Membe: Msije Dar wakati wa ziara ya Obama

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,673
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi waMikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wawageni.

"Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida," alisema.

Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.

"Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao," alisema na kuongeza: "Kama kuna watu ambaohawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao."

Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwani pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.

Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.

Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.

Rais Obama atakwenda katika kituohicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.

Wengine watakaoathirika ni wakazi wa Kimara, Mbezi, Kibamba hadi Kiluvya. Athari nyingine ya usafiri itakuwa katikati ya jiji ambako Obama na msafara watakuwa na shughuli nyingi na hasa ile ya ufunguzi wa barabara karibu na Ikulu na kukutana na wafanyabiashara kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Jumatatu ijayo.

Watumiaji wengine wa barabara watakaopata shida ni wale wa Barabara ya Bagamoyo hasa pale Rais Obama na mkewe watakapokwenda kuweka mashada ya maua kwenye ubalozi wa zamani wa Marekani uliopuliwa na mabomu mwaka 1998.

Ulinzi hoteli za kitalii
Mashushushu wa ndani na nje ya nchi wamezingira kwenye hoteli kubwa za Dar es Salaam na walionekana katika baadhi ya hoteli hizo, wakiwatumia mbwa maalumu kufanya ukaguzi wa chumba hadi chumba.

Tofauti na utaratibu uliozoeleka, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano zimeanza kutumia mitambo maalumu ya kompyuta kuwafanyia ukaguzi wageni wote wanaoingia.

Wamchongea JK
Mtandao wa Kutetea Waandishi wa Habari Duniani (CPJ), umemwandikia barua Rais Obama ukimtaka kujadiliana kwa kina na mwenyeji wake Rais Kikwete wakati wa ziara yake nchini kuhusiana na vitendo vya kuuawa na kuteswa kwa waandishi wa habari wa Tanzania.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa CPJ, Joel Simon na nakala yake kusambazwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete mwenyewe, mtandao huo ulitolea mfano wa kuuawa kwa Mwandishi wa Channel 10, Daudi Mwangozi na Issa Ngumba wa RedioKwizera. Pia kupigwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda.

Marais waja Smart Partnership

Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho, Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza uchumi.

Viongozi watakaohudhuria mkutanohuo ni Waziri Mkuu wa Malayasia, Najib Razak, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Uhuru Kenyetta (Kenya), Boni Yayi (Benin), Ali Omar Bongo (Gabon), Ikililou Dhoinine (Comoro), Faure Gnassingbe (Togo), Ernest Koroma (Sierra Leone), Blaise Compaore (Burkina Fasso), Mahinda Rajapaska (Sri Lanka) na Mfalme waSwaziland, Mswati II, ambaye aliwasili jana.

Chanzo: MCL
 
Haya sasa j3 watu wote watakua maofisini 5am sharp. Maana air force1 ikifika anga la zambia tu huku road zishafungwa.
 
nafikiria jumatatu sisi tunaokaa maeneo y gongolamboto, pugu na kisarawe kutoka na kuingia mjini, kwa wiki hii foleni balaa jioni! muda gani anaingia na kuondoka?
 
Kwa mnaofahamu,Rais wa Marekani anapozuru nchi kama CHINA NA urusi nao wanafanyiwa hivi kweli???ndege za kivita za Marekani zinaruka na kuizunguka miji ya nchi hizo alipofikia Rais wa Marekani kama zitakavyofanya hapa kwetu?maana kama ni kuogopa maadui hata huko wapo.
 
article-2348975-1A84A465000005DC-503_634x517.jpg

nimekaa najiuliza hivi Ziara ya Obama ni raha au kwa raha kwa watanzania

na je tunasubiri hadi ziara kama hizi ndio tufanye marekebisho ya jiji!!!

angalia pele Salenda bridge kulivyo karabatiwa na kupakwa rangi
barabara ya Morocco kwenda posta kumewekewa bendera za Tanzania
pale ubalozi wa Marekani bustani kupaliliwa na nyumba za opposite za Tanesco zilivyopakwa rangi

Huku waziri membe akitoa angalizo kwa watanzania kutosafiri wabaki walipo
hadi shughuli iishe kwani Hoteli,Taksi zoote zimekodiwa

Ufunguzi wa sabasaba kusogezwa mbele hadi Ziara itakapokamilika........
na mengine mengi yanayoendelea kwa sasa

:welcome: to Tanzania
 
Kwa mnaofahamu,Rais wa Marekani anapozuru nchi kama CHINA NA urusi nao wanafanyiwa hivi kweli???ndege za kivita za Marekani zinaruka na kuizunguka miji ya nchi hizo alipofikia Rais wa Marekani kama zitakavyofanya hapa kwetu?maana kama ni kuogopa maadui hata huko wapo.

