Tumuelimishe kidogo Prof. Muhongo kuhusu hii miradi ya Maji ya kuzalisha umeme. Watanzania tuelewane

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Wiki iliyopita tumemsikia Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa zamani Prof. Sospeter Muhongo akidai tuachane na miradi ya umeme wa maji kwa kile alichokidai inachelewa kutoa matokeo na kukupa umeme wa gharama nafuu kwa muda mrefu sana. Sasa hoja kama hizi hata kama ni mufilisi lakini ni vyema zaidi zikajibiwa kwa hoja na sasa tuanzie hapo.

Sasa inawezekana Watanzania walio wengi wanaona na kusikia tu kuhusu habari ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Megawatts 2115 kutoka kwenye Mto Rufiji, mradi uliobuniwa na kuasisiwa na Mwalimu Nyerere toka mwaka 1975 na kuanza kutekelezwa na Rais wa awamu ya 5 Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli.

Tumesikia habari ya ukubwa wake huo mradi, gharama ya utekelezaji, umeme unaoenda kuzalishwa na mambo mengine mengi sana kuuhusu mradi huo mkubwa wa Stieglers Gorge (Bwawa la Mwalimu Nyerere). Sasa leo ngoja tuumulike kidogo mradi huu wa umeme wa maji, tujue idadi ya namba zilizoko za gharama na Megawatts zinazoenda kuzalishwa hapo na tafsili yake kwa Watanzania na uchumi wetu.

Kwanza kuingia kwa Serikali ya awamu ya 5 kulifungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa ya toka mwaka 1975 ya kutaka kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Rufiji. Mradi huo mkubwa kabisa ni wa 4 kiukubwa kwa uzalishaji wa umeme barani Afrika unaoenda kuzalisha Megawatts 2115 kwa gharama ya Trilioni 6.5.

Adhima ya utekelezaji wa mradi huo inakuja wakati nchi ikiwa kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, shindani na wenye kuleta maisha bora kwa watu ambao kwa kiwango kikubwa unategemea sana nishati umeme ya kuwezesha viwanda kupata nishati ya kutosha ili iweze kuzalisha vya kutosha na muhimu zaidi kwa gharama nafuu. Viwanda ni umeme na umeme ni viwanda.

Yote 9 lakini 10, licha ya yote ni wangapi tunaelewa tafsiri halisi ya Megawatts 2,115 za umeme zinazoenda kuzalishwa pale Mto Rufiji? kwa sisi watu wa kawaida ambao si wataalamu wala wahandisi tunaelewa nini kuhusu Megawatts 2115? twende sawa hapo chini.

Kuzielewa Megawatts 2115 na ukubwa wake ni rahisi ukipitia na kujua matumizi ya umeme na mahitaji ya umeme kwa taifa letu. Mfano mwepesi tu ni kwamba mahitaji halisi ya umeme kwa mikoa kama ya Mtwara na Lindi ili umeme usikatike hata sekunde ni Megawatts 22 hadi 30 tu.

Tanzania ina mikoa 31, hivyo ukifanya kila mkoa upate Megawatts 50 tu kama makadirio ya juu kabisa hata kwa mikoa isiyozidi matumizi hayo maana yake ni sawa na kupeleka bahari ya umeme kila mkoa na bado matumizi yetu tutaishia Megawatts 1,550 na bado zitabaki Megawatts 565 kama akiba ya umeme tuliyoiweka kibindoni. Bado hiyo Megawatts 50 kiwastani hata ukijumlisha mikoa yenye viwanda vingi na vikubwa kama Pwani, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza bado ni kubwa sana. Nimeweka kwa kiwango cha Juu sana usisahau matumizi ya Mtwara na Lindi ni Megawatts 22- 30 tu.

Ina maana hapo tunaenda kuua kabisa stori za mgao wa umeme na mambo ya umeme kukatikakatika. Hapo wenye viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kabisa watazalisha bidhaa zao bila tatizo na zaidi kwa gharama nafuu kutegemeana na urahisi wa gharama kwa umeme huu wa maji.

