wananchi ni chombo cha Ulinzi - a defence force, kisichohusiana kabisa na maswala ya mining iweje wasajili kampuni ya uchimbaji madini kwa kutumia jina la jeshi tena basi wasifanye nyumbani likasajiliwe nje ya nchi Uingereza (an offshore company), halafu walipwe na Benki yetu BOT kiasi cha billioni 155 (wakati huo dollar 1 kwa Tsh. 900), bila mauzo wala kubadilishana mikono, fedha za wananchi leo tuambiwe ni swala la Uslaama wa taifa..

Jamani jeshi letu kuwa na kampuni ndani ya nchi za watu kwa siri kama shirika la madini hii imekaa sawa kweli hata kama kuna usiri usiri gani zaidi ya kuvunja sheria!.. Waingereza wangefahamu kwamba tunatumia shirika hilo ku spy nchi yao tutasema nini?..hao waliofikiria hili tu wanatakiwa watueleze huo Usalama ni usalama gani kama sii kujenga Uadui na nchi nyingine!

TPDF hawahusiani kitu na Usalama wa Taifa, unless wanataka kutuambia bomu hili likifumka litahatarisha Usalama wa Taifa, watueleze.. lakini pamoja na yote hayo bunge letu ni sawa na senate wanatakiwa kujua usiri uliopo ili wapate kupiga kura au laaa Rais anaweza ku veto lakini sio swala la waziri mkuu kupindisha sheria za Bunge wakati kuna fedha za wananchi zinazotakiwa maelezo...Billioni 155 zinatakiwa kuwa accounted for...serikali haiwezi ku brush off hoja kama hii kwa visingizio vya Usalama wa Taifa hali Meremeta ni Mining Company ambalo sii shirika la lililosajiliwa Tanzania..

Hata kama serikali ilikusudia kufungua shirika lake nje la kuuza share kwa ajili ya exploration na uchimbaji wa dhahabu wakalisajili ktk soko huria la UK, bado wananchi tunatakiwa kufahamu hakuna siri nchi nyingi zinafanya hivyo na pengine itatupa nguvu Watanzania kununua share zetu ktk shirika hilo isipokuwa kama kuna usiri ambao unaambatana na dhahabu zetu kinyume cha majukumu ya jesahi nadhani Watanzania tuna kila haki ya kufahamu kinachoendelea na haswa zile billioni 155 zilitumika vipi...

Na kama sikosei hii haikuwa mara ya mwisho..Mama Meghji pia alisema marehemu Balali (maelezo baada ya kifo cha Balali) kuwa alimtumia barua kuidhinisha fedha kibao akidai kuwa swala lilikuwa ni la Usalama wa Taifa! kisha akakubali ati alidaganywa!..Je, ni mara ngapi hili neno Usalama wa Taifa limetumika kuiba fedha za wananchi toka Benki kuu?..

Angalia basi hilo swala la Mwananchi Gold ni cha mtoto kabisa tena lina maelezo na ushahidi (evidence) ndilo wanataka kuliwekla wazi wakijua fika litakwisha kirahisi..Kisha wanatufanya sisi wajinga sana wakisema kwa kusisitiza ati ni swala la muda tu wakati sisi tunajua fika kwamba wanasubiri wakati muafaka kwao (uchaguzi) kuliagusha mahakamani, kwa madai kuwa serikali inafanya kazi yake kupigana na ufisadi hali Mapapa wamekwenda zaana kwenye coral reefs visiwani..baada ya uchaguzi tu...kesi zinazimwa, tunaanza upya na kelele za mlangoni....

Ama kweli NDIVYO TULIVYO!
 
Last edited:
You stand to be correct, wizi huu ulifanywa na Raisi Mstaafu kwa kuwashirikisha Wakuu wa Usala, kuanzia Mkuu wa Majeshi JWTZ etc, ndio huo usalama wa Taifa usioweza kujadiliwa

Gen. Robert Mboma anahusika pia ktk hii issue na ndipo mambo ya vifaru hwea na helkopta feki viliingia.....
 
