Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

Bhagosha wane,

Ivi kweli viongozi wetu wafanyapo mambo na waamuapo wao na kutoa hoja zao hufilia alama za nyakati au? au wanajua siku mambo yakija haribika wao watakuwa wameisha kufa ivyo izo hukumu au lawama zita waangukia vizazi vijavyo?? wajue haya mambo huwa yana mwisho na yatawafikisha watu kwenye kiti cha hukumu siku moja hata kama watakuwa na miaka 70 na kuendelea siku izo haita jarisha ati ni fulani ndio alito yale maamuzi ila nawe ulikuwepo kwa lile jopo tuwe makini sana ipo siku itakuwa Tanzania sio ya wadanganyika tena.

Pili
Ivi kweli hawa viongozi wetu wanadhani kuwa sisi hatujui? kuwa wao wanajua wakisemacho wananchi wanakijua fika, nikiburi kimewajaa kuwa wanajua fika twaelewa yote. wataka kuniambia hii nchi haina hivi vitengo?
DHS (Department Of Defense and Homeland Security)
DOJ (Department Of Justice)
DOD (Department Of Defense)
Nikuwa serikali inavuruga mambo hapo na isisingizie ati usalama wa taifa, mbona huko Ughaibuni Security Agency zikichemsha viongozi wanawajibika na kujiuzulu juu kwa utumiaji mbovu wa fedha za walipa kodi na uongozi mbovu iweje hata kwetu wanajifanya wao wanajua Usalama wa taifa wakati, Crime scene nchii zimejaaa kupita kiasi na police ndio hao huwasili kwenye maeneo ya matukio baada ya masaa 2 au 3 eg majuzi kule Mwanza Igoma wezi wameteka mtaa 30mins na police wakaja after 2 hours na Dar huko masaki jana police wamefika after 3hours jamani huo usalama tunao utetea ni upi?? nkwanza ndani ya nchi yako i mean homeland security tu ku i handle ni kazi iwe iyo ya DOD itakuwaje sasa?

inauma sana jamani watu kukubali wazi wazi pesa za walipakodi kutojadiliwa na kuwekwa bayana. na je CAG wakikuta uozo humo ndani nani aadhibiwe? au na report haitatolewa itawekwa kapuni basi wasinge itanga iyo issue nzima na wakaifanya basi kiusalama kimya kimya kama ni wakati wa uwazi hata swala la pesa budget yao nayo yakuficha??

tukutane 2010. kwa mnao tetea majimbo yenu.
 
Hivi kweli ufisadi wa meremeta, tangold ni masuala ya 'national security?'

Suala Usalama wa Taifa linatumika kama kichaka cha kuficha uovu na ubovu wa watatwala wetu. Huko JWTZ ufisadi wa kutisha umefanywa na Wakuu wa Jeshi kwa kushirikiana na Viongozi wa Nchi hii.

Wanadhani wataendelea kutudanganya siku zote na kutufanya mabwege! Watanzania tumelala kwa muda mrefu sasa tumeamka na hatuwezi kuendelea kufanywa kuwa mabwege.
 
Inavyoonekana ni kwamba usalama wa taifa ni serikali nyingine iliyo na madaraka ya kiimla kwani haiwezi kuulizwa wala kuuliza... yenyewe ni twanga pepeta... rusha roho ...

Kama ni mambo ya usalama... basi bunge linaweza kufanya public inqury in clossed door ili watu wa nje wasijue...
Nionavyo mimi hata wabunge pia ni part ya usalama wa Taifa pia, wanayo haki ya kuambia au kuambia mambo ya usalama...
Hatuwezi kujua kama Bil 155 zilikuwa za wizi kama uchunguzi/Ukaguzi hautafanyika kwa kisingizio cha usalama wa taifa... Hilo Taifa ni taifa gani linalowekewa kinga ya usalama ili hali likipeleka majamboz yake kwa nchi nyingine...nina maana kwamba jeshi walifungua kampuni offshore... sasa kama walifungua offshire kuna taarifa walitakiwa kuzipeleka huko...Mbona hawakusema kwamba hawakuweza kufungua offshore account kwa maana vitu kama memorandum of understand and constitution of the company, zinahusu usalama wa taifa?
 