Kumbuka mpaka sasa nchi nzima kutoka kwenye vyanzo vyetu vya kuzalisha umeme vya Kinyerezi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na kwingine tunazalisha Megawatts 1601 tu lakini Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee yake linaenda kutupa Megawatts 2115, umeme wa uhakika tena wa maji ambao ni rahisi zaidi kuliko aina yoyote ile ya umeme duniani ukiachana na wa jua, upepo, nyuklia, makaa ya mawe, mafuta na gesi .

Tukumbuke umeme unaozalishwa na maji ndio umeme wa gharama nafuu na rahisi zaidi kuliko umeme wowote ule duniani. Kumbuka uniti 1 inayozalishwa na maji ni shilingi 36, nyuklia shilingi 65 kwa uniti, wa upepo 103.5, jua pia 103.5, wa makaa ya mawe uniti shilingi 114, wa joto ardhini 118, wa gesi 147 na wa mafuta ambao ndio tunautumia sana tukinunua kwa gharama ya juu sana kati ya shilingi 440 hadi 600.

Hii tafsili yake kukamilika tu kwa Bwawa la uzalishaji wa umeme la Mwalimu Nyerere kutashusha kwa kiwango kikubwa sana gharama ya umeme mpaka shilingi 36 tu kwa uniti hivyo kutoa nafasi kwa bidhaa zetu za viwanda nazo kushuka sana, matumizi ya kawaida nyumbani kushuka maradufu na hata kwa watanzania watakaofungua viwanda vidogo kwa vikubwa wakinufaika sana na gharama ndogo ya uzalishaji wa bidhaa itakayoleta neema na nafuu mpaka kwa watu wa hali ya chini kabisa, machinga, mama nitilie, wajasiriamali na makundi mengine. Zaidi kuvutia uwekezaji.

Unapokuwa na umeme wa uhakika, lakini sio wa uhakika tu tena na wa gharama nafuu ya bei tayali unavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kujenga viwanda hapahapa. Suala la uhakika wa umeme na nafuu yake ni mambo ya msingi sana na ya kwanza kabisa kwa mwekezaji yeyote anayefikiri kwenda kuwekeza sehemu yoyote ile kwasababu kiwanda ni nishati.

Vipi umefikilia hizo Megawatts zingine zaidi ya 565 ambazo tunakuwa tumezitia kibindoni baada kujihakikishia uhakika wa umeme nchi nzima? hapo tunaweza kuamua kuuza kwa majirani zetu hapo Kenya, Malawi, Uganda au Msumbiji ambako tunajua bado hawana uhakika wa umeme. Hapo unazungumza kuhusu umeme wa Rufiji tu, hujaenda Kinyerezi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na kwingine ambako umeme unaendelea kuzalishwa ambao kwa ujumla unafika Megawatts 1601.

Kwa tafsiri, kukamilika tu kwa Bwawa la Mwalimu Nyerere nchi yetu itakuwa na akiba na ziada ya umeme unaofikia mpaka Megawatts zaidi ya 1000. Hii ziada sasa baada ya kujihakikishia umeme wa kutosha ndani tutaamua wenyewe kuipiga hela nje na kama nilivyosema majirani zetu wote hawana umeme wa uhakika hivyo kuweka hela za kigeni kibindoni na kuzipeleka kwenye sekta zingine za uchumi na maendeleo. Nadhani Watanzania mtakuwa mmenielewa na ujumbe utamfikia Bwana Muhongo.
 
Na we umechanganya mada na kwamujibu wa andiko lako hata hatukupaswa kulia kukatika kwa umeme kwan kwamujibu kila mkoa utumie megawatts 50 kwa mikoa yote tutatumia 1550 wakat sisi kwasasa tunazalisha megawatts 1601 Sasa hii imekaaje na hali ya mgao uliokuwa unajitokeza au ulijitokeza ndugu?
 
Mm pamoja sikuahi kuwa mfoasi wa mwenda zake,ila umeme huo ukikamilika utasaidia sana.

Umeme wa nyukilia hiyo sahau pamoja ungewezekakana ungekua bora kuliko wa maji.
 
Mimi siko kwa Muhongo, lakini embu fikiria serikali ilikopa mabilioni ya fedha kuweka miundo mbinu ya kutoa gesi mtwara. Alipokuja marehemu akaona huo mradi haumjengei jina licha ya mabilioni yaliyokwisha tumika na ambayo ni mkopo unaotakiwa kurejeshwa. Akaamua aanzishe wa kwake bila kujua serikali na rasilimali ni zile zile.

