Mengi: Serikali inanuka rushwa

Mengi: Serikali inanuka rushwa

We manufacturing Teachers....by Kikwete
My door is always open...come to me and i will give good deal to invest Tanzania....by Kikwete

Ooohh Kikwete yupo Ikulu Kupiga madili halafu mnategemea atokokeze rushwa wakti yeye mwenye ni Mla rushwa namba mmoja. Ni aibu kumsikiliza huyu kiumbe ni pumba kwenda mbele

<font size="3"><span style="font-family:arial;">
 
Last edited by a moderator:
rushwa ni adui wa haki
mwenyekiti wa kampuni za ipp, reginald mengi ametoboa siri kuwa hakuna mfanyabiashara wa tanzania aliyefanikiwa katika biashara kubwa kwa kusaidiwa na serikali bila ya kutoa rushwa. Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari tanzania (moat), alisema yeye aligoma kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali jambo lililosababisha kupoteza fursa nyingi ambazo zingemfanya awe na maendeleo zaidi ya aliyonayo hivi sasa.


kauli hiyo aliitoa jana jijini dar es salaam wakati akichangia mada katika uzinduzi wa ripoti ya uchumi na maendeleo barani afrika kwa mwaka 2013, uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha diplomasia. Alisema kutokanana na kukithiri huko kwa rushwa, maendeleo ya kibiashara na kijamii hapa nchini hayawezi kufikiwa kama jitihada za kupambana na rushwa zitapuuzwa. "ili ufanikiwe ni lazima uione fursa iliyopo, lakini tatizo liko wapi mnajua&#8230; ni kwa hawa waliopewa dhamana ya kutoa vibali kuendekeza rushwa," alisema mengi. Alisema ni vigumu katika nchi iliyojaa rushwa kuzungumzia suala la amani wakati wananchi wanapata huduma mbovu kutokana na watendaji wa serikali, taasisi na idara zake kuendekeza rushwa.


alibainisha kuwa idara nyingi za serikali hivi sasa zimegubikwa kwa rushwa kiasi cha kuathiri huduma mbalimbali zitolewazo huku akitolea mfano wa matumizi ya bajeti ya serikali ya sh trilioni 18 yaliyoidhinishwa na bunge hivi karibuni. "tunaweza kuangalia dhamira nzuri ya serikali hasa katika bajeti ya trilioni 18, manunuzi ya umma ni asilimia 80. Kati ya hizo asilimia 20 -30 zinaweza kuishia katika mianya ya wizi na rushwa, na mambo haya yanaweza kufanywa na watu wachache huku wengi wakiangamia kwa kukosa huduma muhimu," alisema.


alisema mbali na fedha zinazopotea katika manunuzi ya umma, maeneo mengine yanayofanya madudu kwa kiasi kikubwa ni sekta ya bandari, tanesco na reli ambako alibainisha kuwa wajanja wachache wanatumia fursa walizonazo kujitengenezea mianya ya kufaidi rushwa ya maeneo hayo. Aliongeza kuwa mianya ya rushwa isipodhibitiwa mtanzania wa kipato cha chini ataendelea kuumia hata kama kipato chake kitaongezeka.


alisisitiza kuwa tatizo jingine linalochangia rushwa nchini ni taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) kutokutambuliwa katika katiba pamoja na kunyimwa uwezo wa kuwashitaki watoaji na wapokeaji wakubwa wa rushwa. Alisema katika kupambana na rushwa nguvu ya takukuru inaishia katika kuwashitaki watuhumiwa wadogo, huku wakubwa wakisubiri uamuzi wa mwendesha mashtaka wa serikali (dpp). Mengi alisema ana wasiwasi kuwa kwa hali ilivyo sasa kwenye sekta ya madini nchini hakuna mtanzania atakayebaki miaka michache ijayo iwapo mambo hayatabadilishwa.


alibainisha kuwa sera na kauli zinazotolewa midomoni mwa viongozi zinaelekeza kumuwezesha mtanzania katika fursa mbalimbali wakati uhalisia wa matendo yao hauendani. "viongozi wanasema mdomoni kuwa wanataka kuwawezesha watanzania, lakini ukweli ni kwamba kuna mkakati wa kuwarudisha nyuma kwa kasi kubwa," alisema mengi.