Haki ya Mungu,kwa mawaziri kama hawa akina Sumari watz tuna kazi kweli kweli ya kufika!Mungu wabariki mawaziri wa JK na JK mwenyewe!lkn tunachojua ni kuwa Meremeta haipo jeshini na wala haijawahi kuwa kampuni-tanzu ya jeshi lolote nyumbani tz,na kibaya zaidi kampuni hii ilisajiliwa rasmi tarehe 1 januari,siku ambayo ni sikukuu duniani kote na waajiri wa serikali yeyote duniani huwa wapo majumbani mwao wakipumzika!
Mungu akuzidishie sana Rais JK na baraza lako la mawaziri-Amen!
AMEN tena nikiwa nimesimama. 🙁
 
"Hata Marehemu Balali alipoulizwa kuhusu namna mshiko wa EPA ulivyotolewa alijibu ilikuwa ni kwa ajili ya USALAMA WA TAIFA. Kwa kauli hiyo hata Mama Zakia alijiingiza kichwa kichwa na kusema hivyo japo baadae alichomoa. Swali la kujiuliza ni kwa nini Spika alikataa majibu hayo kutolewa Ijumaa kama ilivyotakiwa? Ama ilibidi wakaombe ushauri kutoka kwa Mkuu wa Kaya! Waendelee kutudanganya lakini naamini ni vigumu sana kusimamia uongo na kila lifanywalo kwenye giza, panapo mwanga jambo hilo litaonekana tu."
_____________________

taffu 69:

Spika 6 anaogopa kupoteza uspika na pia jimbo lake maana akina RA wameshasema lazima ang'oke na wametangaza jimbo lake na ya wengine wanne yako wazi.

Polepole ameanza "ku-toe the line" as ordered by King Maker RA.

Ni uchafu mkubwa usio mfano tunaoshuhudia Bungeni sasa hivi.
 
Jeshi hili ni la nani, mimi nauliza nini,
La nini tena kwanini, mwenye kujibu ni nani
Nauliza kwa makini, mtanipa jibu gani,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Meremeta ni ya nani, Mkuu tuelezeni,
Twataka mtangazeni, tujue wazi kwanini,
Mnachotuficha nini, mnamuogopa nani,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Mnatuzuga kwanini, kwa majibu yalo duni, (mbadala- "ya kihuni")
"Tusiseme hadharani", mwatung'akia Bungeni,
Hivi nyinyi kina nani, mnatuona wageni,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Ati wabunge "nyamazeni, serikali ni makini,
Mambo haya ya sirini, hatutawajulisheni,
Mengine yajadilini, Meremeta iacheni,"
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Si kura tuliwapeni, mtuwakilishe Bungeni,
Kimya chenu ni cha nini, mnaburuzwa na nani,
Mbona mwagwaya kwanini, vigugumizi vya nini,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Mwamunyange ndiye nani, Jeshi lake ndiyo gani,
Sumari yeye ni nani, Jeshi ni la nchi gani,
Walipa kodi ni nani, Jeshi linaitwa nini,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwa nini?

Walioiba kina nani, wakijificha jeshini,
Ni usalama wa nani, mbona hatuambiani,
Na usalama wa nini, nawauliza semeni,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Nasema nyinyi kubalini, Meremeta ni uhuni,
Uchafu umilikini, na bora jisafisheni,
Mtatuficha mpaka lini, hamtaweza jamani,
Siri hizi ni za nini, zanani, tena kwanini?

Kagoda nayo ninini, Dipu girini magirini,
Mwanchi goldi ya nani, Tanigolidi ya nini,
Haya yote mpaka lini, nauliza kijiweni,
Siri hizi ni za nini, zanani, tena kwa nini?

Mtakula mpaka lini, mtavimbiwa jamani,
Kula huku kula gani, ni njaa namna gani,
Bila kunawa watani, hadi ndotoni kwanini,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Watoto waje kula nini, na mnakomba chunguni,
vidole mwavilambani, njaa haiwaisheni,
Uraiani na jeshini, mwamega na kumegani,
Siri hizi ni za nini, za nani, tena kwanini?

