Meremeta & TANGOLD Revealed!


I think this company has nothing to do with Mining gold. I think it has to do with training and modernizing our armed forces. That is training specia forces and so forth. Remember Kiwete once said, he wants to modernise our army? Now that is why it can not be disclosed by the government, I THINK!!!
 
Nsunza I Beg To Differ With You When You Say Army Training.....thats Not True At All.
 

SASA KAMA KULIKUWA NA WANAJESHI MAFISADI WENYE HISA AMBAO WALIITUMIA NAFASI HIYO KUTUIBIA WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA ccm MTANDAO..THEN NI KWANINI MWEMA ASIKAMATE?
KWANI KUNA WATU WANAHODHI NCHI KAMA MALI BINAFSI NA SISI TUKAE TU?
 
Nsunza I Beg To Differ With You When You Say Army Training.....thats Not True At All.

Huyu mtu hapo ameonyesha kuwa hakuna connection yoyote ile ya kuweza kusema MEREMETA NI MALI YA JESHI NA SI WATU FLANI FLANI WALIOJIKABIDHI TAIFA LETU KWAO NA KWA FAMILIA ZAO!
NI MPAMBANO WA UHURU!
NA NDIO MAANA NIKASEMA KABLA HATUJAPIGANIA UHURU WA ZIMBABWE..TUUPIGANIE WETU KWANZA!
 
Mbinu za baadhi ya mafia wa mataifa ya kimagharibi pamoja na wale wa AFRIKA za kuanzisha vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa ku channel pesa za rushwa na kuwakumba hata wale ambao ni safi ili wasiweze kuukemea Ufisadi inavyotakiwa...Pia wasiweze kuyapinga mataifa hayo wazi wazi wakati wa propaganda zao za WEST!

HATUA HIZO YA KIMAFIA...IMEPELEKEA MAPIGANO MAKUBWA YA WENYEWE KWA WENYEWE NA NDIYO MAANA AFRIKA HAIKALIKI!
AFRIKA TUKATAE!

TUNAANZIA TZ HADI AFRIKA NZIMA!

TUWAKATAZE ZIMBABWE KUPIGANA WENYEWE KWA WENYEWE KWANI THE NEW SCRAMBLE FOR AFRIKA IS ON THE WORK!

PIA MSIACHE KULIOMBEA TAIFA,BARA NA DUNIA KWA UJUMLA!
 
Mimi niliwaambia watu huyu mtu bonge la joker the very first day aliposimama katika bunge kukubali uwaziri mkuu.

Watu ooh aaah, tunaona sasa.

Pundit, i beg your pardon. Sio joker...... kuna kitu zaidi ya hapo. Kadanganywa vibaya sana. Bunge, lisiambiwe ni usalama wa Taifa. Kamati ya Rais ya Madini inaambiwa.... usalama gani wa Taifa kwa watu ambao hata hawajala kiapo cha kuficha siri? Usalama gani wa Taifa mbele ya wafanyabiashara wasio wabunge na wengine hawajawahi kuwa katika utumishi wa Umma. Kuna distortions from the government side and from the opposition side. Now the whole truth has to be said. HAKUNA USALAMA WA TAIFA. Nipo Kigoma, narudi huko. Mungu aniweke tu.... Nasema hapa ilki iwe wazi na sina cha kuficha ili niibuke tu Bungeni.

Its not about Pinda, its the nation. Our country!
 

Zitto,

Mwaka huu hata wakitumia visingizio vya usalama wa taifa kama ambavyo wamekuwa wanafanya miaka yote bado moto utawawakia.... jipange vizuri ili wazidi kubanwa....

Tunakuombea mwanawane.....
 

Usiwe narrow minded Mushi
Zimbabwe ni ajenda na tutaendelea kuizungumza na Ufisadi ni ajenda ya ndani. Umeona wapi nchi haina interest na mataifa mengine wewe? Ukiambiwa meremeta ina links na zimbabwe utasemaje? Be broad wewe, uwe na bigger picture ya mambo na usiwe parochial
 
Meremeta haina uhusiano wowote na "siri" za kijeshi! Huo ni ufisadi mwingine!
Masuala ya "Training" huu ni uzushi mazoezi yote ya kijeshi wananchi wamekuwa wakitangaziwa, hususani wale walio karibu na eneo la mazoezi, sasa hayo mazoezi yalifanyikia wapi "MARS" ama "JUPITER" na lini!!??

Kama tuliweza kuambiwa manunuzi ya "rada" na "helkopta" mbili za kijeshi, nini tena kilichobaki ili kuwa siri ya kijeshi??
 
Wakuu naomba kuuliza kaswali: Hivi miradi ya Jeshi huwa haiingizwi kwenye orodha ya mali za Serikali? na hesabu zake huwa hazikaguliwi na makaguzi mkuu wa Serikali? na nafasi ya hao wakurugenzi yaani the late Balali, Chenge nk ni ipi?
 
Sio joker.... Kadanganywa vibaya sana....

