Uchaguzi 2020 Membe, soma alama za nyakati

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,170
23,865
Siasa ni mchezo mmoja wa ajabu. Siasa haitaki hasira wala kuilazimisha. Taabu anayopata Mh Magufuli kujinadi sasa hivi haikutegemewa, pamoja na mazuri mengi aliyofanya.

Ndugu yetu Membe kaingia siasa kwa mdundiko wa wengi.
Wapiga mdundiko walipotuliza ngoma sasa ndo tunaona mambo dhahiri.

Membe soma alama za nyakati, na nyakati zimebadilika sana kuliko ilivyokuwa miezi miwili tu iliyopita. Kwa sasa kisiasa hatuwezi kusema Membe ni prime mover, hana mtaji huo.

Membe soma alama za nyakati.

UPDATE
Membe kwa kweli amesoma mambo vilivyo, kimya kinaongea
 
Membe anaoption mbili tu kurudi ccm au kumuunga mkono lissu.wagombea urais ni jiwe na lissu.hao wengine washehereshaji tu.
Kweli mkuu.
Mtaji wa kisiasa aliofikiri anao mzee Membe umetetereka sana.
He is not a firebrand that we thought he was.
Au aliji overate mno.
 
Katika siku za karibuni, sintofahamu ya baina ya vyama vya siasa iko dhahiri.
Na kumya kikubwa cha Membe kinaashiri kukubaliana na alama za nyakati.
 
Membe ana akili zake, ACT na CHADEMA waliwapiga chenga CCM wakidhani hawataungana. Ndio maana hajafanya kampeni hata moja ya URAIS mara anasafiri mara anasema ukata. Ni mkakati, walishaamua kumuunga mkono Lissu.

Ndio maana msaidizi wake walimkamata, hawaamini nyendo zake

Sio Membe tu wako wengi ndani ya Chama na Serikali ambao wanamuunga mkono Lissu
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom