The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,320
- 117,611
kyeeri iki nkulalya kabisa foo..........
nkwiifo kukee nsurume ro shoo wa womi............
kwa mpata mwaanya shiruuya lurere kinyoo shoo.
tafsiri please
kyeeri iki nkulalya kabisa foo..........
nkwiifo kukee nsurume ro shoo wa womi............
kwa mpata mwaanya shiruuya lurere kinyoo shoo.
Mentor utaoa lini2008, January 28 Jumatatu
Ndo nilikuwa natimiza miaka 26. Kijana mtanashati miaka miwili kazini katika kampuni moja ya vinywaji.
Siku hii bosi wangu alinipa ofa ya a whole crate ya vinywaji..my fellow workers wakaorganize surprise bash for me. Kwa kweli sikuwa nimeitegema kwani birthday yako ikiangukia Jumatatu (kama ya mwaka huu) huwa huna plan yoyote kubwa since unajua the following day ni kazini!
Nilipotoka kazini mshkaji akanipigia simu;
Mike: Oya Mentor upo wapi?
Me: Dah ndo natoka job mtu wangu naenda home tu
Mike: Aaah pitia hapa NISIKUONE NA MWANANGU pub bana kuna mshkaji anasema anajua biometric readers vizuri labda anaweza kukusaidia project yako
Me: Mh Mike, hatuwezi kutana weekend?
Mike: mshkaji mwenyewe si wa kukaa sana ka vipi pitia tu si ndo njia hiyohiyo ya kwenda home mwana?
Basi bana mbele ya teknolojia? Ikabidi na uchovu wangu nijikongoje hadi pale.
NISIKUONE NA MWANANGU Pub, 1830hrs
Ile naingia tu..nasikia SUUURPRIIISEEE!!! Ndo nikashtuka aaah kumbe its my birthday I was really surprised kwa kweli but delighted as well...We really drank that night.
Something extraordinary happened I met a girl.
A very beautiful lady. 23 yrs was her age. A finalist at Muhimbili.
Namimi kwa courage ya birthday boy nikamfuata nikaomba kudance naye. Ofcourse alikubali haha
Basi kidogo kidogo tukaanza kupiga stori za hapa na pale na hata muziki ulipoisha tukaenda pembeni kuendeleza stori.
Aliniambia kuwa alikuja pale na dada yake ambaye ni co-worker wangu. Basi nikachukua contacts zake tukawa tunaendelea kuwasiliana.
To cut the long story short
Kidogo kidogo tulizoeana na ilichukua two months tu kuhakikisha amekuwa wangu. Alionesha kunipenda kwa dhati na hata alipomaliza chuo nilimwambia nataka kuanza michakato ya kumfanya awe mke wangu. Alinijibu sentensi ambayo kwa kipindi kile sikulitilia maanani, Hilo tulishalijua!
Basi michakato ya kwenda kwao ilianza nikamtumia mshkaji wangu Mike koz alikuwa amenizidi anisaidie kufanya hiyo michakato ifane. Kama kupeleka barua na formalities nyingine.
Nilimvalisha pete (ambayo alisisitiza aichague yeye kwenye duka specific) na tukawa tunasubiri siku ya harusi tu tuhalalishe mambo.
2010 January 23 Jumamosi
Alikuja kwangu Ijumaa. Tukaenda kuangalia live band ya kina Hamis Mwinjuma then ikabidi aje kulala kwangu aondoke asubuhi awahi kazini kwani ni nesi na alikuwa zamu siku hiyo.
Basi kwa haraka ya kuwahi job akasahahu simu yake kwangu.
Mida kama ya saa tatu hivi ndo nashtuka kusikia inaita alikuwa akipiga shoga ake mmoja ivi. Iliita kama mara tatu ikanibidi niipokee tu.
Nikapokea;
Shosti: We mwanga wa kike nikipiga mimi unajifanya upo na jianaume lako ambalo kama sio mimi usingelipata. Muone kwanza na leo nina maagizo toka kwa mganga wako nimeamua nikuambie kwa mdomo si unajifanya kusoma message hujui!
