![]()
Mwenye kuchukua hatua ni yule tuliyemkabidhi usukani kuendesha melikebu hii kwa usalama kwa muda wa miaka mitano. Ninachoshangaa anao washauri wazuri mno hata ambao wamepenya hadi kuwa katika chombo muhimu na kikubwa duniani kama Unaibu Katibu Mkuu umoja wa mataifa, lakini nini tatizo?
At least Mengi can dare
say this in public. Sio kunuka ni kuoza kabisa na ni kansa ya kukata
hii. Jivii na yuso havitaiponyesha. Mengi angekuwa anajua 'kukaa vizuri'
na hawa jamaa angemzidi bhakhresa!
Felix Mosha nae anataka serikali iwekeze kwenye kilimo cha kisasa, kwa
nini hakutumia fursa hiyo kwa zile hela za watanzania maskini
alizokusanya nicol? Nae ni wale wale tu!
Wewe kwanini ulingelea "wengine" na usingejisemea mwenyewe tu kama huwezi kuwajibia wengine? Khaaa unanchekesha!
Faiza unaweza kutoa rushwa kwa mtu/watu ambao hawana uwezo wowote wa kukunufaisha kwa namna moja au nyingine!? Mengi ananufaika vipi kwa kutoa rushwa kwa walemavu!?
umeona mkuu kabila01, wengine ndo hivyo wanahonga, zote hizo ni rushwa. Inshu inakuja watu wanapotumia mali isiyokuwa yao kujinufaisha au kudai kitu kidogo wakati mwisho wa mwezi analipwa that's means watu wanataka zaidi ya kile wakifanyiacho kazi.Wengine tunapiga ndogo ndogo kama buku 2 kwa traffic
![]()
Mwenye kuchukua hatua ni yule tuliyemkabidhi usukani kuendesha melikebu hii kwa usalama kwa muda wa miaka mitano. Ninachoshangaa anao washauri wazuri mno hata ambao wamepenya hadi kuwa katika chombo muhimu na kikubwa duniani kama Unaibu Katibu Mkuu umoja wa mataifa, lakini nini tatizo?
RUSHWA NI ADUI WA HAKI
MWENYEKITI wa kampuni za IPP, Reginald Mengi ametoboa siri kuwa hakuna mfanyabiashara wa Tanzania aliyefanikiwa katika biashara kubwa kwa kusaidiwa na serikali bila ya kutoa rushwa. Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), alisema yeye aligoma kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali jambo lililosababisha kupoteza fursa nyingi ambazo zingemfanya awe na maendeleo zaidi ya aliyonayo hivi sasa.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada katika uzinduzi wa ripoti ya uchumi na maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013, uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Diplomasia. Alisema kutokanana na kukithiri huko kwa rushwa, maendeleo ya kibiashara na kijamii hapa nchini hayawezi kufikiwa kama jitihada za kupambana na rushwa zitapuuzwa. Ili ufanikiwe ni lazima uione fursa iliyopo, lakini tatizo liko wapi mnajua ni kwa hawa waliopewa dhamana ya kutoa vibali kuendekeza rushwa, alisema Mengi. Alisema ni vigumu katika nchi iliyojaa rushwa kuzungumzia suala la amani wakati wananchi wanapata huduma mbovu kutokana na watendaji wa serikali, taasisi na idara zake kuendekeza rushwa.
Alibainisha kuwa idara nyingi za serikali hivi sasa zimegubikwa kwa rushwa kiasi cha kuathiri huduma mbalimbali zitolewazo huku akitolea mfano wa matumizi ya bajeti ya serikali ya sh trilioni 18 yaliyoidhinishwa na Bunge hivi karibuni. Tunaweza kuangalia dhamira nzuri ya serikali hasa katika bajeti ya trilioni 18, manunuzi ya umma ni asilimia 80. Kati ya hizo asilimia 20 -30 zinaweza kuishia katika mianya ya wizi na rushwa, na mambo haya yanaweza kufanywa na watu wachache huku wengi wakiangamia kwa kukosa huduma muhimu, alisema.
Alisema mbali na fedha zinazopotea katika manunuzi ya umma, maeneo mengine yanayofanya madudu kwa kiasi kikubwa ni sekta ya bandari, TANESCO na reli ambako alibainisha kuwa wajanja wachache wanatumia fursa walizonazo kujitengenezea mianya ya kufaidi rushwa ya maeneo hayo. Aliongeza kuwa mianya ya rushwa isipodhibitiwa Mtanzania wa kipato cha chini ataendelea kuumia hata kama kipato chake kitaongezeka.
