Menyu za makabila

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
db_zambian-food-nshima-nsima-ugali-sadza07inswa1.jpg

MAISHA NA MAFANIKIO

Hiii ni baadhi tu kwa wale wa makabila, wanaweza kutuletea zaidi zinazofanana hapa. Hii kitu inaitwa Kumbikumbi, KAMA ILIVYO senene kule kanda ya ziwa, inapatikana katika msimu fulani tu wa majira ya mwaka.
 
Hapana, kumbi kumbi hawana mafuta sana. Ukiwakaanga wanakauka wana taste ya karanga zilizokaangwa.
 
Sasa hii kutoleana udenda namna hii maana yake nini Mkuu?

Huna huruma na mate yetu? Sasa hivi yanashuka tu kwa hasira.....
 
nilishawahi kula nilivyokuwa mdogo,sasa hivi hata unipe tena siwataki tena.naona kama nakula wadudu,ingawa enzi hizo,nilikuwa nawaona watamu tu
 
Sisi kwetu huwa tunawakausha na kuwatunza na hutumika hata wakati wa kiangazi. Ila haya mambo ya kutamanishana jamani hayafai
 
Kwani hiyo sahani yenye mahindi imeambatana na nii? Maana naona chamaki nchanga ndo nini?
 
hiyo menyu ya wakusini ni kiboko sana yaani si mchezo mahindi ya kuchemsha na samaki mchanga kweli mlo thabiti
mwenzenu nilipokuwa mdogo nillikuwa nawakamata kumbikumbi na kuwatumbukiza mdomoni yaani walikuwa watamu sana si mchezo
mpaka mate yalikuwa yanadondoka katikati ................. si mchezo mwana lete menyu ya wachaga basi
 
nilikuwepo muda mrefu sana sasa kabla haijawa jamiiforum kipindi hicho ilikuwa bongo chat lakini hawa wananiweka wakukongaga
 
Back
Top Bottom