Mengi VS Rostam: Where is the Government?

Mengi siyo mnafiki, kwa sababu alitoa shutuma zake mbele ya wananchi, na yuko kwenye record kimaandishi, sauti na picha za luninga.
 
How can the government investigate itself? Mnacheza nyinyi. Hapa hakuna lolote zaidi ya sarakasi na mazingaombwe.

Halafu malumbano ya hawa wawili sidhani kama yanaihusu serikali. Wao waachwe wapakane kwenye vyombo vya habari na mwishowe wataacha wenyewe.

Kinachoniogopesha tu ni kwamba malumbano ya hawa watu yana divert attention kabisa kutoka mafisadi nyangumi na papa wengine kama Li Mkapa na lile Li Mbuna, Mi Chenge..Mi Mahalu na mingineyo.

Upuuzi mtupu unaoendelea hapa.
Well said niko nyuma yako 100%
 
Naandika hii post kuwajuvya wamiliki wa hii Forum kuwa tuko hapa kuelimishana na kupeana habari,sasa mnapochaguwa kuficha vitu ambavyo sababu ni kuwa vinawagusa katika kuwabeba watu fulani katika jamii mnakuwa hamtutendei haki. Kuna post za upuuzi kabisa zikiwa na post tele mradi tu zinawakuneni mnachotaka na kuzificha zile mnazoona zinawaonyesha rangi halisi ya WAPENZI WENU.
Nafikiri hili linarudisha nyuma na kuudhi sana.
 
Eti mafisadi papa na mafisadi nyangumi - ha ha haaaa ! Kinachochekesha zaidi ni dai la kuwepo vita kati ya fisadi na fisadi, moja likiwa papa na lingine likiwa nyangumi. Ninachojua ni kuwa kama ingekuwa kweli hali ni hiyo, ingekuwa rahisi sana kundi moja kuliangamiza kundi lingine - kisa cha mafahali wawili.

Ninachojua ni kuwa kuna state sponsored ufisadi, hili la nyangumi na papa ni la kufikirika tu kwa sababu tunayo serikali moja inayotambulika. Hivyo ukitokea mvutano wowote ule lazima tukubali kuwa pande hizi mbili zinapingana na kwa hulka ya kibinadamu malengo yao hawa hayawezi kufanana kamwe.

Ama Mengi ni fisadi nyangumi na kaiweka serikali mfukoni na Rostam ni msafi na anatetea maslahi ya taifa au Rostam ni fisadi papa na ndiye kingmaker serikalini na Mengi ni mzalendo aliyechoshwa na ufisadi. Kufuatana na mambo yanavyozidi kufumka, jibu la hiki kitendawili haliko mbali na its just a matter of time.

Kila moja wetu kwa nafsi yake hivi sasa anajipanga nyuma ya mojawapo wa hawa mafahali. Tunachopaswa kujadili ni hili - kwa kuwa tuna serikali iliyowekwa madarakani kihalali, tumefikafikaje katika hali hii. Mengi kama ndiye fisadi anapata wapi jeuri hiyo na kama ni Rostamu, hiyo jeuri yake inatoka wapi.
Whether it's Mengi au Rostam, the buck stops with the president, period.​
In this saga, there cant be any neutral ground.
 
Mimi naamini kwamba huo mchezo mkuu wa inchi ameipa mibaraka ndio maana unaona wamenyamaza.Na inaweza anakamkono bila hivyo ungeona ambacho kingetokea.Kuna mtu apendwi hapo.
 
Back
Top Bottom