Mengi (WATANZANIA) Vs Prof. Muhongo (WAWEKEZAJI)

Mengi (WATANZANIA) Vs Prof. Muhongo (WAWEKEZAJI)

Mengi ni mzee mzalendo sana. Muhongo ni msomi ambaye ana kiburi cha ufahamu. He has intellectual arrogance.

Pambano la Ngumi a.k.a Ndondi ndilo litaamua nani mshindi kwani kwenye Malumbano kuitana waongo Mara hv itachukua kipindi kirefu kupata mshindi
 
Hivi Muhongo miaka aliyoishi Tanzania na aliyoishi nje ya Tanzania ipi ni mingi? Kama mimi kabla hajachagulia kuwa mbunge wa viti maalum nilikuwa hata simjui. Lakini Mengi tangu nipo shule ya msingi namfahamu. Hivyo akili yangu inanituma kuwa Muhongo amekaa mda mwingi nje ya nchi na pia amewahi kuukana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa kigeni. Alivyoitwa kuwa mbunge wa viti maalum ili apewe uwaziri ndipo akapewa uraia wa Tanzania.Kwa mtu kama huyu je atakuwa na uchungu kwa WaTZ? ndio maana siku zote amekuwa akiendekeza dharau kwa waTZ na sisi tunamwangalia tu.
Huu ni mkakati ule ule wa EHM, Ballali nae hakuwa raia wa nchi hii, yeye ni Raia wa Marekani ...
 
Naona pesa ya Mengi imeanza kufanya kazi ya kumchafua mhongo.
 
[h=1]kiukweli huwa nawamiss sana gazeti chambuzi la mwanahalisi...soma makala hii ya 2011...[/h]


