Chechetuka,
..dont invest too much on Tanzanian politicians. you will be disappointed my friend.
..sasa kama unaweza hebu fanyia kazi madai na tuhuma nzito alizoshusha mchangiaji kanda2.
NB:
..mimi nimeuliza tu, kulikoni Lindi wabunge karibu wote ni watu wa usalama?
..sasa fanyia kazi madai hayo nayo halafu tuletee tathmini yako.
..tueleze yupi ni usalama yupi siyo.
MgonjwaUkimwi said:Kwa taarifa Membe alishaondoka usalama wa taifa kabla hajawa Mbunge mwaka 2000. Kifo cha utatanishi cha aliyekuwa director general wa usalama, Kombe mwaka 1997, kitendo cha Mkapa cha kumtaka Membe aombe radhi usalama wa taifa kwa madai kwamba alivujisha Ufisadi wa Kitine akishirikiana na Mkapa kwa gazeti la jenerali ulimwengu, na ambitions za Membe kuwa mbunge katika jimbo lake ndivyo vilivyomfanya Membe ajiondoe usalama wa Taifa.
Hivyo basi, swali lako kwamba nani sio usalama wa Taifa, Membe alipoanza ubunge hakuwa usalama wa taifa. Na sasa si mtu wa usalama wa taifa.
Jibu ndiyo hao watatu tuliowataja humu ni usalama wa Taifa na MEMBE bado anajifanya Usalama.kanda2,NasDaz,
..mbunge wa Lindi Mjini ni Mheshimiwa Mohamed Abdulaziz.
..je, ni kweli kwamba wabunge wote wa Lindi ni watu wa Usalama?
MwanaFalsafa1 said:uraisi kuna minimum requirements zake kikatiba ambazo kwa ufupi ni kuwa raia, kuwa na umri juu ya miaka 35 nk. Kama mtu katimiza vigezo vyote hivyo na aka gombea uraisi hamna tatizo. Ni juu ya wapiga kura wenyewe kuangalia vigezo vya ziada na kuangalia kama anafaa au la. Membe akigombea uraisi mme lazimishwa kumchagua?
Hivi kuna tatizo gani Membe akigombea uraisi? Mtu kugombea
MwanaFalsafa1,
..hakuna mtu aliyeleta madai kwamba Membe hana sifa za msingi[uraia, umri,...] kuweza kugombea nafasi ya Uraisi.
..nadhani wachangiaji hapa, ambao naamini wana sifa za msingi kabisa kuwa wapiga kura ktk uchaguzi wa Raisi, wanajaribu kuangalia, kama ulivyoelekeza, kama Membe ana sifa za ziada kugombea nafasi hiyo.
..binafsi najiuliza will he stands as a CCM candidate will he be an upgrade or downgrade from who we have right now?
..zaidi ya kumlinganisha na wagombea wa vyama vingine, najaribu kumpima na wagombea wa majirani zetu na mataifa mengine ya Kiafrika.
..kwa mfano: Rwanda the next person in line inasemekana ni Dr.Donald Kaberuka, sasa huyu unamlinganisha vipi na Membe. je, ataweza kutuwakilisha na kungara anaposhindanishwa mbele ya macho ya Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya watu kama Kaberuka?
..hebu, tuangalie Ghana ambao ndiyo mfano wa demokrasia na uongozi ktk Afrika. je, Membe ataweza kuwekwa kundi moja na mwanazuoni kama Prof.Atta Mills?
..halafu turudi tena kuhusu masuala ya ndani. Membe amefanya kazi gani na ana mafanikio gani kutuhakikishia kwamba anaweza kutoa mwongozo na kuwa "kilongola" ktk harakati za kuinua uchumi wa nchi yetu? does he have the necessary skills, background, and exposure?
..tuingie ndani ya CCM. katika masuala ya utendaji, bongo inayochemka,vision for the future of the country, maadili ya kazi etc hivi Membe anawazidi wana CCM wenzake wanaotajwa tajwa kama Dr.Shein, Prof.Eng.Mwandosya, Pombe John Magufuli, au Mizengo Pinda?