awali, mwenyekiti wa shirikisho la wenye viwanda (cti), felix mosha akiwasilisha ripoti ya uchumi na maendeleo 2013 kwa bara la afrika alisema ukosefu wa miundombinu bora katika bara hilo unachangia kwa kiasi kikubwa wawekezaji kushindwa kuwekeza katika maeneo yatakayoweza kumkwamua mwananchi wa kawaida. Alisema nchi imefanya makosa makubwa kupuuzia kilimo cha kisasa na kukimbilia kuwekeza katika sekta nyingine huku ikiwaacha watu takribani asilimia 80 katika mbio za kuelekea katika mafanikio.


"tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani na katika afrika ni kati ya tano bora ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa, lakini wananchi wake wanaendelea kuwa katika hali duni. Hii ni kwa kuwa uwekezaji unafanywa katika maeneo yasiyowashirikisha wananchi moja kwa moja," alisema mosha.

hata baba wa taifa alisema maneno haya.swala ni tufanye nini.?ufumbuzi ni kuachana na magamba.IT IS SIMPLE AD CLEAR.waliasisi rushwa,wanaiishi.hawawezi kuondoa rushwa!!!!sasa wewe ni gamba halafu unasema nchi inanuka rushwa.it may be a joke of the week.naiko?kwa akili hizi kweli tutafika???
 
Mengi anawalipa kiasi gani waajiriwa wake na hasa waandishi wa vyombo vyake vya habari? Tusiangalie serikalini tu bali kote na kwenye taasisi binafsi zinasaidiaje kuzuia rushwa.
 
at least mengi can dare say this in public. Sio kunuka ni kuoza kabisa na ni kansa ya kukata hii. Jivii na yuso havitaiponyesha. Mengi angekuwa anajua 'kukaa vizuri' na hawa jamaa angemzidi bhakhresa!


Felix mosha nae anataka serikali iwekeze kwenye kilimo cha kisasa, kwa nini hakutumia fursa hiyo kwa zile hela za watanzania maskini alizokusanya nicol? Nae ni wale wale tu!

mengi nae anatuhumiwa kwenye naicol wewe.waliwekeza pesa za nicol kwenye kiwanda kilichokuwa kinafilisiwa.kiwanda chenyewe ni cha ndugu yake mengi.once a gamba always a gamba.ni ukoo wa panya.
 
Hakuna MCHAGA ambae hakwepi kodi,
Hapa asitake kupata huruma ili agombee urais nafasi ya Mgombea binafsi.
Huyu Mengi alikuwa akimfadhili Mchungaji Mtikila ashughulikie suala hilo, na ndio chanzo cha kuanzisha IPP MEDIA.

Kama kweli Huyu Mengi ni msafi aonyeshe mapato yake na kodi anazolipa hapo TRA kama hajaabika kabla hajafika Kibosho, kama sasa ameanza kuchakachua Maji ya Kilimanjaro na kuuza maji fake,Kama Mengi ni Msafi mwaka 2008 alifanya nini kwenye Hisa za NICOL na ndugu yake wa karibu.
MENGI na Rushwa ni sawa na Pete na Kidole.
Hana jipya,Watanzania Haya mambo tunayajua kuliko wanavyodhani.
 
Mfanyakazi wa chini kabisa Ipp analipwa laki 4.. Hakuna sekta binafsi hapa Tanzania inayomfikia mengi kwa kujali wafanyakazi...
Mengi anawalipa kiasi gani waajiriwa wake na hasa waandishi wa vyombo vyake vya habari? Tusiangalie serikalini tu bali kote na kwenye taasisi binafsi zinasaidiaje kuzuia rushwa.
 
Well spoken Reggie Mengi; japo kwa kuwa facts are stubborn, na wasema kweli mara nyingi huchukiwa sana na penginepo huwindwa na kuuwawa; utachukiwa sana kwa hili uililolisema; I wish Jakaya Kikwete had the courage to say the same in the same terms.
 