SERIKALI inasema sekta ya madini inakua kwa kasi. Ripoti mbalimbali kipindi cha miaka mitano iliyopita, zinaonyesha sekta imeingiza mapato ya dola 4.7 bilioni.
Kabla ya 2000, haikuwa na mchango wa maana kwa pato la taifa kwani hakukuwa na uwekezaji mkubwa.
Shughuli za utafiti, utafutaji na uchimbaji wa madini zilianza kushamiri mwaka 1998 ilipotungwa sheria na wawekezaji kuhamasishwa kuja.
Hatua hiyo iliongeza shughuli za utafiti na utafutaji madini na leo – miaka 13 baadaye, ndiyo tuna makampuni yaliyomilikishwa migodi kama ya Bulyanhulu, Buzwagi, North Mara, Tulawaka, Geita, Nzega na Buhemba.
Kwa hivyo, uwekezaji mkubwa unaofuatana na teknolojia ya kisasa, unaendelea kwa madini zaidi kugunduliwa – mengi yakiwa ni dhahabu.
Sasa Tanzania inatajwa kama nchi ya nne barani Afrika kwa kuzalisha madini; na ya tatu – nyuma ya Afrika Kusini na Ghana – kwa uzalishaji wa dhahabu.
Kiwango cha uzalishaji dhahabu nchini kimekua katika kipindi hicho kutoka tani moja ya dhahabu kwa mwaka hadi tani 50 mwaka 2010.
Sekta ya madini ni moja ya sekta zinazopewa kipaumbele katika mipango ya serikali kwani mchango wake kiuchumi unafuatia sekta ya utalii.
Maana yake, sekta ya madini inakua kwa kasi zaidi ya sekta nyingine, ikitanguliwa na utalii ambayo kwa wastani huchangia asilimia 25 katika Pato la Taifa.
Hata hivyo, mchango wake wa asilimia 3.8 ungali mdogo mno kulinganisha na faida inayopatikana. Mapato zaidi yangeingia serikalini iwapo utunzaji wa takwimu na utoaji wa misamaha ya kodi kwa wawekezaji ingetazamwa upya.
Uwezo mdogo wa serikali kuitawala na kuiongoza sekta hii, kiwango kidogo cha hatua za uongezeaji thamani kwa madini ghafi na uharibifu wa mazingira, huchangia sana kuinyima serikali mapato.
Isitoshe, sekta hii haijatoa mchango stahili katika kukuza sekta nyinginezo kama ajira, viwanda na miundombinu. Pia haijasaidia kuongezea wenyeji uwezo wa kuhudumia machimbo yao.
Malipo ya mishahara yanayopimwa kwa kiwango cha dola, na marupurupu makubwa kwa wafanyakazi wa nje, ni hatua zinazoneemesha wageni zaidi kuliko wenyeji ambao ilitarajiwa wanufaike na maliasili iliyoko nchini kwao.
Lipo tatizo la serikali kutoa misamaha ya kodi hata isiyofikirika kwa makampuni ya kigeni ikiwemo ile ya kulipa tozo dogo la mrabaha la dola 30 kwa kila wakia moja yenye thamani ya dola 1,000.
Mwaka jana, 2010, serikali iliifanyia marekebisho makubwa sheria ya madini. Lakini, bado kiwango cha mrabaha cha asilimia 4 kilichowekwa kutoka asilimia 3.8 ni kidogo kulinganisha na thamani halisi ya maliasili inayovunwa na kupelekwa nje.
Takwimu zinaonyesha mauzo ya nje ya dhahabu peke yake yalichangia asilimia 40 ya mapato yote yaliyotokana na uuzaji wa mazao yaliyozalishwa nchini kwa mwaka wa fedha uliopita.
Wataalamu wa uchumi wanasema mazingira mazuri ya kijiolojia na hali tengamano kisiasa iliyopo nchini, zimesaidia ukuaji wa sekta hii.
Lakini, tatizo kubwa kwa sasa ni ukuaji wa sekta hii kutosaidia ustawi wa jamii zinazoishi ilipo migodi.
Pale wawekezaji wanapovuna utajiri na kuusafirisha nje kibiashara, wenyeji wanabaki na mashimo na mazingira yaliyochafuliwa.
Wapo wanaosema Tanzania inajitakia kukosa mapato stahili. Kwa mfano, iweje viongozi waridhike na hata kusaini mikataba ya uchimbaji madini isiyozingatia maslahi ya nchi?
Iweje waziri alazimike kwenda Ulaya kusaini mkataba wa kuruhusu kampuni ya kigeni kuchimba madini nchini?
Kile alichowahi kukisema Rais Jakaya Kikwete kuwa utaalamu mdogo miongoni mwa Watanzania katika mikataba ya kimataifa, huchangia mikataba ya namna hiyo, hakikubaliki.
Kauli hiyo, inabeza msimamo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliyetambua umuhimu wa maliasili ya madini hata kuamua kutoruhusu makabaila kuingia.
Akikataa kuruhusu wageni kuchimba madini, Mwalimu alisema, “Maliasili za nchi yetu, kama madini, ni kwa ajili ya Watanzania wa leo, wa kesho na wa keshokutwa.”
Ndiyo maana alikataa hoja za kukaribisha wawekezaji, kuja kupora madini yetu.
Alitaka wachimbaji wadogo waendelee kuchimba madini kwa kuamini mavuno wakati ule yalitosheleza haja ya kuinua ustawi wao na uchumi wa nchi. Alichukia falsafa ya “hatutakuwepo watajiju” na aliamini kuchimba zaidi ingekuwa ulafi!
Laiti sekta hii ingesimamiwa vizuri, tija ingepatikana na kuchangia kupunguza umasikini. Tungeshuhudia maendeleo makubwa maeneo yanayozunguka migodi.
Miradi michache ya kijamii ambayo wawekezaji wanasifia kuigharamia kama hisani na siyo shuruti kimkataba, si endelevu na thamani yake kifedha haiendani na kiwango cha faida waipatayo.
Mfano mzuri ni Mwendakulima, kijiji cha wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Wananchi wanalalamika ahadi za wawekezaji wa mgodi wa Buzwagi, hazijatimizwa.
Waliahidiwa barabara nzuri, maji safi na salama, zahanati ya kisasa, ukamilishaji sekondari ya kijiji ikiwemo maabara ambayo walijenga jengo tu.
Halmashauri ambayo hulipwa dola 200,000 (zaidi ya Sh. 300 milioni) kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya watu, ndiyo iliyopaswa kuweka vifaa vya maabara. Haijatekeleza.
Badala yake, iliamuru wanakijiji wachangie ununuzi wa madawati. Kumbe, fedha hizo zinazotolewa na wawekezaji hazipelekwi moja kwa moja kwao, bali hujumuishwa na mapato ya wilaya na kupangwa mipango inayofikiria maeneo yote.
Mipango ya halmashauri si lazima iwe ndiyo vipaumbele vya eneo ulipo mgodi.
Tangu mwaka 1998 kampuni ya Resolute Co., Limited ya Australia ilipoanza kuchimba dhahabu mgodi wa Lusu chini ya mradi wa Golden Pride, wananchi wanaoishi maeneo yanayouzunguka, hawana cha kujivunia.
Miongoni mwao ni zaidi ya watu 1,000 waliokuwa wakinufaika na mgodi huo, wilayani Nzega, mkoani Tabora, kupitia uchimbaji mdogo.
Hawakulipwa fidia. Wajasiriamali wakiwemo mamia ya wanawake, waliokuwa wakitoa huduma ya biashara mbalimbali eneo la machimbo, siyo tu hawakulipwa kitu, bali hata mali zao zilizoteketezwa wakati wa uvunjaji makazi ya wachimbaji, hazikujaaliwa fidia yoyote.
Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari wakati ule wala sasa kusikiliza kilio cha watu hao ingawa viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini walifika Lusu. Wote waliondoka kwa kuahidi kutafuta ufumbuzi. Hakuna aliyerudi kutimiza ahadi.
Wakati viongozi wakikwepa uwajibikaji, vijiji karibu vyote vinavyopakana na mgodi havina huduma ya maji safi. Lakini, lita zipatazo milioni moja huteketea kila mwezi kwa shughuli za mgodi.
Sasa baadhi ya mashimo ya uchimbaji yanafungwa, huku shimo jipya likisubiriwa kuanza uchimbaji. Hakuna taarifa muafaka za jambo hili. Wananchi hawajajulishwa; wala mali zao zikiwemo makazi, hazijatathminiwa. Nani anajali?
Somo: Tusikubali kuingiza mwekezaji mgodini bila kujua hatima ya wachimbaji wadogo; bila kujua manufaa watakayopata wananchi wa karibu na mgodi. Hawa wamilikishwe hisa na kuhakikishia wananchi miradi ya kijamii. Vinginevyo, jitihada za uwekezaji katika sekta hii zitakuwa sawa na kupiga ngumi ukuta; na matamshi ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja hadi bungeni, yatamrudia.
 
