Mkuu huu ni uongo na kama wewe ni mfuasi wa dini tafadhali nenda katubu kwa kuongopa JF. Ramadhani Mwikalo hana ubavu wa kumpigia Membe kampeni na kumfanya awe waziri, na kwa taarifa yako Mwikalo hata maisha yake USA hayajanyooka na kama angekuwa na ubavu wa kampeni basi angegombea ubunge kwao Tanga na kumtoa Kigoda kwenye jimbo lake.
Mwikalo, Membe na JK ni watu wanaojuwana kwa muda mrefu. JK alisoma shule moja na Mwikalo (sekondari), na Membe alimfahamu Mwikalo alipokuwa ubalozini Canada miaka ya 90, kabla Mwikalo hajahamia USA alipoona maisha yanamshinda Canada. Mwikalo ni IT guy by profession na mwaka 2005 alikwenda Tanzania kama IT consultant wa kanisa Moja Tanga, ndipo alipoonana na Membe wakati wa kampeni. By no means alikwenda kufanya kampeni za Membe. Kwanini akafanye kampeni za Membe, si angefanya za JK aliyesoma naye shule moja na kucheza naye Basketball?
Mkuu naona unataka kuondoa credibility ya JF badala ya credibility Membe. Huu ni uongo mwingine. Membe ni waziri Maskini kuliko mawaziri wote wa JK as of now. HANA UBAVU WA KUWA NA MILIONI 300. Acha uongo. Kama Masilingi alipewa hizo ela na Membe, je Membe angekuwa na ubavu wa kumrudisha nyumbani mdogo wake Masilingi mara baada ya kushindwa kazi katika ubalozi wa Tz Canada?
Sasa kama wewe nawe unaleta uongo na majungu hapa JF, unatofauti gani na huyo Membe unayesema ana umbea na majungu? Katubu.
Mkuu umejichanganya mwanzo unasema JK,Mwikalo na Membe wanajuana muda mrefu.
MEMBE kwenye Tanzania Daima la jumatano hii anasema anajuana na JK toka mwaka sabini.mbele unasema kuwa MWIKALO alimjua Membe kwenye kampeni 2005,katikati umesema walijuana na Mwikalo Canada, kama JK na Mwikalo ni marafiki wa karibu basi lazima Membe angemjua Mwikalo toka hiyo miaka ya 70 aliyosema alikuwa na JK kwani Jk amesoma Tanga school na Mwikalo.
naomba nikukanushe kuwa MWIKALO hajafanikiwa Marekani nakuuliza unajua analipwa kiasi gani kwa utalaam wake wa IT?Mwikalo ni katika waTanzania walifanikiwa kwenye fani ya ITanalipwa malaki ya madola kwa mwaka.Kuonesha kuwa najua vizuri MWIKALO alikwenda MTAMA jimboni kwa Membe 2005 wakati wa uchaguzi.
kwa faida yako na ya wasomaji JK watu wake wa karibu walikuwa ni Marehemu Ditopile Mzuzuri,Hamad Rashid,Seif Shariff Hamad,Edward Lowassa,Rashid Makame,n.k kiasi cha kuwa kampeni meneja wa Seif Sharrif Hamad alipogombea urais wa ZNZ ndani ya ccm Miaka ya 80.
sio lazima kila mtu awe mbunge kwani wewe huwajui wabunge waliopo Bungeni ambao wamefadhiliwa na kufanyiwa kampeni na watu wengine?Mwikalo inawezekana hana nia ya ubunge au hana sifa za kumfanya awe mbunge.
Kauli yako ya kusema Membe ni waziri masikini kuliko mawaziri wote wa JK,huo ni uongo nenda katubu ndugu yangu,kwanza unapokuwa waziri agharabu kuwa masikini,unataka kuniambia kuwa waziri Membe hana pesa mbele ya waziri CELINA KOMBANI?au Waziri WASSIRA,WAZIRI NSWANZUGWAKO,WAZIRI SITTA,KAPUYA,WAZIRI IDD SEIF n.k
ANAWEZA asiwe na pesa kama MAGUFURI,MRAMBA,YONA,MASHA.LAKINI yeye sio waziri masikini kuliko wote.
kWANZA yuko kwenye wizara yenye marupurupu mazuri kutokana na safari anatengeneza pesa nyingi za safari za nje.fuatilia bajeti ya hivi karibuni na pesa zinazotumika kwa Safari za nje ambako Membe ndio kinara,
wizara kama ya Mama Sitta haina safari labda Mama Sitta alazimishe.
PIA MEMBE yuko nyuma ya mradi wa vitambulisho vya Taifa akishirikiana kwa karibu na Mwikalo, so far wao ndio wameshinda huko atavuna pesa nyingi sana ni mabilioni ya shilingi.
Milioni mia tatu kwa MEMBE sio tatizo kwani MWIKALO hashindwi kumsaidia.
kuhusu mdogo wake Masilingi,naomba uelewe mtendaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje ni katibu mkuu sio waziri.chini ya katibu mkuu kuna wakurugenzi wa madawati hawa ndio wenye kujua na kufanya nani kafanya nini?sio MEMBE.
lakini tuchukulie kuwa kweli Membe ndiye kamtoa mdogo wake Masilingi, hiyo sio hoja kwanza Membe ni rafiki na mtu wa karibu wa Masilingi sio mdogo wake.
pia kama kaharibu jambo MEMBE hawezi akamezea kwa vile mdogo wa rafiki yake wakati jambo hilo linaweza kumuhatarishia kampeni yake ya uraisi.
nakupa mfano JK ni rafiki wa LOWASSA sio kama wa LOWASSA,lakini alipoona rafiki yake habebeki akambwaga.tena LOWASSA na JK wametoka mbali sio kama Membe na Masilingi waliojuana kwenye kampeni yake ya kuwania urais 2015.
Naomba uishie hapa usiendelee,namjua MEMBE kama shilingi,ajibadili tabia yake tutampenda.