Unaweza kuwa na mawazo mazuri ila ukafeli kwa kukosa mipango na njia sahihi ya kutekeleza wazo lako.

Mwalimu Nyerere alituasa kupanga ni kuchagua.

Cha muhimu sasa nchi imeingizwa kwenye utawala wa awamu ya 6 na MUNGU mwenyewe. Tuangalie tusije tukaaharibu kwa papara na kupenda sifa kusiko na busara.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU?
 
Mimi siko kwa Muhongo, lakini embu fikiria serikali ilikopa mabilioni ya fedha kuweka miundo mbinu ya kutoa gesi mtwara. Alipokuja marehemu akaona huo mradi haumjengei jina licha ya mabilioni yaliyokwisha tumika na ambayo ni mkopo unaotakiwa kurejeshwa. Akaamua aanzishe wa kwake bila kujua serikali na rasilimali ni zile zile...
 
Hawa viongozi wengine ni tabu tupu! Eti na Muhongo hapo kashauri, anashauri ujinga
Report ya CAG imewavuruga vichwa hao yatima, Yamebaki kushauri upuuzi tu..
IMG_20210411_143317.jpg
 
Mm pamoja sikuahi kuwa mfoasi wa mwenda zake,ila umeme huo ukikamilika utasaidia sana.

Umeme wa nyukilia hiyo sahau pamoja ungewezekakana ungekua bora kuliko wa maji.
Hivi tunakwama wapi na mradi wa Nuclear!? Make pale Dodoma kuna a lot of Uranium imegunduliwa toka 2010 kwani bado hatujapata wawekezaji hata wa kuchimba
 
Na we umechanganya mada na kwamujibu wa andiko lako hata hatukupaswa kulia kukatika kwa umeme kwan kwamujibu kila mkoa utumie megawatts 50 kwa mikoa yote tutatumia 1550 wakat sisi kwasasa tunazalisha megawatts 1601 Sasa hii imekaaje na hali ya mgao uliokuwa unajitokeza au ulijitokeza ndugu?
Mleta mada ameelezea vizuri ila kwenye suala la kukatika kwa umeme amejichanganya.

Umeme unapita hatua tatu muhimu kabla ya kumfikia mlaji.
- Ufuaji (Generation)
-Usafirishaji(Transmission)
-Usambzaji(Distribution)

Kwa muktadha huo, ikitokea hitilafu yoyote katika hatua mojawapo bila kujali ubora wa hatua zilizobaki mteja hatapata umeme.
Maana yake ni kwamba, unaweza ukafua umeme mwingi ila usafirishaji ukiwa dhaifu mteja hatapata umeme inavyotakiwa (utakuwa wa katika katika).
 
Na we umechanganya mada na kwamujibu wa andiko lako hata hatukupaswa kulia kukatika kwa umeme kwan kwamujibu kila mkoa utumie megawatts 50 kwa mikoa yote tutatumia 1550 wakat sisi kwasasa tunazalisha megawatts 1601 Sasa hii imekaaje na hali ya mgao uliokuwa unajitokeza au ulijitokeza ndugu?
Sure hajui hata anaongea nini
 
Hivi tunakwama wapi na mradi wa Nuclear!? Make pale Dodoma kuna a lot of Uranium imegunduliwa toka 2010 kwani bado hatujapata wawekezaji hata wa kuchimba
Nilisha eleza japo sio kuanzisha uzi ila kwa mchango tu.

Kuna kitengo cha umoja wa mataifa kinaitwa I.A.E.A. chenyewe kina kazi ya kusimamia mambo hayo ya uranium.

Wameweka vigezo na vigezo hivyo hakuna hata nchi moja kwenye bara la afrika lenye kutimiza vigezo vyao.

Hapa wazungu wanajua kwenye nchi yako ukiweza kurutubisha uranium utaweza kuzalisha umeme mwingi na wa uhakika.

Ambao unaweza kuwafanya mjitegemee hasa kwenye maendeleo ya viwanda nk.

Lakini pia unaweza kurusha hata setelaiti yako na kujenga mawasiliano yako.
 
Duh noma sana!
 
Duh
 
Back
Top Bottom