Naona pesa ya Mengi imeanza kufanya kazi ya kumchafua mhongo.
Mkuu mbona unapotoka? Mtu mchafu kama Muhongo atachafuliwa vipi wakati mchafu tayari? data zake za uongo, kuwanyima watanzania haki ya kumiliki rasilimali zao kwako si uchafu? kuukana uraia wake na baadae kurudi kama mamluki kwaajili ya kuwatumikia mabwana zake Ballali Style kwako si uchafu?...
 
mengi ni muongo na mnafiki, aliahid kima cha chin mishahara wafanyakaz wake 400,000/- lkn mpaka sasa hajatekeleza, wafanyakaz wa makampuni ya ipp hali mbaya mzee mengi ni mnyonyaj kwa wafanyakaz wazawa kwenye makampuni yake ss atawezaje kutumia rasilimali kuwanufaisha watz, usipokua mwaminifu ktk lililo dogo huwez kua mwaminifu kwa lililo kubwa
 
mengi ni muongo na mnafiki, aliahid kima cha chin mishahara wafanyakaz wake 400,000/- lkn mpaka sasa hajatekeleza, wafanyakaz wa makampuni ya ipp hali mbaya mzee mengi ni mnyonyaj kwa wafanyakaz wazawa kwenye makampuni yake ss atawezaje kutumia rasilimali kuwanufaisha watz, usipokua mwaminifu ktk lililo dogo huwez kua mwaminifu kwa lililo kubwa
Simply you don get it... Hapa tunaangalia maslahi mapana ya wananchi kumiliki rasilimali zao Gesi na Madini badala ya hali ilivyo sasa rasilimali hizo zinamilikiwa na wageni kwa 100%... DSE iko kwaajili ya nini? kwanini Barrick et al huwa wanapeleka kuuza hisa zao London? kwanini mapato ya madini yasihifadhiwe kwenye mabenki yetu ili tuweze kuratibu ulipaji kodi?... fanya utafiti kabla ya kuropoka mkuu...
 