Mengi mbona anjitekenya mwenywe na kucheka yeye mwenywe kwani yeye ameacha lini rushwa.
 
hakuna mchaga ambae hakwepi kodi,
hapa asitake kupata huruma ili agombee urais nafasi ya mgombea binafsi.
Huyu mengi alikuwa akimfadhili mchungaji mtikila ashughulikie suala hilo, na ndio chanzo cha kuanzisha ipp media.

Kama kweli huyu mengi ni msafi aonyeshe mapato yake na kodi anazolipa hapo tra kama hajaabika kabla hajafika kibosho, kama sasa ameanza kuchakachua maji ya kilimanjaro na kuuza maji fake,kama mengi ni msafi mwaka 2008 alifanya nini kwenye hisa za nicol na ndugu yake wa karibu.
Mengi na rushwa ni sawa na pete na kidole.
Hana jipya,watanzania haya mambo tunayajua kuliko wanavyodhani.

hahahahahahaha lengo lako ni nini?!!! Tunachojadili ni credibilty ya mengi kuwa nae ni mlaa rushwa au serikali imeoza kwa rushwaa..!!!!!??????? Mnayumbisha topic makusudi ili ku-suit interest zenu.... Inawezekana kweli hayo unayosema ni kweli ila si sababu ya kutufanya kuacha kujadili kile alichokisema. Kama wewe kweli ni mzalendo utakubaliana nae kuwa serikali ya tanzania imeoza kwa rushwa.. Ukienda polisi hakuna haki bila kuingia mfukoni, ukienda hospitali watakuambia x-ray na ct scan mbovuu ila ukiingia mfukoni itafanya kazii, shuleni mtoto hawezi kufaulu bila tuition, tra ukifuta tartibu za kawaida utachukua mwezi na watakukamua mpka ukome ila ukiingia mfukoni masaa tuu mambo yako yamenyooka. Haya ndio tunayoyajadili na wala siii uzuri auu ubaya wa msemaji.. Hata saaa mbovu huwa inasema ukweli, rushwa ni adui wa haki na wajibu wa mtanzania yeyote mzalendo na mpenda haki kuipiga vitaa...
 
Mengi mwenyewe tunajuwaje siri yake? mimi huona akitowa rushwa kwa walemavu diamond jubilee. Au ni nini kile?

hapo umepotoka, kuwasaidia walemavu ni kutoa rushwa?????/ ameanza kusaidia jamii long tym ago back in 90's, nahisi ulikuwa haujaja mjini
 
hapo umepotoka, kuwasaidia walemavu ni kutoa rushwa?????/ ameanza kusaidia jamii long tym ago back in 90's, nahisi ulikuwa haujaja mjini

"Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo. Basi, unapotoa sadaka, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata malipo yao. Lakini wewe unapotoa sadaka, mkono wako wa kushoto usijue mkono wa kulia umefanya nini. Toa sadaka yako kwa siri. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atawapa thawabu. "(Mathayo 6:1-4 Biblia)
 
j8.jpg


mwenye kuchukua hatua ni yule tuliyemkabidhi usukani kuendesha melikebu hii kwa usalama kwa muda wa miaka mitano. Ninachoshangaa anao washauri wazuri mno hata ambao wamepenya hadi kuwa katika chombo muhimu na kikubwa duniani kama unaibu katibu mkuu umoja wa mataifa, lakini nini tatizo?

asikudanganye mtu.once a gamba always a gamba.
 
Binafsi ninaamini rushwa itaendelea kuitafuna Tanzania hadi pale Katiba itakapoainisha wazi meno yake juu ya wala rushwa!! Viongozi wanapatikana kwa kutoa rushwa tena hadharani, weziwanaombwa kurudisha mali walizoiba! Kiama cha rushwa ni kutoichagua CCM!! Lowasa ananuka rushwa na hata bunge lilithibitisha kupitia kamati zake! Na amekua anagawa pesa wazi wazi na watu wanamshabikia awe rais ajae!! Kama ni hivo tuendelee kua taifa la wala rushwa na wauza madawa ya kulevya!
 
Back
Top Bottom