Ukweli juu ya what happened with the so called Meremeta unajulikana na Dr. Slaa alikuwa anauliza ili kusikia uongo wa serikali juu ya hili suala. Lakini soon or later suala hili litawekwa wazi na kila mtu atajua what actually transpired. Usalama wa Taifa ni neno linalo tumika kutaka kuzima hoja lakini hakuna siri yoyote ambayo wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hawapashwi kujua. Usalama unaozungumziwa hapa ni usalama wa wezi wa pesa za walipa kodi na si vinginevyo.

Tiba
 
Hata Marehemu Balali alipoulizwa kuhusu namna mshiko wa EPA ulivyotolewa alijibu ilikuwa ni kwa ajili ya USALAMA WA TAIFA. Kwa kauli hiyo hata Mama Zakia alijiingiza kichwa kichwa na kusema hivyo japo baadae alichomoa. Swali la kujiuliza ni kwa nini Spika alikataa majibu hayo kutolewa Ijumaa kama ilivyotakiwa? Ama ilibidi wakaombe ushauri kutoka kwa Mkuu wa Kaya! Waendelee kutudanganya lakini naamini ni vigumu sana kusimamia uongo na kila lifanywalo kwenye giza, panapo mwanga jambo hilo litaonekana tu.
 
Haya sio majibu kwa mtu mwenye akili timamu. Viongozi wetu naomba muwe wajasiri kama kuna wizi kama inavyohisiwa basi waliousika washughulikiwe. Msiogope. Kama upo wizi halafu unasema ni USALAMA WA TAIFA? eti PM ameshasema hivyo, kwani ndiye mawaziri mmelazimishwa mseme kama alivyosema PM?

Haijakaa vizuri mbele ya macho ya umma.
 
Ni kichekesho serikali kusema wizi hauwezi kujadiliwa kwani umefanywa na Usalama wa Taifa. Hakuna sheria inayoruhusu Usalama wa Taifa au JWTZ kuiba.

Yaani Bunge limwagize CAG akakague shirika lililodaiwa kuiba fedha za umma, kisha serikali isema hakuna ruhusa? Katiba ya Tanzania inasema Bunge litasimamia shughuli za serikali. Ni uvunjaji wa katiba kwa serikali kukataa Bunge kukagua idara zake.

Kwa vyovyote vile, tunapigia mbuzi gitaa. Haiwezekani viongozi waliochota mabilioni ya wananchi wakajifunga wenyewe. Ni mpaka CCM itakapokaa benchi ndipo ukaguzi wa wizi uliofanywa na viongozi wake utawezekana. Najua Slaa anafahamu hivyo. Anavyouliza maswali yake, ni vizuri tu kwani ni namna mojawapo ya kuhamasisha wananchi ili wakubali kuiweka CCM benchi. Then, and only then, ukaguzi wa dhati utafanyika na wezi wa mali ya wananchi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Ikiwa swala la Jeshi linaweza kuuzwa kwa kampuni yenye hisa nusu this means hiyo kampuni inazifahamu siri za jeshi. Kama kampuni inaweza kufahamu vipi bunge letu linyimwehaki ya msingi? yaani wageni wajue siri za jeshi sisi tunyimwe! Hapo serikali mmechemsha. ... Ni wizi tuu na lazima itakuja kujulikana. Iwe leo au kesho. Wahusika mjiandae!
 
Ni kichekesho serikali kusema wizi hauwezi kujadiliwa kwani umefanywa na Usalama wa Taifa. Hakuna sheria inayoruhusu Usalama wa Taifa au JWTZ kuiba.

Yaani Bunge limwagize CAG akakague shirika lililodaiwa kuiba fedha za umma, kisha serikali isema hakuna ruhusa? Katiba ya Tanzania inasema Bunge litasimamia shughuli za serikali. Ni uvunjaji wa katiba kwa serikali kukataa Bunge kukagua idara zake.