Jembe ninaweka chini, wamenikera mtimani,
Dharau yao ya nini, mipasho nayo ya nini,
Watapeta mpaka lini, atawazuia nani,
Siri hizi ni zanini, za nani, tena kwa nini?


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Last edited:
Afadhali Dk Slaa kamwandikia Spika kumweleza kuwa anaanza kupungukwia na imani juu yake na juu ya ofisi yake kuhusiana na masuala nyeti yanayofanywa na serikali
 
Hivi hiki kiburi cha watawala kinatoka wapi? Au ndiyo wameshajihakikishia kuwa wabongo ni mabwege and for them is for granted? There need more than an action which will amke them learn a lesson; but which type of action!! It is now our life and death; our children and their future; this is our country!!
 
Siri hizo za wenyewe,
Kuzijua ni taabu,

Zina mbawa kama mwewe,
Huzioni kwa vitabu,

Usihoji uambiwe,
Afadhali uwe bubu.
 
Mara ya mwisho niliposoma jina la Jeshi letu lilikuwa linasomeka "JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA" - na kwa kimombo "Tanzania People's Defence Force"

Sasa najiuliza:

a. Ni lini jeshi letu liliacha kuwa la Wananchi wa Tanzania na kuwa Jeshi la Serikali ya Tanzania?

Mwenye contact za Mwamunyange au au msemaji wa Jeshi hilo naomba mnipatie. Tafadhali.
 
Siri hizo za wenyewe,
Kuzijua ni taabu,

Zina mbawa kama mwewe,
Huzioni kwa vitabu,

Usihoji uambiwe,
Afadhali uwe bubu.

Machozi yamenitoka kwa kusoma tunzi zenu. Kwa kweli naomba utume kopi hii kwenye magazeti mbalimbali.
Inguluvi ivatangage wayawe nyenye. Mgendelage uludodi ulukavu luladenyeka
 
nimekumbuka maandamano makubwa yaliyofanywa UKRAINE!matatizo yao hayapishani sana na matatizo yetu kiuongozi.

lakini kufanikiwa moja kwa moja ni lazima WANANCHI WAGUSWE,then mambo mengine yaendelee.

SWALI LANGU:elimu ya uraia,na haki za kikatiba imewafikia wananchi walau kwa asilimia sitini?

ukweli hapa ndipo mgogoro unapoanza.viongozi wanatake advantage of our ignorance in knowing our rights,constitutional right
 
Machozi yamenitoka kwa kusoma tunzi zenu. Kwa kweli naomba utume kopi hii kwenye magazeti mbalimbali.
Inguluvi ivatangage wayawe nyenye. Mgendelage uludodi ulukavu luladenyeka

ye mukwi yi nguluvi!
Inguluvi yitanga ndauli muyawe?
Unoge mwanakwetu?
 
Jamani Meremeta Mkapa anahusika moja kwa zote, hili ni kweli. unajua wakati mwingine nakubali hoja ya Mtikila kwamba Mkapa alitoka msumbiji akiwa na miaka mitano na mzazi wake( kama mnakumbuka issue ya kutaka kuchomolewa uraia kwa G.Ulimwengu iliendana sambamba na bomu alilotoa Mtikila). Sasa mimi najiuliza ni Mtanzania gani anayeweza kufanya mambo aliyoweza kufanya yule tunayemwita mstaafu? Alingoja mwalimu afukiwe atuonyeshe sura ya kwao msumbiji. Watanzania hatujakuzwa kwenye maadili hayo bwana wote tunajua.
Augustine, Unafikiri CCM watataka kuachia ngazi kwa urahisi ili muwakate vichwa?? thubutu kaka, hiyo haiwezi tokea nafiki labda kipindi cha wajukuu zetu..Muangalie mtu kama Museveni anachofanya, kwa sababu anajua maovu yake ndiyo maana hataki kutoka, yupo radhi wananchi wafe yeye asiguswe.Mzee ukitenda dhambi moja unatenda na nyingine unless uwe mjanja kugundua na kukubali kosa.
 