mengi ni muongo na mnafiki, aliahid kima cha chin mishahara wafanyakaz wake 400,000/- lkn mpaka sasa hajatekeleza, wafanyakaz wa makampuni ya ipp hali mbaya mzee mengi ni mnyonyaj kwa wafanyakaz wazawa kwenye makampuni yake ss atawezaje kutumia rasilimali kuwanufaisha watz, usipokua mwaminifu ktk lililo dogo huwez kua mwaminifu kwa lililo kubwa
Well said mkuu - Charity begins at home.
 
Kutokana na upeo wako mdogo wakufikiri ndio unaona hvyo ila kwa wale tunao mfahamu Mengi tunajua anatetea maslahi ya watanzania juu ya umilikaji wa rasilimali za taifa.

Toka lini Bepari akatetea maslahi ya wananchi? Umeona wapi hii? Hana jipya sana sana hawa wanamambo yao ambayo pengine hatuyajui, ila HAITOTOKEA hata siku moja Bepari akatetea maslahi ya wananchi, NEVER labda kama anataka kuingia kwenye siasa tena atawalaghai muone anawatetea na mkimpa tu kura buuuuuuuu anaingia mitini kuendelea kuwanyonya kwa kutumia passport ya.....
 
Mengi anasema kuwa Dhahabu yote ya Tanzania inathamani ya dolla 60 Billion ambapo wageni wanamiliki 99.99% Iweje Gesi yenye thamani ya dola 500 Billion iendelee kumilikiwa na wageni kwa 100%?... Mengi hapa anapoint, wananchi wa Mtwara nao wanastahili kuungwa mkono kwa nguvu zote!!! Dhahabu inakwisha, Almasi wameshaimiliki kabla ya uhuru, Tembo na wanyama wengine wanauawa, iko siku Mt Kilimanjaro nayo watailipua...sijui tutabaki na nini zaidi ya mabusha na vitumbua...Prof Muhongo pamoja na kwamba wewe ni EHM unaetumiwa na mabwana zako wa ulaya lazima utambue kuwa nchi hii inatuhusu sote...fedha za Mobutu ziko wapi? mitego ya kuwekewa fedha Uswis ni wa kishamba wanakuhadaa hao mabazazi... siku si nyingi utatukumbuka ...
HIVI NIULIZE WAZIRI ANAPOSEMA 70% YA MINING CONCESSIONS ANA MAANA GANI KUWA 70% YA MINING RESOURCE UNDER CONTROL OF THE INDIGENOUS PEOPLE AU ANAMAANISHA NINI. KAMA 70% YA RASLIMALI MADINI ZINAZOCHIMBWA ZIPO CHINI YA WAZAWA NINA IMANI TUNGEKUWA MBALI SANA . LAKIN WAZIRI ANACHEZA NA AKILI ZA WATU TUNACHOTAKA NI SEHEMU YA MAPATO INACHUKULIWA NA WAZAWA NA SIO WATU SABIN KATIKA MIA WENYE UWEZO WA KUCHIMBA MADINI ANAYOCHIMBA TAJIRI 1 KUTOKA KUNDI LA 30% mUHONGO HIYO HESABU NI YA WAPI?
 
Mengi Ana washabiki wake na Muhongo Ana washabiki sasa liandaliwe pambano la Ngumi uwanja wa taifa Tujue ni nani Zaidi ktk nguvu za mikono kinyume na hapo watu watashabikia malumbano ya Wazee wawili pasipo kujua hatma yake

Hatima yake ni Umeme umepanda mpaka Tshs 100/= kwa Unit, Migao ya kifala ---- kila wakati bila taarifa!!
 