Alisisitiza kuwa tatizo jingine linalochangia rushwa nchini ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokutambuliwa katika katiba pamoja na kunyimwa uwezo wa kuwashitaki watoaji na wapokeaji wakubwa wa rushwa. Alisema katika kupambana na rushwa nguvu ya TAKUKURU inaishia katika kuwashitaki watuhumiwa wadogo, huku wakubwa wakisubiri uamuzi wa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP). Mengi alisema ana wasiwasi kuwa kwa hali ilivyo sasa kwenye sekta ya madini nchini hakuna Mtanzania atakayebaki miaka michache ijayo iwapo mambo hayatabadilishwa.
Alibainisha kuwa sera na kauli zinazotolewa midomoni mwa viongozi zinaelekeza kumuwezesha Mtanzania katika fursa mbalimbali wakati uhalisia wa matendo yao hauendani. Viongozi wanasema mdomoni kuwa wanataka kuwawezesha Watanzania, lakini ukweli ni kwamba kuna mkakati wa kuwarudisha nyuma kwa kasi kubwa, alisema Mengi.
Awali, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Felix Mosha akiwasilisha ripoti ya uchumi na maendeleo 2013 kwa bara la Afrika alisema ukosefu wa miundombinu bora katika bara hilo unachangia kwa kiasi kikubwa wawekezaji kushindwa kuwekeza katika maeneo yatakayoweza kumkwamua mwananchi wa kawaida. Alisema nchi imefanya makosa makubwa kupuuzia kilimo cha kisasa na kukimbilia kuwekeza katika sekta nyingine huku ikiwaacha watu takribani asilimia 80 katika mbio za kuelekea katika mafanikio.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani na katika Afrika ni kati ya tano bora ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa, lakini wananchi wake wanaendelea kuwa katika hali duni. Hii ni kwa kuwa uwekezaji unafanywa katika maeneo yasiyowashirikisha wananchi moja kwa moja, alisema Mosha.

utacheka sana , kwani sioni kama unatumia kichwa chako ku-reason. wewe nani alikuambia wote wanaotoa msaada wanatoa kwasababu wanafuata maandiko matakatifu?
Long time!. Good to see you!. Welcome back FF, kumbe sometimes mwezi huu unaleta baraka hadi jf..........
Long time!. Good to see you!. Welcome back FF, kumbe sometimes mwezi huu unaleta baraka hadi jf.
Karibu tena kwa jina lako la zamani!.
P.
Wewe ule sio msaada, msaada hautolewi kwa kujitangaza? wewe lini ulikuja kujitangaza JF kuwa umetowa msaada. Upo hapo ulipo?
kwahiyo Janga la Kitaifa(JK) anavyofuturisha ikulu , ile nayo ni rushwa?
au Janga la Kitaifa (JK) anavyotoaga chakula na mavazi kwenye sikuku ya Iddy kwenye vikundi vya mayatima na kuoneshwa kwenye vyombo vya habari, ile nayo ni rushwa?
jaribu kutumia akili kidogo kuliko kuendeshwa na mihemko na kutumia sehemu ndogo ya ubongo wako kufanya maamuzi.
Huyo Janga la Kitaifa JK ni Julius Kambarage?
Unashindwa kuelewa ni kuwa Urais ni Taasisi na fedha zinazotumika Ikulu ni za Serikali na Serikali ina wajib wakuonesha inayoyafanya, ule ni wajib na si sadaka ile.
Jee, wewe ukitoa sadaka zako unakuja kutangaza JF?
Angalia mipaka yako safari hii utakula life ban JF umekuja na munkari sana
Huyo Janga la Kitaifa JK ni Julius Kambarage? Unashindwa kuelewa ni kuwa Urais ni Taasisi na fedha zinazotumika Ikulu ni za Serikali na Serikali ina wajib wakuonesha inayoyafanya, ule ni wajib na si sadaka ile.
Jee, wewe ukitoa sadaka zako unakuja kutangaza JF?
unamanisha nini? ameshakuomba rusha nawewe!Mengi mbona anjitekenya mwenywe na kucheka yeye mwenywe kwani yeye ameacha lini rushwa.