Fact zipi? za kumilikisha wageni rasilimali zetu 100%? yaani wewe umwambie mzungu ajichimbie akirudisha gharama zake ndo aanze kulipa! Hiyo akili matope? Ukisema watanzania hawana mitaji ni dhihaka maana Ophir Gas ya Mkapa via Motto Mubanga wametengeneza trillion za kutosha kwa kuuza vitalu tu! Kwanini capita kwa watanzania isiwe hivyo vitalu kisha wawekezaji wakaingia ubia moja kwa moja na wazawa?...Serikali inayojinasibu kuwa itasimamia kwaniaba ya Wananchi mbona wameshindwa kwenye Dhahabu na Almasi?...Mengi anataka kufanya udalali anataka kutuzuga wazawa. Kila kitu amiliki yeye bana. Muongo anaongea facts
wewe ndio unapotoka, huo ushahidi wa kuukana uraia wake uko wapi? ushahidi wa kuwatumikia watu wengine zaidi ya sisi maskini uko wapi? Data za uongo ziko wapi, mhongo katoa data, mengi katoa data ni jukumu lako kutafuta usahihi wa data. Muhongo kaongelea Mengi kuhodhi vitalu vya madini dar x3, mengi anajibu nina vitalu vya gesi=0, wapi na wapi kama sio usanii?
Phd ya Mengi haitambuliki dunia nzima, nani muongo hapo?
Mnapoongea leteni ushahidi sio kuropoka tu.
Acha kugeneralise mambo
wewe! Mengi mliwauzia viwanda vipi? TBL? TCCC? ATCL?TRL? Tanganyika
packers? Magunia? Ngozi? General Tyre? Kiltex?Mwatex?Sunguratex?ZZK
Mbeya? TANCAT? NAFCO?... Acha porojo wewe kuwadi wa rasilimali za
Watanzania...kawaambie wakupe data za kutosha si unakuja hapa na porojo
zako za buku 7
The government says new investments in the blocks will be under new production sharing contracts where the state will take up to 75 per cent.
The production-sharing formula will either be 35 per cent to investors and 65 per cent to the government or 25 per cent to them and 75 per cent to us, President Jakaya Kikwete said at the launching ceremony.
The majority shares of the state in the new investments will be under the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) on behalf of the people."
Msiingie kwenye mjadala na kuanza kurusha mawe kama hamna taarifa za kutosha, mnapiga kelele tu.
Hiyo TPDC inachukua reference kutoka wapi? Shirika gani la uma limewahi kusimama badala ya watanzania na ikafanikiwa? kumbuka kuwa hawa Jamaa game wanalijua vizuri sana, wanatambua kuwa mali ya wote si ya yeyote...ndiyo maana wanahujumu kila shirika. TANESCO iko hoi, Reli, Bandari, ATC...???... Acheni kudanganya Watanzania ...Imetosha jamani, Zaidi ya miaka 50 sasa mnaendelea kuwapiga sound...
Sijui ni ufahamu mdogo
unakusumbua ama unatumika visivyo? wages kwa makampuni ambayo ni labor
intensive huwa inafika hadi 50% ya mapato ya kampuni! GGM walizalisha
zaidi ya $ 20 Billion kwa msimu wa 2011/2012 pekee, wazungu walilipana
bonus kibao! Mbona wabongo hawakulipwa chochote? MIshahara ya
wafanyakazi wa IPP na Bakhresa unategemeana na faida na mapato ya
makampuni husika!... Mbona Makampuni ya Simu hayalipi mamilioni wakati
wanatengeneza faida kubwa? Niambie Kampuni gani ya wawekezaji hapa Bongo
yenye kujali wafanyakazi wake kiasi cha kuwalipa hicho kiasi
unachotuambia! BP ya Waingereza ndo hovyo zaidi... Waambieni watawala
ukweli kuwa Sheria zetu na sera za CCM ndio kikwazo kikubwa, Kapuya
aliwahi kuwaambia wawekezaji wasilipe mishahara inayotofautiana sana na
ya serikali kwa kuhofia kuwa serikali itakosa watumishi! ... Makaburu
walisherehekea usiku kucha baada ya Chama cha Wafanyakazi kudai fedha
mbuzi wakati wanaingia TBL... kwa taarifa yako wawekezaji wengi hasa
kutoka ktk nchi za magharibi huwa wanatumia Ethnocentric model ambapo
mishahara na marupurupu yote inakuwa inaendana na rate ya nchi husika ie
going rate approach! Ni jukumu letu kama nchi kuweka wazi kuwa
mishahara itategemea parent company ilikotoka...