Mengi anasema kuwa Dhahabu yote ya Tanzania inathamani ya dolla 60 Billion ambapo wageni wanamiliki 99.99% Iweje Gesi yenye thamani ya dola 500 Billion iendelee kumilikiwa na wageni kwa 100%?... Mengi hapa anapoint, wananchi wa Mtwara nao wanastahili kuungwa mkono kwa nguvu zote!!! Dhahabu inakwisha, Almasi wameshaimiliki kabla ya uhuru, Tembo na wanyama wengine wanauawa, iko siku Mt Kilimanjaro nayo watailipua...sijui tutabaki na nini zaidi ya mabusha na vitumbua...Prof Muhongo pamoja na kwamba wewe ni EHM unaetumiwa na mabwana zako wa ulaya lazima utambue kuwa nchi hii inatuhusu sote...fedha za Mobutu ziko wapi? mitego ya kuwekewa fedha Uswis ni wa kishamba wanakuhadaa hao mabazazi... siku si nyingi utatukumbuka ...

TAARIFA YA DKT. REGINALD A. MENGI MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 20 DESEMBA 2013

Baada ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe 16 Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho nimekuwa nikipigania. Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana.

Ningependa kuwaeleza Watanzania wenzangu yafuatayo.

Profesa Muhongo ni muongo
Imefika wakati wa Watanzania kubaini kwamba Mhe. Profesa Muhongo ni mtu mwenye hulka ya kusema uongo. Kwa mfano:

1. Kwenye kongamano la tarehe 8 Desemba 2013, Mhe. Profesa Muhongo alisema kwamba moja ya kazi yake, alipokuwa akifanya kazi kama mwanasayansi huko nje, ilikuwa kutabiri umuhimu wa sayansi katika uchumi wa dunia miaka 3,000 ijayo. Huu ni uongo wa mchana kweupe.

2. Mnamo Julai 2012 Mhe. Profesa Muhongo aliwaahidi Watanzania kwamba hakutakuwa na mgawo wa umeme tena. Sote tunashuhudia mgao wa umeme ukiendelea hadi sasa.

3. Mnamo mwezi Septemba 2012, Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akizungumzia mikataba ianayohusiana na vitalu vya gesi akisema kwamba “baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa” na “sitovumilia mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache”. Baada ya hapo, Mhe. Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi uliopangwa kufanyika mwezi huo na kupitia upya mikataba yote iliyokuwepo awali. Sasa zaidi ya mwaka umepita na Mhe. Profesa Muhongo hajarekebisha mkataba hata mmoja.

Profesa Muhongo na takwimu zake za maeneo ya madini

1. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Profesa Muhongo alitoa takwimu za kuonyesha kwamba mimi ninamiliki eneo kubwa mara tatu ya Dar es Salaam kupitia kampuni zangu tanzu.

2. Jumapili iliyopita mimi nilimjibu Mhe. Profesa Muhongo kwa kumueleza kwamba takwimu zake kuhusu mimi ni za uongo, na vilevile hizo alizotoa Bungeni pia ni za uongo na nilimweleza kwamba swali la Mhe. Tundu Lissu lilikuwa ni “nani anamiliki maeneo ya migodi”.

3. Katika eneo la kutafuta madini unaweza ukapata au ukakosa – ni bahati nasibu, ndiyo maana maeneo ya utafutaji yanakuwa makubwa. Vilevile wakati unatafuta madini shughuli nyingine za wananchi waliopo katika eneo hilo huwa zinaendelea, kwa mfano kilimo, makazi, uchimbaji mdogo mdogo nk. Unapopewa leseni ya mgodi inamaana kwamba tayari umeshapata bingo – madini yapo na unaanza kuchimba. Kwa mantiki hiyo maeneo ya migodi inakuwa midogo – isiyozidi kilomita 10 za mraba, na shughuli zote za wananchi katika eneo hilo zinasitishwa.

4. Sasa kwenye maelezo yangu ya Jumapili iliyopita nilitamka wazi kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja tu wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba. Profesa Muhongo hajakanusha hili, badala yake anaturudisha Watanzania kule kule kwenye maeneo ya utafutaji badala ya migodi.