Eti hebu watuambie wanaojua
 
Ni hali ya kawaida kwa watanzania kuanzia level ya familia kufanya usafi wa hali ya juu kunapokuwepo ugeni wenye uzito Fulani. Kwa hili sishangai
 
angalia pele Salenda bridge kulivyo karabatiwa na kupakwa rangi
barabara ya Morocco kwenda posta kumewekewa bendera za Tanzania
pale ubalozi wa Marekani bustani kupaliliwa na nyumba za opposite za Tanesco zilivyopakwa rangi

Huku waziri membe akitoa angalizo kwa watanzania kutosafiri wabaki walipo
hadi shughuli iishe kwani Hoteli,Taksi zoote zimekodiwa

Ufunguzi wa sabasaba kusogezwa mbele hadi Ziara itakapokamilika........
na mengine mengi yanayoendelea kwa sasa

:welcome: to Tanzania[/QUOTE]

Mimi kwangu nimependezeshwa na hilo la taksi na Hoteli kujaa, kwani Wananchi watafaidika, Mahotelini wataneemeka kuanzia tipp mpaka Madada poa, wenye taksi nao vivyo hivyo, ila mimi ningeenda mbali kidogo kuwataka Serikali watoze kodi hizo huduma zote ili fedha izunguke na sio kuishia kwa mwenye Taksi na Wenye hoteli tu!
 
Hivi alipokuja bush mbona haikuwa kero hivyo! Imekuaje mjaluo anakuja na usumbufu kwa wenyeji unakuwa mkubwa hvyo. Lakn ajiangalie tz kuna vitu vizito vyenye ncha kali virukavyo!
 
watu8..
anasema kwetu tanzania ni Mgeni njoo Mwenyeji........
Kweli mgeni njoo mwenyeji apone. Nilichofurahia tu ni ukarabati wa barabara ya Mwai Kibaki maana ilikuwa inatisha kwa ubovu na kusababisha foleni isiyo ya lazima. Mvua zikinyesha magari yalikuwa yanazama kwenye madimbwi kama mitumbwi!
 
Hivi nani aliyewaambia watawala wetu kuwa sisi vitu vizuri hatuvipendi? Manake naona anaandaliwa mgeni apite palipo bora na sio sie........kumbe hela mnazo eeh?! Sie tukiomba tunaambiwa hamna fungu, hizi mmetoa fungu lipi?
 
Tatizo liko kwenye hii serikali yetu hewa inayoongozwa na viongozi hewa wasiojua majukumu yao mpaka waje wageni ndo waanze kuchakarika ili tu kuficha aibu yao.

Ndo maana unaambiwa "Kama nchi itaongozwa na viongozi hewa, hupelekea nchi yote ionekane imejaa watu hewa" kwa maana serekali inaongozwa na wajinga kadhaa hii inatufanya sisi sote tuonekane wajinga.

Haya marekebisho tunayaona sana tunapopata ugeni kutoka nje.
Mfano:Ukirudia ugeni wa George Bush, nao ilikua vivyo hivyo.
 
Kwa kwel ata me ningependa kujua hzo hela za mandalizi yoye hayo zimepatikana wap...basi kama hvo natoa ombi wageni wazito kama huyo obama wawe wanafanya ziara tz atlist 3 times per year ili tz irekebishwe ing'are..on the other side hii ni karaga as shughuli zimekwamishwa n nahisi huu ujio utatulaza njaa sis mafundi viatu, machinga, wauza vitumbua na wafanya biashara wote wado wa posta na maeneo mengine ya jijn..hii naona haijaka mkao
 
Back
Top Bottom