Mkuu hoja zako zote nazikubali. Nilicho kuwa nasemea mimi ni sawa tu na wewe ulicho kisema mwanzo. Kwamba kugombea uraisi kuna minimum requirements. Sasa sisi wapiga kura ndiyo kazi yetu kuangalia kama mtu ana hizo za ziada au la. Kama mtu anafaa tunampa kama hafai hatumpi. So Membe kugombea uraisi is a non issue. Wengi wa wananchi hawana access ya process ya kuchagua wagombea wa chama fulani. Sisi tunapewa haya huyu wa CCM na huyo wa chama fulani. Inakua kazi yetu kuchagua nani anayefaa kati yao.
Kwangu mimi Membe hajafanya chochote kinacho onyesha kuwa yeye ni bora au la kuliko JK. Honestly lakini I can't imagine any one doing any worse then JK. Maana JK kwa bahati mbaya alichaguliwa zaidi kutokana na charisma kuliko leadership skills zake. Na pia he had too many political debts to pay ndiyo maana baraza lake la kwanza akajaza watu ambao hawafai.
Membe is in a good position kutu wakilisha vizuri kimataifa kutokana na kuwa waziri wa mambo ya nje. Sisemi ataweza ila nasemaa tu kwa nafasi hiyo ingetosha kwake kupata experience ya kuweza kutu wakilisha nje au la. Whether he can or will bado naona ni debatable but he is in a good position to gain those skills kama kweli yupo serious about doing so.
Mkuu mimi naona wanasiasa wengi wa CCM ni very partisan na politics as usual. Kumuweka adui au mtu wa itikadi tofauti kwa maendeleo ya chama kwao inakua vigumu.
In my honest opinion katika hao uliyo wataja naona John Magufuli ndiye anayefaa. Tatizo litakua kama Magufuli mwenyewe ana interest ya kugombea au la. Salim is a good diplomat. Lakini kwa hali yetu ya sasa sidhani kama tuna hitaji rahisi ambae skills zake kubwa ni kimataifa. Tuna hitaji raisi ambaye ata concentrate zaidi nyumbani. Mambo ya diplomasia na foreign service mtu huyo awekwa wizara ya mambo ya nje. Sasa swala pia linakuja kama Membe nae kutokana na nafasi yake ya kuwa waziri wa mambo ya nje ata concentrate kwenye medani ya kimataifa kama Kikwete au atakua home based zaidi. Kupata feel ya Membe zaidi ingebidi term ijayo awekwe kwenye wizara nyingine then mwisho tuangalie wapi ali excel zaidi. Dr. Shein nae he is formidable. Kwa ninavyo muona atakua raisi ambae ata concentrate nyumbani badala ya kutalii talii kama Kikwete. Pia anaonekana ni mtu wa vitendo zaidi ya maneno. Hao wengine wote waliotajwa sioni uwezo wao wa kuongoza kusema ukweli.
Tatizo nchi yetu ni ukosema wa data nzuri ya kupima potential leaders. Ndiyo maana tunaishia kufanya guess work na matokeo yake ndiyo tunapata maraisi kama Mkapa na JK ambao initially watu waliwaona wanafaa kweli lakini ndiyo hivyo. It's hard kujua mtu atakua raisi wa namna gani mpaka atakapo shika nafasi hiyo. Let us hope the next generation of potential presidents wata offer a more diverse pool of candidates. Lakini kwa ninavyo ona Tanzania sasa we are just choosing the best among the worst and not the best of the best.
Mkuu wangu unamsifia nyoka mwingine - Swila, kwa rangi za ngozi yake na uwezo wa kulala ubavuni mwako usiku kucha asikudhuru lakini sumu ya Swila ni kali kuliko hiyo ya nyoka wa mdimuni..Tuulize sisi wa bara tunayemjua Swila..."Membe ni Nyoka anayekaa kwenye mdimu wakati hali majani wala matunda ya mti huo"
Ni kauli tata na nzuri sana hasa ukijua ndugu Mudhihiri alichokuwa hasa akilenga, real this man is very intellegent,Maudhui ya ujumbe yalikuwa akionyesha ni kwa jinsi gani huyu bwana Membe alivyo na roho mbaya, mbinafisi na anayependa maendeleo ya jimbo lake tu, yuko tayari kufanya chochote ili mradi tu maendeleo yote yaelekezwe jimboni kwake kama siyo kijijini kwake, sasa kama malighafi inapatikana jimboni kwa mudhihiri, ni kwa nini anang'ang'ania kiwanda kijengwe jimbono kwake??
