Membe: Msije Dar wakati wa ziara ya Obama

Membe: Msije Dar wakati wa ziara ya Obama

Tanzania haina tofauti na Ghetto la masela... Sasa mpaka majani wameapaka rangi a Kijani si balaa hili??
 
Waziri wa mambo ya nje bwana Benard Membe anapothubutu kusema eti kuimarisha ulinzi katika ujio wa Obama anawashauri waTz walioko mikoani wasiende Dar kwa kweli ametusikitisha sana, Membe mbona unavunja taratibu za misingi ya kiusalama, kwani ujio wa Obama ndio uzuie shughuli za kiuchumi za nchi, Membe unajuwa misingi namna ya kujipanga katika ulinzi leo unaivunja , nakumbuka wewe ulihudumu katika idara ya usalama wa taifa [TISS] enzi hizo ukiwa na akina marehemu Benald Walingozi,Peter Kuhanwa,Ally Nissi,Mwasokwa. n.k leo papara zako zinakupelekea siko.
 
Pia tunaomba akishaondoka na nyie viongozi msije huku mikoani kwani tutakuwa bize na kazi zetu nadhani mnanipata.
 
Kweli mgeni njoo mwenyeji apone. Nilichofurahia tu ni ukarabati wa barabara ya Mwai Kibaki maana ilikuwa inatisha kwa ubovu na kusababisha foleni isiyo ya lazima. Mvua zikinyesha magari yalikuwa yanazama kwenye madimbwi kama mitumbwi!

Huo ukarabati ni wa muda tu. mgeni akiondoka tunarejea maisha yetu ya kawaida. Hii yote ni kuonyesha jinsi Vasco anavyompapatikia Obama.
 
Membe asituzingue kwani ziara ya obama mm kabwela inanihusu nn
 
1. wangetangaza hizo siku ambazo jaluo atakuwa bongo ni public holiday ili kupunguza mizunguko ya watu mjini hasa wafanyakazi ambao ni wengi.
2. tatizo kubwa linakuja kwasabau hatuna miundombinu mbadala, hatuna treni za kasi jijini ili kupunguza usumbufu wa movements za watu, barabara chache sana ndo mana hadi wanafikia kukurupuka kusema wa mikoani wasije dar. kungekuwa na barabara nyingine wala kusingekuwa na tatizo
3 hivi wanjua athari zitakazowapata wamiliki wa mabasi ya mikoani ambao kwa ujumla ni hasara kubwa sana?

mlioajiriwa hapo dar subirini talaka kwa wake zenu au kufukuzwa na waajiri wenu.
 
hivi kikwete akienda kwa obama kunakuwa na hali hii?
 
Hivi huyu nyoka wa mdimu anamtisha nani? mamamake Chinga! Jijini lazima tutie timu nyambaf!! Kama ni hivyo tupeni off ya wiki nzima basi mpaka Jaluo nyeupe iondoke!
 
mwa J kwani we hutaki kwenda marekani
Marekani ninakwenda na kurudi bongo kwangu. Kwani presidaaa wetu akienda marekani wamarekani huwa wanahaha kama tunavyohaha sie sasa hivi?
 
Huo ukarabati ni wa muda tu. mgeni akiondoka tunarejea maisha yetu ya kawaida. Hii yote ni kuonyesha jinsi Vasco anavyompapatikia Obama.

Kumbe pesa za kuweka mazingira safi na kukarabati barabara huwa zipo ila zinasubiri MGENI MAALUMU.
 
Haya sasa j3 watu wote watakua maofisini 5am sharp. Maana air force1 ikifika anga la zambia tu huku road zishafungwa.

Hahaaa mkuu unanichekesha. Air force ikitokea SA inapita juu ya anga la Msumbuji usawa wa bahari kuna monowari zipo bahari ya Hindi zinafuatilia nyendo zake
 
Back
Top Bottom