5. Siyo hilo tu. Mhe. Profesa Muhongo anafahamu kwamba kuna aina 6 za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini. Lakini kwa makusudi kabisa Mhe. Profesa Muhongo anafananisha leseni ya Mtanzania anayetafuta au kuchimba kokoto na leseni ya mwekezaji wa kigeni anayetafuta au kuchimba urani au dhahabu. Kweli unaweza kufananisha kokoto na dhahabu?

6. Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa utafutaji madini (mineral prospecting) ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta ya madini kwa sababu bila utafutaji hakuna ugunduzi na uendelezaji wa migodi hapa nchini. Lakini kuanzia Julai mwaka jana Waziri Muhongo alipandisha tozo za vitalu kwa asilimia kati ya 100 na 500. Matokeo yake Watanzania wengi wanarudisha leseni zao na kasi ya ugunduzi wa migodi imepungua.

7. Nia ya mtu inajionyesha siyo tu kwa yale anayosema lakini bali pia kwa yale anayoacha kusema. Sasa kama kweli nia ya Mhe. Profesa Muhongo ni nzuri, kwa nini hatoi takwimu zinazohusu gesi? Kwa mfano, kwa nini hawaambii Watanzania kwamba:

a. Eneo ambalo limeshatolewa kwa ajili ya mafuta na gesi lina ukubwa wa kilomita za mraba 243,000 ambalo ni sawa na karibu robo ya eneo la Tanzania nzima au mara 175 ya eneo la mkoa wa Dar es Salaam au eneo la mikoa 9 ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga na Kagera.
b. Kwa nini Mhe. Profesa Muhongo hataki kuwaambia Watanzania kwamba hakuna hata mzawa mmoja anayemiliki kitalu cha kutafuta au kuchimba mafuta na gesi?
c. Kwa nini Mhe Profesa Muhongo hataki kuweka wazi kwamba vitalu vyote 27 vya gesi ambavyo vinaanzia katika mpaka wetu na Kenya hadi mpaka wetu na Msumbiji, vimegawiwa kwa wageni? Je, kugawa vitalu vyote vya gesi kwa wageni siyo hatari kwa mustakabali wa usalama wa taifa letu?
d. Lakini cha muhimu ni kwamba Watanzania wafahamu kwamba gesi ambayo imeshagunduliwa Tanzania inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 500 bilioni wakati dhahabu yote iliyokwishagunduliwa hadi sasa na bado haijachimbwa inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 60 bilioni kwa bei ya sasa ya dhahabu.

Kwanini Profesa Muhongo hawaambii Watanzania takwimu hizi?

Profesa Muhongo na kauli zake kwamba Watanzania hawawezi kushiriki katika mchakato wa mafuta na gesi

1. Mara nyingi tumesikia kauli za Mhe. Profesa Muhongo kwamba Watanzania hatuwezi kufanya biashara ya mafuta na gesi kwa sababu biashara hiyo inahitaji mtaji mkubwa na utaalamu, vitu ambavyo Watanzania hawana. Mhe. Profesa Muhongo amewahi kusema kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri, wavivu wa kusoma na washamba sana katika masuala ya uwekezaji na kwamba uwezo walionao Watanzania ni kuuza juisi au soda. Huu ni uongo. Watanzania wanajua wanachokisema na gesi yetu ni mtaji mkubwa sana.

2. Kwanza kabisa katika karne ya 21 utalaamu ni bidhaa ambayo mtu asiye nayo anaweza kuinunua. Mhe. Profesa Muhongo anaweza asilifahamu hili kwa sababu yeye mwenyewe hajawahi kufanya biashara katika maisha yake – anayasoma masuala ya biashara kwenye makaratasi tu.

3. Namsihi Mhe. Profesa Muhongo akumbuke kwamba gesi ni mali ya Watanzania na wana haki ya kuzaliwa ya kumiliki rasilimali yao ya gesi.

4. Mhe. Profesa Muhongo anataka Watanzania waamini kwamba kuna mwekezaji wa nje anaweza kumiliki na kuendesha kitalu kwa fedha zake yeye mwenyewe. Hii si kweli. Fedha zinazotumika ni za watu wengi waliowekeza katika masoko ya hisa. Sisi pia tungehamasishwa na kuwezeshwa, tunaweza kuunganisha nguvu zetu hivyo hivyo na kuwekeza katika gesi yetu kwa kushirikiana na wageni. Mimi sipingi uwekezaji wa wageni. Watanzania nao washirikishwe katika umilikaji. Mgeni aje mwenyeji apone, siyo mgeni aje mwenyeji akose fursa ya kushiriki katika umiliki wa uchumi wake.

