Meneja TANESCO Mkoa wa Arusha umempuuza Makonda kuhusu mgawo wa umeme?

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,156
Alipokuja katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wananchi wa Arusha walilalamika kuwa mgawo wa umeme unaoendelea siyo fair. Unakuta kuna eneo linakatwa umeme kila siku kuanzia asubuhi mpaka jioni, kuna eneo lenyewe lina umeme kila siku mchana wanakatiwa jioni, hawa kila siku jioni wanakuwa gizani, kwa maana nyingine watoto wao hawawezi kufanya homework wala kutumia runinga zao.

Haya yanafanyika hasa maeneo ya pembezoni au nje ya miji. Kwa mfano maeneo ya Kikatiti wilaya ya Arumeru ni wiki 2 sasa kila ikifika saa 1 jioni umeme unakatwa na kurudishwa usiku wa manane wakati mmeshalala. Kwanini hivi ndugu meneja wa Mkoa?

Tumeshalalamikia ofisi ya wilaya Arumeru iliyoko Usa-River, yule meneja wa pale ana dharau sana anawapuuza wananchi. Km imempuuza mwenezi wa chama kilichounda serikali utamsikiliza na kumtii nani. Km vp mwondoeni huyu jamaa pale Arumeru.
 
Alipokuja katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wananchi wa Arusha walilalamika kuwa mgawo wa umeme unaoendelea siyo fair. Unakuta kuna eneo linakatwa umeme kila siku kuanzia asubuhi mpaka jioni, kuna eneo lenyewe lina umeme kila siku mchana wanakatiwa jioni, hawa kila siku jioni wanakuwa gizani, kwa maana nyingine watoto wao hawawezi kufanya homework wala kutumia runinga zao. Haya yanafanyika hasa maeneo ya pembezoni au nje ya miji. Kwa mfano maeneo ya Kikatiti wilaya ya Arumeru ni wiki 2 sasa kila ikifika saa 1 jioni umeme unakatwa na kurudishwa usiku wa manane wakati mmeshalala. Kwanini hivi ndugu meneja wa Mkoa? Tumeshalalamikia ofisi ya wilaya Arumeru iliyoko Usa-River, yule meneja wa pale ana dharau sana anawapuuza wananchi. Km imempuuza mwenezi wa chama kilichounda serikali utamsikiliza na kumtii nani. Km vp mwondoeni huyu jamaa pale Arumeru.
Mlitaraji nini ndugu?
 
Back
Top Bottom