Kwa vyovyote vile, tunapigia mbuzi gitaa. Haiwezekani viongozi waliochota mabilioni ya wananchi wakajifunga wenyewe. Ni mpaka CCM itakapokaa benchi ndipo ukaguzi wa wizi uliofanywa na viongozi wake utawezekana. Najua Slaa anafahamu hivyo. Anavyouliza maswali yake, ni vizuri tu kwani ni namna mojawapo ya kuhamasisha wananchi ili wakubali kuiweka CCM benchi. Then, and only then, ukaguzi wa dhati utafanyika na wezi wa mali ya wananchi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mkuu nakubaliana na wewe! inabidi wapumzike. Nafikiri imefika nafasi ya wao kukaa benchi waone mechi pengine wanaweza kufahamu makosa yakwapi! Na hata Spika japo na mkubali lakini wakati mwingine kuna maamuzi anayoyafanya yanaashiria kukibeba chama. We need impartial speaker, who of course belongs to no political party.

At least, even if theoretical, will some how help. having CCM speaker, who is leading the National assembly and at the same time the same CCM is the one forming government, that speaker being neutral is a bit kind of dream or more theoretical piont.
 
Hivi mawaziri hawa na wabunge ambao wamebaki kuwa mabubu kuhusu upotevu wa mabilioni haya siku zao zinahesabika tutaweka ndani wote na kutaifisha mali zao.Wamefanya wizi kweupe wanakuja wanatudanganya eti swala la jeshi kwa hiyo jeshi wakifanya ufisadi wasishitakiwe?
 
Njia ya muongo ni fupi.Tunalea uongo ili matatizo yetu yasing'amuliwe na kuweza kujirekebisha, baadae unakuja kutuumbua kama ilivyotokea bunge la afrika
 
Hawa mawaziri watudanganye na kutufanya kama wote wajinga, ila watambue kuwa with time haya mabo yote yatakuja julikana wazi na wahusika wote wataumbuka.
 
Ukweli ni kwamba, jitihada zozote zinazofanywa na serikali kuzuia mijadala ya Meremeta ni sawa na kuahirisha tatizo. Nijuavyo mimi, kuahirisha tatizo hakulipunguzi tatizo lenyewe bali kunaliongeza. Matatizo hukua, si kusinyaa (kama hayatafutiwi suluhu). Serikali kuzuia mijadala ya Meremeta kwa visingizio hafifu vya usalama wa Taifa ni kuonyesha kuwa wamepungukiwa sense of responsibility, accountability na loyalty kwa Katiba na wananchi waliowachagua. Haki ya nani, hawatafika mbali na hili. Litaendelea kutafuna vichwa vyao, roho zao mpaka watakapoamua kuliweka bayana na kulifunga kwa ukweli na umakini unaostahili.

Hoja kuwa Meremeta haijadiliki ni hoja chafu na changa. Haitoshi kwenye akili ya mtu mzima na mstaarabu yeyote. Sababu zake ni kama zifuatazo;

1. Meremeta haikuwa kampuni inayoshughulika na masuala ya kijeshi hata kidogo. Hivyo ilikuwa na waajiriwa ambao wengi wao ni raia wa kawaida, watu kutoka mataifa mbalimbali n.k. Hivyo haikuwa ikilinda usalama wa Taifa letu wala taifa lolote zaidi ya kufanya biashara

2. Meremeta imechukua pesa kutoka BoT ambazo zinatakiwa kukaguliwa. Ingekuwa wame-generate wenyewe pesa hizo ama wamezipata kutoka kwenye vyanzo vingine visivyohusiana na hazina yetu, wangeweza kudai kuwa haijadiliki. Inatakiwa tujue pesa za wananchi masikini wa nchi hii zinatumikaje na kwa manufaa gani. Ni haki yetu wote tunaolazimika kulipa kodi na kukaza mikanda ya maisha. Si haki wala ustaarabu kwa pesa za wakulima na wafanyakazi kuibiwa na kuishia kuambiwa kuwa zimetumika kwa usalama wa Taifa. Zilipitishwa na Bajeti gani?