bado tuna safari ndefu..

ndefu sana mkuu!watu wanao pata AWARENESS mara nyingi ni wale wenye access na mitandao,na magazeti na redio!

asilimia kubwa ya watz hawana ustaarabu wa kusoma magazeti wala kusikiliza redio.

ipo asilimia kubwa tu ya watu hawana uwezo wa kununua magazeti

ipo asilimia kubwa zaidi hawafikiwi na magazeti!

kwakweli ili tuifupishe safari ingefaa wanaharakati wakarisk hata maisha yao kama kina mandela.

i suggest we shift to PLAN 'B'
 
Hivi hiki kiburi cha watawala kinatoka wapi? Au ndiyo wameshajihakikishia kuwa wabongo ni mabwege and for them is for granted? There need more than an action which will amke them learn a lesson; but which type of action!! It is now our life and death; our children and their future; this is our country!!
Umeongea maneno ambayo ni hali halisi. Watanzania hawataki kuamka katika usingizi huo mzito kama wa kupewa dawa, kwa kuwa ni dhahiri kuwa pindi uchaguzi ujao ukifika, watawachagua hao hao. Ni akili hiyo??
 
Fikiria mikataba ya madini; ilifikia tumekubali kuwa mikataba ni siri, ni lazima iwe siri na itakuwa hivyo for ever. Mikataba ya madini ni documents au ni Nyaraka ambazo zitawahusu viongozi wote watakaokuja baadaye. Inaihusu jamii nzima imekubaliana nini na hao wanaochimba madini. Hiyo mikataba imebaki siri, na itaendelea kuwa siri. Tumeambiwa katika mikataba hiyo kuna kipengele kinachozuia mabadiliko yoyote ya sheria ya kodi inayowahusu walioingia mikataba na sisi. Ni kwamba huwezi kubadilisha sheria yoyote ikagusa makubaliano hayo. Hata katiba.

Sasa haya ma kina meremeta, sijui nini yanaangukia kwenye uozo huo huo. Hakuna kujadiliana lolote. Tumeambiwa ni mambo ya usalama wa nchi. Maana yake haturuhusiwa kujadili usalama wa nchi hii. Usalama wa nchi hii ni Domain ya wateule waliowekwa kutulinda; hata tukigundua kuwa wanatupiga chenga ya mwili.

Hili ni tatizo la kimaadili, ni tatizo la kiutendaji ni tatizo la kiakili vile vile. Uongozi umefirisika na hauna hoja, unajificha na kuzama ndani ya vitisho.

Tufanye nini? Hizo siri wameshaapa hawaezi kuzitoa kamwe. Tuendelee kulalamika hata miti itatusikia na kutoa ushahidi. Tuanzishe mgogoro wa kiraia kupambana na nguvu ya dola kama inavyofanyika kule Iran?

Lazima kitu fulani kifanyike ili hao wateule waone kuwa sasa umma hautaki, vinginevyo shughuli kama kawaida (business as usual)
 
It is rather ridiculous!! mtu anaulizwa ametumiaje hela ya Wananchi, jibu analotupa ati ni siri,lakini kinachoulizwa ni legitimacy ya kutumia hela na inaonekana kuna ujanja/wizi umefanyika sasa kama bunge haliwezi kuambiwa matumizi yetu yakoje ni nani mwingine anayewakilisha interest za watanzania?

Mimi naomba Spika atoe kibali bunge liende kwenye closed session kwamba sisi wengine tusijue wabunge wamekula kiapo hivi waelezwe kwa undani na umakini alafu wao watapima kama ni usalama wa nchi ulikuwa at stake or wa CCM or wa Ikulu peke yake kwa maana watu walikwiba ili ipatikane hela ya Campaign au ni wizi tu kama wa EPA lakini kusema ati tusizungumze wala kuuliza kwa sababu Pinda alisema hawezi kusema!!

Ni kutetea wizi nami siamini kama bunge zima liko pale kulinda wizi wa watu wachache.

Mungu Ibariki Tz watu wafunguke macho na haki itendeke.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom