Mengi (WATANZANIA) Vs Prof. Muhongo (WAWEKEZAJI)

Kumbe unaongelea ujanja.
ulitaka tuendelee kuwa mazoba tusihoji uhalali wakuingia mikataba mingine ya hovyo kuliko ile ya mangungo? Dhahabu kwishnei! Diamond kwishnei, Uranium Kwishnei na gesi nayo mnafanya kificho! dah! kweli ninyi hamnazo...
 
Mkuu hayo makampuni Tanzu yanamadeni kiasi gani? unazungumzia TPDC na STAMICO?... TANESCO tayari tunajua mmeshaitwisha deni la 400 Billioni ili hatimae muiuze kwa Symbion...
 
Kwa hio unataka Mengi apewe zawadi ya vitalu?
 
Ni upuuzi uliotukuka kusema Mengi anawatetea watanzania. Charity Begins at home...mbona ameshindwa kuinua vipato vya wafanyakazi wake IPP badala yake anawanyonya tu! Mengi ana maslahi binafsi ila anatumia 'Utanzania au Uzawa' ili apate support ya watanzania wanaolipuka kushabikia mambo bila kuyachuja.Mengi ni 'manipulator', anajua kutengeneza maneno mazuri mbele ya jamii but behind those words huwa ana maslahi yake.
 
Unang'ang'ania uzalendo tu,hautaki ukweli, hebu we niambie ni mzalendo gani anayeweza kuwekeza kwenye mradi wa gesi na akafanya biashara hiyo na mataifa makubwa nje ya nchi?
Samahani mkuu, unauelewa wa level gani? kupitia wanahisa Watanzania wataweza kuwekeza na kumiliki biashara kubwa kama hiyo ya Gesi...CCM na serikali yake wanataka STAMICO na TPDC ndiyo wawekeze kwa niaba ya wananchi wakati wakurugenzi wake ni wateule wa Rais...hii haikubaliki kwasababu tunajua TANESCO inavyohujumiwa na hawa wanasiasa...
 

Mzee 10000 naona umeua kimtindo.....
natamani kumpigia Prof Muhongo aendelee na msimamo wake/wa serikali,natamani Prof muhongo asome hii kitu,serikali kupitia TPDC Imiliki 49% hapo itakuwa safiii,lakini ukiwapa hawa wazawa wenzetu hakianani hata uwe na uingineer wako,master na mengine ukiajiriwa tu,mshahara wako hutazidi laki 9,serikali ichukua kodi kwa haya makampuni ya Gesi,pia iwe na hisa asilimia 49% hivi ili iwawakilishe wananchi ipasavyo,pia watu najua wataajiriwa na kupata ujira wa ukweli more than a MILIONS PER MONTH.
Mzawa akikuajiri hela atakayokulipa mshahara duuu,Mhhhh,serikali eee hebu simamia hii kitu kodi na hisa Tu,wazawa waende kwenye hoteli bwanaa.
 
Nakubaliana na utaratibu wa serikali kuitumia TPDC kamamwakilishi wa wananchi wote katika secta hii ya Gesi na Mafuta.Kwanininakubaliana nao?kwanza ukiangalia mfumo mzima wa secta hii kwa sasa NationalOil Companies Duniani kote ndio zinazo takeover kwa sasa. Mfano ukienda Oman wana Oman State,Qatar wana Qatarpetroleum na pia angalia hata "Seven Sisters"(Oil Companies)zote nimashirika ya mafuta na Gesi zinazomilikiwa na Serikali mbalimbali.Hatakitakwimu makampuni kama ,Total, Shell na ExxonMobil n.kwanamiliki 23% tu ya Mafuta na Gesi duniani.Kwa National Oil Companies ni over61%.sasa ikiwa wenzetu waliogundua Gesi na Mafuta zamani,na wenye ujuzi namambo haya wanabadilika na kuzifanya serikali ndio wawakilishi wao sisitunashindwa kitu Gani?
Pili suala la kujiuliza ikiwa TPDC ndio wanaotuwakilishakupitia serikali je! ni kweli Serikali itapata "fair share"ukilinganisha na makampuni ya nje ambayo yamegundua Gesi au Mafuta hayo?Je!kuna information za wazi ambazo zitaonesha/zinaonesha Serikali inapata mapatokiasi gani kutokana na hiyo Gesi?Je! mapato ya serikali yanatumikaje na ni yapimaendeleo yake?Jamii itanufaika vipi kutokana na resource iliyogundulika?Niwatanzania wangapi wnategemewa kunufaika katika kupata kazi na shughuli zakibiashara?Ni kwa kiasi gani ugunduzi wa Gesi na Mafuta utapunguza gharama zaumeme?.
 
Kwa mawazo yako unadhani gesi au dhahabu haina tija kwako?

Inayo tija lakini bora apewe BP aajiri mameneja watanzania awalipe milioni 15 kwa mwezi kuliko apewe Mengi aniajiri mimi anilipe laki 8 , au apewe Rostam Aziz/Bakhresa walete wataalam wa kihindi kutoka Punjab. Si ndio wazawa wenyewe hawa?
 
Mengi aoneshe mfano kwanza kwa IPPMEDIA yake kila siku watu wanalia njaa.

Kama magazeti yanamshinda atakiweza kitalu cha gesi au mafuta?
 
Mengi aoneshe mfano kwanza kwa IPPMEDIA yake kila siku watu wanalia njaa.

Kama magazeti yanamshinda atakiweza kitalu cha gesi au mafuta?

Tukimtoa Mengi leo ukachukua nafasi yake ungefanyaje?
 
Sio kweli, wote tuna sauti labda wewe na wenzio wachache.

Kama we pia una sauti mbona hukuwepo alipokuwepo Mengi kuongea na wewe ukasikika?
Nadhani ulichoshindwa kuelewa ni kwamba Mengi alipata hiyo fursa na akaamua kuitumia kama ambavyo wewe ungeitumia.
Sina hakika sana kama ungeitendea haki kwa kiwango kile alichotendea yeye haki.
 
Kutokana na upeo wako mdogo wakufikiri ndio unaona hvyo ila kwa wale tunao mfahamu Mengi tunajua anatetea maslahi ya watanzania juu ya umilikaji wa rasilimali za taifa.

TPDC pekee ndiyo inaweza kulinda maslahi ya watanzania,Kelele zoote hizo za Mengi ni ubinafsi wake tu unaomtawala.Aliponyimwa Kilkimanjaro hotel akapewa kiwanja ajenge hotel lakini akakiuza kwa Fidha Hussein!Huyo Mengi nae ni dalali tu.
 
Inayo tija lakini bora apewe BP aajiri mameneja watanzania awalipe milioni 15 kwa mwezi kuliko apewe Mengi aniajiri mimi anilipe laki 8 , au apewe Rostam Aziz/Bakhresa walete wataalam wa kihindi kutoka Punjab. Si ndio wazawa wenyewe hawa?

Sijui ni ufahamu mdogo unakusumbua ama unatumika visivyo? wages kwa makampuni ambayo ni labor intensive huwa inafika hadi 50% ya mapato ya kampuni! GGM walizalisha zaidi ya $ 20 Billion kwa msimu wa 2011/2012 pekee, wazungu walilipana bonus kibao! Mbona wabongo hawakulipwa chochote? MIshahara ya wafanyakazi wa IPP na Bakhresa unategemeana na faida na mapato ya makampuni husika!... Mbona Makampuni ya Simu hayalipi mamilioni wakati wanatengeneza faida kubwa? Niambie Kampuni gani ya wawekezaji hapa Bongo yenye kujali wafanyakazi wake kiasi cha kuwalipa hicho kiasi unachotuambia! BP ya Waingereza ndo hovyo zaidi... Waambieni watawala ukweli kuwa Sheria zetu na sera za CCM ndio kikwazo kikubwa, Kapuya aliwahi kuwaambia wawekezaji wasilipe mishahara inayotofautiana sana na ya serikali kwa kuhofia kuwa serikali itakosa watumishi! ... Makaburu walisherehekea usiku kucha baada ya Chama cha Wafanyakazi kudai fedha mbuzi wakati wanaingia TBL... kwa taarifa yako wawekezaji wengi hasa kutoka ktk nchi za magharibi huwa wanatumia Ethnocentric model ambapo mishahara na marupurupu yote inakuwa inaendana na rate ya nchi husika ie going rate approach! Ni jukumu letu kama nchi kuweka wazi kuwa mishahara itategemea parent company ilikotoka...
 
TPDC pekee ndiyo inaweza kulinda maslahi ya watanzania,Kelele zoote hizo za Mengi ni ubinafsi wake tu unaomtawala.Aliponyimwa Kilkimanjaro hotel akapewa kiwanja ajenge hotel lakini akakiuza kwa Fidha Hussein!Huyo Mengi nae ni dalali tu.
Hiyo TPDC inachukua reference kutoka wapi? Shirika gani la uma limewahi kusimama badala ya watanzania na ikafanikiwa? kumbuka kuwa hawa Jamaa game wanalijua vizuri sana, wanatambua kuwa mali ya wote si ya yeyote...ndiyo maana wanahujumu kila shirika. TANESCO iko hoi, Reli, Bandari, ATC...???... Acheni kudanganya Watanzania ...Imetosha jamani, Zaidi ya miaka 50 sasa mnaendelea kuwapiga sound...
 

Mifano yako nivema ikaendana na uhalisia! Kila nchi ina shirika lake la ndege, ina reli, zingine zina bandari. Hali ikoje kwetu? hali ikoje Kwao?... Kwanini hamfanyi tathmini kulingana na uhalisia wa nchi?... chini ya serikali ya CCM wananchi bado mnamatumaini kuwa CCM inaweza kuwa upande wa wananchi? Mmelogwa au?...
 

Kwa maana hiyo unaona ni bora tupigwe sound na kina Mengi?ambao tuliwabinafsia viwanda vyetu na leo hii ni magodown?
 
Acha kugeneralise mambo wewe! Mengi mliwauzia viwanda vipi? TBL? TCCC? ATCL?TRL? Tanganyika packers? Magunia? Ngozi? General Tyre? Kiltex?Mwatex?Sunguratex?ZZK Mbeya? TANCAT? NAFCO?... Acha porojo wewe kuwadi wa rasilimali za Watanzania...kawaambie wakupe data za kutosha si unakuja hapa na porojo zako za buku 7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…