3. Ni kivipi suala la Meremeta linahusiana na Usalama Wa Taifa? Bunge linayo haki walahu ya kujua uhusiano uliopo kati ya JWTZ na Meremeta, na vile vile uhusiano kati ya Meremeta na usalama wa Taifa letu. Baada ya hapo, ndipo tujulishwe usalama huo umelindwa kwa kiasi gani katika kutafuta wabia wa kushirikiana na Serikali/Jeshi katika uundwaji wa Meremeta.

4. Ni kivipi serikali inaweza kushawishi bunge na wananchi kuwa, uwezekano wa kutumia pesa za hazina yetu kwa manufaa ya wachache haupo tena kama ilivyotokea kwa Meremeta? Ina maana kama suala hili lisipojadiliwa, viongozi wataona mwanya wa kupitisha pesa za nchi hii na kuzichukulia jeshini kwa kuwa zitakuwa zimetumika kwa usalama wa Taifa, hivyo ni lalali kufanya hivyo na hazikaguliwi.

5. Naomba nielimishwe kidogo tafadhali: Hivi kwanini jeshi lisikaguliwe? Yaani hata wanaojihusisha na jeshi pia hawakaguliwi? Ni majeshi yote yako hivyo? Mbona tunasikia kila mara Serikali za nchi kubwa duniani zikiomba pesa kwa matumizi bayana ya kijeshi? Jeshi letu lina tofauti gani?

Maswali ni mengi. Na maswali yataongezeka sana endapo serikali haitajibu wawakilishi wetu Bungeni kuhusiana na Meremeta na pesa za BoT. Tutafikia mahali serikali itapoteza imani kidogo iliyobaki na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi. Serikali ina wajibu wa kutunza amani na utulivu ambao ni desturi ya waTanzania. Dhamana hiyo wanayo na ni lazima wa ienzi.
 
Binafsi nimeshindwa hata kucomment. Rais Kikwete, Spika Six, Mawaziri na viongozi wote tunashukuru sana kwa yote mnayotufanyia. Tuliwapa dhamana ya kutuongoza kwa ridhaa yetu lakini kinyume chake MNATUDHALILISHA NA KUTUFANYA WOTE NI VICHAA PUNGUANI TUSIOWEZA KUFIKIRI LOLOTE. HII NCHI MMEIFANYA YENU NA VIZAZI VYENU KWA MAANA KUWA MNAWEZA KUFANYA LOLOTE HATA LA AIBU NA MSIULIZWE. LAKINI KUMBUKENI YUPO MUNGU. DAMU NA MACHOZI YA WATANZANIA TULIOPEWA HII NCHI NA MUNGU HAVITAPOTEA BURE ASILANI. AHSANTENI.
 
CCM wamegeuza Bunge la Wadanganyika kijiwe cha mipasho. Sikuamini nilipomuona Waziri Sumari akimwambia Dk Slaa kuwa atafute hoja nyingine kwa staili ya waimba taarabu.

Kitu muhimu ni kuwa Watanzania wanazidi kuelewa uovu uliokithiri ndani ya Sirikali ya Wadanganyika.
 
Kwani Jeshi si Jeshi la wananchi sasa kwa nini swala hilo lisijadiliwe hivi kuna ambaye yuko juu ya sheria,hatutaki kujua mambo ya kitaalamu na kiitelijensia ya Kijeshi tunataka kujua matumizi yaliendeja na kwa vipi ,wasitufanye sisi wote ni ndodocha,kwa sababu kwa namna hiyo kunaibua maswali mengi
 
Kama kauli ya kwamba " hakuna aliye juu ya sheria" ni kweli, basi hawa watu wapelekwe mahakamani badala ya kuwaomba ruhusa kujadili ubadhirifu unaowahusu moja kwa moja
 
Back
Top Bottom