Ilinibidi nikate simu kwa mshtuko curiosity got the best of me ikanibidi niingie ndani ya simu ambayo kwa muda wote wa mahusiano yetu sikuwahi kuigusa. Nakumbuka kuna kipindi niliishiwa credits ghafla ikabidi nimuombe nimpigie mshkaji akanitaka nitaje namba aandike mwenyewe na nilipomaliza akataka kukata mwenyewe.
Nikazama kwenye messages
Nilishtuka sana siku ile. Sikujua kama haya mambo bado yapo ya kwenda kwa waganga? Binti mrembo vile? Na kanisani mbona alikuwa anaenda? Na usomi wake je?..nilijiuliza mambo mengi sana nikakosa jibu..
: kulikuwa na masharti ya kuhakikisha ananipata na ninakuwa mumewe kwa hali yoyote ile
: kulikuwa na masharti ya kuhakikisha anapata pesa kama kuvaa chupi kwa mwezi
:kulikuwa na masharti ya kuendesha gari bila kuvaa chupi
:masharti ya kulala juu ya kaburi (hizi ni siku aliniambia anaenda safari za kikazi)
I have been single since then
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
it wasn't meant for you dude!
BTW karibu zanzi
you get an award lolz!
Mentor kumbe walikuwa wanakuboost,
Duh umenifanya niwe scared duh hawa wanawake wengi wao wanaboost
rafiki umekuwa siku hizi....................ila umenipotezeaje best??hahahahahahahahahah hapo pekundu nimejikuta nacheka sana, kuna catalyst inatumiwa eeehh kuspeed up the chemical reaction, All in all ni kudanganyana tu, we mtu anakwambia anatoa dawa ya mapenzi au ndoa wakati watoto wake mwenyewe wapo wamezalishwa nyumbani na hakuna ndoa.....mimi ninaamini huyu dada alipendwa kweli sema tu hakujiamini kwani ingekuwa uganga unampa mtu mume kweli basi asingekamatika, mara nyingi hizi ni short cut za shetani ambazo watu hawatafakari kabla ya kuzitekeleza
Hilo ni suala ambalo lipo kinywani mwangu katika kila muda ambao nakuwa mbele za Mungu{Maombi}... Ki ukweli wengi wameshau kumwambia Mungu kuhusu aina ya wenza wanaowataka... Vijana wengi huwa wanaomba Mungu awape mafanikio ya kimaisha pekee..... Bado sijakata tamaa. Najua Mungu ameniandalia mke mwema. Ni suala la kusubiri wakati wake tu na sitaacha kumkumbusha.... Kuna hali inaitwa PUSH{Pray Until Something Happen}.. Na apply hiyo PUSH.....
nope!Upo zanzibar?
vacation?
Jaman wewe bestito, nilikuwa sijakua huko nyuma? mie nipo tu full kukimbizana na maisha na kupingana na shetani kwa nguvu zote....pray 4 me.....rafiki umekuwa siku hizi....................ila umenipotezeaje best??
love you
hahahahahahahahahah hapo pekundu nimejikuta nacheka sana, kuna catalyst inatumiwa eeehh kuspeed up the chemical reaction, All in all ni kudanganyana tu, we mtu anakwambia anatoa dawa ya mapenzi au ndoa wakati watoto wake mwenyewe wapo wamezalishwa nyumbani na hakuna ndoa.....mimi ninaamini huyu dada alipendwa kweli sema tu hakujiamini kwani ingekuwa uganga unampa mtu mume kweli basi asingekamatika, mara nyingi hizi ni short cut za shetani ambazo watu hawatafakari kabla ya kuzitekeleza
Hahaha, may be it works ndiyo maana wanapelekana ku boost watu. ila nayeye huyo dada wa ajabu mentor alimpenda kabla hajamboost sasa sijui aliona mentor atabadili mawazo akaamua awahishe reaction
Njia pekee ya nyie wanaume kuepukana na haya ni kumng'ang'ania Mungu na kulishika neno lake, la sivyo shetani ameamua kuwatumia wanawake waliokubali kutumiwa nae ili kuwapotezea nyie muelekeo na kufanya maamuzi sahihi ya kumpata mwenza wa kweli kutoka kwa Mungu. Sasa kazi kwenu kujipanga kwa maombi.
Twende tufanyiwe maombi, lakini mimi si boostic aisee.