Hii ni tabia chafu sana na ndoimetufikisha mpaka hapa tulipo, barabara zote nzuri ziko eneo moja hapa nchini kisa kuna mkuu anatokea huko, angalia hata umeme utagundua hao Nyoka wanaoishi kwenye Mdimu ambao Membe anawawakilisha ni wengi sana hapa Tanzania, je tuko tayari kuongozwa na hao nyoka 2015??
Kwa hili ndugu Mudhihiri utapata maadui wengi sana lakini ukweli utabakia pale pale, angalia bajeti ya wizara ya miundo mbinu ilivyokuwa,je hii tabia si ya hao nyoka??
MgonjwaUkimwi,
..kwani Mkapa alihusika vipi na udanganyifu ktk matumizi ya fedha za serikali uliofanywa na mke wa Col.Kitine?
..ninavyokumbuka Lt.Gen.Imran Kombe alifariki akiwa tayari ameshaondolewa Usalama wa Taifa na nafasi yake kuchukuliwa na Apson.
..je, unafahamu sababu zilizosababisha Kombe kuondolewa usalama? je, unaweza kusema kimaadili Lt.Gen.Kombe alikuwa mtu wa aina gani? rekodi yake kama Dir if Inteligence ilikuwaje?
Haya ndio maneno mkuu wangu.. nakukubali..Nikirudi kwenye maswali yako, sitapenda nitoe data zaidi ya nilizotoa. Kwani kufanya hivyo ni kutowafanyia haki wahusika na ni mwanzo wa kutoka nje ya mada husika. Na ieleweke kwamba mchango wangu juu ya hili ni kukanusha madai ya Mudhihir juu ya Membe na madai kwamba Mwikalo ndie aliyefanya Membe awe waziri. Vile vile nikatika kujibu hoja yako juu ya wabunge kuwa watu wa usalama wa taifa. Na hapa nitarudia tena kwamba TANGU 2000 MEMBE SI MTU WA USALAMA.
Nitaendelea kuimba kwamba MWIKALO SIO MFADHILI WA KAMPENI ZA MEMBE. Yeye mwenyewe (Mwikalo) kama mfuasi HALISI wa dini ya uislamu anajuwa kwamba uwaziri wa MEMBE SIO MATUNDA YAKE, bali ni matunda ya urafiki wa Membe na JK ulioanza miaka ya mwisho ya 70, na kuimarika 1995 Chimwaga wakati Membe alipoikacha kambi ya Mkapa (jirani yake kimkoa) na kujiunga na kambi ya Kikwete. Yeyote anayesema kwamba Mwikalo ndio mfadhili wa Membe hamjui Mwikalo, wala hajui urafiki wa Membe na JK.
Typical GT.
Start an allegation without explanation and leave it to the wolves.
But give us something to bite on. For example you mention national interests and national security and leave it hanging.surely Home of GREAT THINKERS na INSIDERS watatengua tuuu usitie taabu
saa zingine bora kuadopt style ya Mwanakijiji
sijawahi kukutana na waziri mpenda sifa na muongo kama MEMBE kwenye maneno matano chukua moja. watu wa karibu na huyu bwana mwambieni aache kudanganya watu,uongo wake nadhani ni wa kuzaliwa au kurithi.
Nimeona nami nije na style ya Mwanakijiji ya kuwapa Vitendawili mvitengue.
Wakati masakata ya akina Sitta na wenzie yanawaweka watu bize..huyu bwana has been busy na mambo mengi tuuu ambayo ni sinister na yanaenda na kinyume na NATIONAL INTEREST na NATIONAL SECURITY
Sasa hiki ni kitendawawili ambacho naamini GREAT THINKERS na INSIDERS wataweza kukitengua
JF home of GREAT THINKETS & INSIDERS
btw
tegemeeni influx wale watetezi wake wa wakati wa sakata la dili lake la Vitambulisho