- Wa-Tanzania, tufike mahali tusikubali kudanganywa anytime unapoona kuna mtu au kiongozi anadai serikali au rais aingilie kati hili soo maana yake ni moja tu kwamba anataka Rostam aokolewe, ndio maana tunasema serikali na rais wakae pembeni, kwa sababu hakuna sheria iliyovunjwa so far Mzee Mengi kumtwanga Rostam na yeye kujibu, na sasa mahakama na Takukuru, ingawa ni fair kumuuliza Rostam kwa nini ameenda Takukuru badala ya mahakamani? Hili ni swali zito sana wananchi tunatakiwa kujiuliza WHY Takukuru? Kuna nini huko?
- Kuitwa pembeni it is too late, na Mengi akikubali kuitwa pembeni ajue he is done(FINITO), maana the next thing watamchezea karata chafu sana kama walizomchezea DK. Salim kwenye uchaguzi wa 2005, sasa hivi Rostam na wapapmbe wake wamepagawa hawaamini, kwamba the mighty Rostam is in trouble, yes he is in trouble kwa sababu the more this war inaendelea kama ilivyo sasa ni more wananchi watajiunga na Mengi, huhitaji kuwa professor wa siasa kuelewa hili, The genius Rostam alikosea pale tu alipokubali kujitokeza Kempiski, ninasema hivi kwa mara ya kwanza toka aanze kuchanganya siasa na biashara he is in trouble tena big time, enzi zake rais angemuita Mengi na kumtuliza lakini not anymore, infact alikuwa amebanwa sana na Mengi kwamba akajaribu kuwatumia CC, huko wamemtolea nje sasa tuone kama Takukuru wana ubavu wa kumuosha, ananuka!
- Ya kuitwa pembeni Mengi asikubali ng'o! Akikubali tu ameisha na maji, Rostam hana ubavu tena, hata huko Mtandao ni Karamagi ndiye anaye-run the show anyways kwa sababu hawawezi tena ku-afford kuongozwa na a high profile na political liability kama Rostam, mambo yao huko gizani hufanikiwa wanaposhughulika bila kuonwa yaani chini ya radar, kwa hiyo hata huko sio siri nao wameshafika mwisho naye, mimi ninasema hivi ukimshika Rostam basi umekamata kichwa cha nyoka, akibanwa sana tutapata majibu ya maswali yote muhimu sana kwa mabadiliko ya taifa hili,
Huyu ndiye chanzo cha ufisadi wote nchini, majibu kama ya ufisadi wa Mkapa na Balali, yote anayo huyu, Mengi asikubali idea ya kuitwa pembeni akiendelea naye kwenye sheria, pole pole wananchi tutajiunga na hivi vita ndipo Rostam ataelewa kwamba kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, na hasa ufisadi! amani ya taifa letu iko sawa sana tena kuliko wakati wowote tuwe na uhuru, hii ishu iachwe itajifungua na kujifunga yenyewe, so far haijavunjwa sheria yoyote ya jamhuri!
Respect.
FMES!