...Kuna distortions from the government side and from the opposition side

Its not about Pinda, its the nation. Our country!


Sasa hapa Mkuu wangu Zitto naomba awe makini, makini, makini mno kusema Pinda anadanganywa.

"Distortions from the goverment"? Kama Serikali sio Pinda, basi hakuna kitu kinachoitwa Serikali!

Waziri Mkuu ana uwezo wa kupata ukweli wa nyeti yoyote ile. Chochote. Tena Pinda katoka Ikulu na Usalama, anajua nani ana 'dataz' na atampata vipi.

Kusema "Its not about Pinda, its the nation. Our country!" inaweza kutafsiriwa vibaya sana Mkuu Zitto.

Kana kwamba unataka ku deflect the heat from Pinda. Iende kwa Serikali. Serikali ni nani?
 

...ambavyo vyote hivi sasa tunajua kuwa vilikuwa bomu au vilinunuliwa kwa njia za kiufisadi.... kwenye haya wanayotaka kuficha itakuwaje sasa?! ....kauli zao kwa kweli hivi sasa zinatia kinyaa!!
 

Kama Madai Yako Ya Kunidhalilisha Kuwa Nina Akili Finyu!
Then Soma Hii Habari Hapo Chini Na Uniambie Umeilewa Vipi Na Ukishindwa Sisemi Kitu Hadi Ukamwite Rafikiyo Fisadi Kikwte!

 


Wakuu mtanisamehe pale nitakapokuwa nimekosea unajua umri tena kumbukumbu zinapotea.

Wakati wa uongozi wa jenerali Mbona kuliwahitokea kutunishiana misuli kati ya Mkapa na Mboma katika kipindi ambacho Mboma alikaribia kustaafu. Nyepesi nyepesi zilisema ilikuwa ni mambo ya pesa(labda ndo hiyo Meremeta) ili kumpooza Mboma, vibali vya kuingiza sukari toka nje bila ushuru vilitolewa. Baada ya magazeti kuandika kuhusu utolewaji huo wa vibali na waziri wa fedha(Yona)bila kufuata taratibu wakaona watumie kofia ya jeshi, lakini ukweli ni kuwa matani ya sukari iliyoingizwa yalimnufaisha Mboma, kuanzia ushuru.

Nimekaa nikafikiri kwanini Mkapa amekuwa jeuri kwa kashfa zote hizi, kwanini JK amekaa kimya kuwachukulia hatua hawa majambazi,wakati nchi yake inateketea,kwanini viongozi wetu wanatuibia na kuja kutudanganya waziawazi kama akina Pinda, kwa nini wabunge wetu baadhi wako kimya na wengine wanatetea maafisadi? Hii gut na courage wanaitoa wapi? Nikagundua wanaitoa kwetu sisi wananchi. Yaani kwa kuibiwa kote huku na bado tunadanganywa na viongozi tunaotegemea wachukue hatua, tumeshindwa hata kuandamana tu!!! Viongozi wetu wanajua kama wao nimazumbukuku basi sisi wanachi nimazumbukuku no. 1. Pinda asingekuja na utumbo huu kama angejua kuwa wananchi tutachukua hatua.
Maandamano ya amani ya kushinikiza uwajibikaji, majibu sahihi ya kashfa zote na uchukuliwaji wa hatua kwa wahusika wote ndo dawa.
 
Huu ni mwaka wa shetani na mafisadi lazima wataokoka tuu kwani wamelinywa na sasa lazima walikoroge...
 

Haya ndiyo mambo ya "The president was misled"

Rais akiwa misled, akichukua ushauri bila ku verify, hilo suala linakuwa responsibility yake na si ya aliyempa ushauri kwa sababu rais ana nguvu zote za dola na responsibility yote huishia kwake.

Mara nyingi watu wanaosema "The president was misled" au "the PM was misled" wanakuwa either ni wapambe au watu fulani ambao wako diplomatic to a fault na hawawezi kusema "The president erred" of "The PM erred"
 
Eti ZIMBABWE ZIMBAWE!
ZIMBABWE NA NCHI IMEUZWA?
NI VITA YA UHURU!
NANI KAKUPELEKA BUNGENI KUPIGA KELELE ZA ZIMBABWE ULIZOAMBIWA NA KIKWETE?
HIVI NIWAULIZE HAO WANANCHI WAKO WA HUKO KIGOMA AMBAKO KUMEPIGIKA KAMA WALIKUTUMA KUFANYA NINI?
NA KAMA UNGEWAAMBIA KUWA UNAKWENDA BUNGENI KUFANYA KAZI ZA KIKWETE NA ZIMBABWE,UK,KICHAKA NA WENZANKE...KWA AKILI ZAKO NYINGI WANGEKUPA KURA?
KUMBE WENGINE WATOTO KWENYE POLITICS NYIE!
I DIDN'T CHOOSE POLITICS...POLITICS CHOSE ME!
NA SITATEREKA HATA KAMA UNA WAPAMBE!
LETENI MAMBO NIKO HAPA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…