Profesa Muhongo hana nia nzuri kuhusu ushirikishwaji wa Watanzania katika gesi ?

1. Katika kongamano lilofanyika tarehe 8 Desemba 2013 Mhe. Profesa Muhongo alisema Watanzania wenye uwezo wa kifedha wazipeleke TPDC tarehe 10 Desemba 2013 na watapewa vitalu vya gesi. Vilevile alisema kwamba baada ya tarehe hiyo, hoja ya suala la wazawa kumiliki vitalu litafungwa. Watu waliokuwepo kwenye hilo kongamano walipigwa butwaa kwa sababu Profesa Muhongo alishanukuliwa akisema kwamba kwenye uongozi wake wazawa hawatapewa vitalu vya gesi na kwamba “suala la vitalu halina mambo ya uzawa”.

2. Kwa kuzingatia kwamba maagizo ya Mhe. Profesa Muhongo yalikuwa ni batilii (huwezi kutangaza zabuni kwenye kongamano) wafanyabiashara wa Tanzania walimpuuza na hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba haya mazingaombwe ya Mhe. Profesa Muhongo yalitufumbua macho Watanzania kung’amua kwamba kumbe kazi ya TPDC ni kupokea maagizo tu na anayegawa vitalu vya gesi ni Profesa Muhongo mwenyewe.

3. Nimekuwa nikirudia mara kwa mara kwamba mtaji sio tu fedha hata rasilimali kama gesi ni mtaji.
Hitimisho

1. Ningependa kutofautiana na Mhe. Profesa Muhongo na kusema kwamba adui wa maendeleo ya Watanzania siyo Watanzania wenyewe kama alivyosema ila ni Watanzania wachache sana wenye kauli za dharau za kutuambia kwamba Watanzania hatuwezi.

2. Katika suala la gesi mimi sipiganii mambo yangu binafsi, kwa sababu mimi nimeshafanikiwa kibiashara. Ninachopigania ni Watanzania wenzangu nao wapate fursa. Naomba nieleweke kwamba ninaposema Watanzania nina maana kuanzia yule mfanyabiashara mdogo wa sekta isyo rasmi, mfanyabiashara wa kati na wafanyabiashara wakubwa. Nataka kuwepo sera ambayo itahakikisha kwamba wanawezeshwa na siyo kusema tu kwamba hawawezi. Nafanya hivyo kwa sababu ninaamini kwamba utajiri uliobarikiwa ni ule uliopatikana kwa njia halali na unatumika kusaidia wanaohitaji msaada.

3. Ni wazi kwamba Mhe. Profesa Muhongo anachuki binafsi na mimi. Hii ni utashi wake, siyo lazima anipende na mimi siyo lazima nimpende. Lakini suala la gesi ni kubwa mno kuliko mahusiano kati ya Mhe. Profesa Muhongo na mimi – linagusa kila Mtanzania wa leo na wa vizazi vijavyo. Kwahiyo napenda kumsihi ndugu yangu Mhe. Profesa Muhongo aache kuchanganya chuki zake binafsi kwenye suala la gesi.

Dr. Reginald Mengi
Dar es Salaam
 
Mkuu mbona unapotoka? Mtu mchafu kama Muhongo atachafuliwa vipi wakati mchafu tayari? data zake za uongo, kuwanyima watanzania haki ya kumiliki rasilimali zao kwako si uchafu? kuukana uraia wake na baadae kurudi kama mamluki kwaajili ya kuwatumikia mabwana zake Ballali Style kwako si uchafu?...

wewe ndio unapotoka, huo ushahidi wa kuukana uraia wake uko wapi? ushahidi wa kuwatumikia watu wengine zaidi ya sisi maskini uko wapi? Data za uongo ziko wapi, mhongo katoa data, mengi katoa data ni jukumu lako kutafuta usahihi wa data. Muhongo kaongelea Mengi kuhodhi vitalu vya madini dar x3, mengi anajibu nina vitalu vya gesi=0, wapi na wapi kama sio usanii?
Phd ya Mengi haitambuliki dunia nzima, nani muongo hapo?
Mnapoongea leteni ushahidi sio kuropoka tu.
 
