Bikirajohola
JF-Expert Member
- Jun 11, 2022
- 356
- 632
Meneja wa TRA mkoa wa Kigoma bwana Gabriel Mwangosi amesimamishwa kazi na kamishina mkuu wa TRA bwana Alphayo Kidata baada ya kupandisha ushuru wa forodha mkoani humo kutoka millioni 15 kwa mwezi hadi millioni 300 kwa mwezi!
Alichokifanya bwana Mwangosi alipofika Kigoma ni kuziba mianya yote ya upigaji na kuwaelekeza wafanyabiashara wote kulipa mapato halali TRA na kupata risit halali matokeo yake mapato yakapanda maradufu kitendo ambacho kiliwakera wakubwa ikiwemo wafanyabiashara wakubwa na kuamua kumzushia zengwe na hatimaye amesimamishwa kazi na mapato ya forodha mkoani humo yameshuka tena na kuwa vilevile millioni 15 kwa mwezi!.
Ni kama tu Sabaya alivyoikuta wilaya ya Hai ikiwa ya 144 kwenye mapato na kuipandisha mpaka ikawa ya nne kitaifa lakini akaishia kuzushiwa zengwe na kupelekwa mahakamani. Jambo hilo la wazalendo kutafutwa kwa tochi na kuzushiwa mazengwe limemkera mbunge Tabasamu na kukataa kuomba radhi kwenye mwongozo wa waziri Simbachawene.