Kutokana na upeo wako mdogo wakufikiri ndio unaona hvyo ila kwa wale tunao mfahamu Mengi tunajua anatetea maslahi ya watanzania juu ya umilikaji wa rasilimali za taifa.
Hakuna mahali popote duniani bepari aliwahi tetea maslahi ya wananchi, Mengi anatetea maslahi yake, watetezi wa wanyonge siku zote hufa maskini kama Nyerere na kina Ken Saro Wiwa
 
HIVI NIULIZE WAZIRI ANAPOSEMA 70% YA MINING CONCESSIONS ANA MAANA GANI KUWA 70% YA MINING RESOURCE UNDER CONTROL OF THE INDIGENOUS PEOPLE AU ANAMAANISHA NINI. KAMA 70% YA RASLIMALI MADINI ZINAZOCHIMBWA ZIPO CHINI YA WAZAWA NINA IMANI TUNGEKUWA MBALI SANA . LAKIN WAZIRI ANACHEZA NA AKILI ZA WATU TUNACHOTAKA NI SEHEMU YA MAPATO INACHUKULIWA NA WAZAWA NA SIO WATU SABIN KATIKA MIA WENYE UWEZO WA KUCHIMBA MADINI ANAYOCHIMBA TAJIRI 1 KUTOKA KUNDI LA 30% mUHONGO HIYO HESABU NI YA WAPI?

Maana yake ni kuwa katika sekta ya madini Mengi na wenzake wana 70% ya vitalu vyote vya madini Tanzania. Hii ilikuwa kuthibitisha kuwa Mengi and co, hawana hela ya kuendeleza vitalu, ndio maana pamoja na kuhodhi hiyo percentage, bado mambo ni bila bila! sasa wanataka pia wahodhi vitalu vya gesi badala ya kupambana na watu wenye hela Taifa lipate faida.
 
Hatuhitaji madalali kama tuko tayari na tunauwezo tutachukua 'share' kwenye makampuni ya taifa.
 
Kutokana na upeo wako mdogo wakufikiri ndio unaona hvyo ila kwa wale tunao mfahamu Mengi tunajua anatetea maslahi ya watanzania juu ya umilikaji wa rasilimali za taifa.

Acha porojo Dr Mengi anatetea mslahi ya watanzania wapi?? Kaulize anavyowalipa wafanya kazi wake ndo utajua kama mzee huyu anamaslahi na taifa au hapana . Hili swala la gesi siyo la porojo porojo wazawa kama tunaweza basi atuna buti kushindana na wawekezaj. Kama hatuwezi tuliachie TPDC lituwakilishe watanzania wote

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Kutokana na upeo wako mdogo wakufikiri ndio unaona hvyo ila kwa wale tunao mfahamu Mengi tunajua anatetea maslahi ya watanzania juu ya umilikaji wa rasilimali za taifa.

kwa kuwalisha maskini, hebu mengi atueleze ni kwa namna gani migodi anayoimiliki nchini inavyolipa kodi kwa serikali? afafanue ni kwa namna gani hao anaowaita watanzania wanaweza kupata fedha za kuwekeza ikiwa hata gharama za maisha kwao bado ni mzigo. mengi hapa anataka kubadilisha mada kwamba tutoe rasilimali zetu kwa baadhi ya watanzania kisha waweze kuivuruga serikali kwa pesa zao chafu. hii haikubaliki hata kidogo. sisi watanzania tutawekeza kwenye sekta hii kupitia kampuni yetu ta TPDC ambayondiyoyenye leseni ya kuchimba gesi. hisa zitauzwa pole soko la hisa la dar es salaam. kisha wote kwapamoja tushindane kununua vipande. mengi nimlafi tuwala hana hoja ...asubiri chakula kiive apakuliwe ashindane na wengine.TAIFA KWANZA
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATOTO WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom