Membe: Kuna CCM Mpya na CCM ya Zamani

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,796
2,000
7 Julai 2020
Rondo, Lindi

Tanzania

’CCM ilinionya, Ukimchallenge huyu kutaka Urais utafukuzwa chamani ’ Bernard Membe

Sisi wale wa CCM ya zamani tulionekana kama kwamba hatujafanya lolote jema na hawa wanaojiita CCM Mpya.

Membe aelelezea utofauti wa aliyoiita 'CCM ya zamani' na 'CCM mpya'. Hii hapa ndio sehemu ya mazungumzo hayo.

Hapo Jana Bernard Membe,aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na kada wa muda mrefu wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM), alirudisha kadi yake ya uanachama wa CCM kitendo kilichomaanisha ukomo rasmi wa uanachama wake CCM.

Source: BBC Swahili
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,486
2,000
Nasikia harufu ya mzee wa Msoga kwa mbali akipiga jaramba chini kwa chini.

Waandishi mnaoendelea kumuhoji, muwe macho hii nchi ishabadilika.

Huu ubaguzi haujaishia kwa wapinzani tu, sasa umejikita mpaka kwenye chama chao!

Sasa mtaanza kuyaelewa maneno ya Lissu kwa vitendo.
 
Elli M

Verified Member
Mar 17, 2008
42,263
2,000
Hiki ndo kinachoendelea CCM
 
Attachments

  • IMG-20200708-WA0012.jpg
    File size
    27.5 KB
    Views
    0

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,796
2,000
Zile tetesi kuna makundi ndani ya CCM sasa yamethibitishwa na huyu kada wa zamani na makundi hayo mawili ni CCM Mpya vs CCM ya zamani.

Kipindi hiki tutaona 'vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kisiasa na ideolojia' ndani ya CCM katika kuwania nafasi za uongozi wa dola ngazi zote.

Kutoka maktaba :
1 July 2020

Membe: Huu ni utaratibu wa Hovyo kabisa, ni ushamba, Dunia nzima upo Tanzania tu, tuukemee bila woga
Source : ABC HABARI
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
139,572
2,000
Kama anataka urais Membe atulie sasa na aachane na mipasho. Alishafukuzwa na kilichobaki sasa ni kuchanga karata vizuri. Kuongea ongea mipasho mwishowe watu watamzoea na kumwona mlalamikaji tu na mbishi. Amekulia CCM na sasa anajifanya kama haijui CCM vizuri. Bulshit!

Start sounding presidential and leave these petty issues to the petty minded
 
Leo Membe,kesho itakuwa zamu yenu.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,494
2,000
7 Julai 2020
Rondo, Lindi
Tanzania

’CCM ilinionya, Ukimchallenge huyu kutaka Urais utafukuzwa chamani ’ Bernard Membe

Sisi wale wa CCM ya zamani tulionekana kama kwamba hatujafanya lolote jema na hawa wanaojiita CCM Mpya.

Membe aelelezea utofauti wa aliyoiita 'CCM ya zamani' na 'CCM mpya'. Hii hapa ndio sehemu ya mazungumzo hayo.

Hapo Jana Bernard Membe,aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na kada wa muda mrefu wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM), alirudisha kadi yake ya uanachama wa CCM kitendo kilichomaanisha ukomo rasmi wa uanachama wake CCM.

Source : BBC News Swahili
Hivi bado kuna watu wanatatanishwa na hizi "Mpya"?

"CCM 'Mpya'"

"Tanzania 'Mpya'"

"New Victoria" ile meli iliyokarabatiwa, inaitwa mpya!

Na pengine kuna "Mpya" nyingi nyingine zipo njiani kuzinduliwa hivi karibuni tukielekea kwenye kampeni na uchaguzi.

Ni nani 'Great Thinker' wa hapa JF anayeweza kutudadavulia maana ya haya yote wakati huu?

Au, ilitakiwa nianzishe mada ya pekee juu ya swali hilo?

Ngoja niiache hapa nione kama kuna watu watamwaga fikra zao hapa.

Ninachoweza kudokeza ni kwamba huu ni mkakati maalum unaofanywa kwa sababu maalum.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,494
2,000
Nasikia harufu ya mzee wa Msoga kw mbali akihusika

Waandishi mnaoendelea kumuhoji, muwe macho,hii nchi ishabadilika.

Huu ubaguzi haujaishia kwa wapinzani tu,sasa umejikita mpaka kwenye chama chao!

Sasa mtaanza kuyaelewa maneno ya Lissu kwa vitendo.
Leo nilikusema mahala, hapa JF, na kabla ya siku kwisha unatoa kitu kama hiki hapa.

Simamia humo humo, usiyumbeyumbe. Huo ndio ukomavu.

Na hawa watu (unaowazungumzia hapa) kuendeleza unafiki wao kwa wakati huu hakutawaacha salama.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,494
2,000
Zile tetesi kuna makundi ndani ya CCM sasa yamethibitishwa na huyu kada wa zamani na makundi hayo mawili ni CCM Mpya vs CCM ya zamani.

Kipindi hiki tutaona 'vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kisiasa na ideolojia' ndani ya CCM katika kuwania nafasi za uongozi wa dola ngazi zote.

Kutoka maktaba :
1 July 2020

Membe: Huu ni utaratibu wa Hovyo kabisa, ni ushamba, Dunia nzima upo Tanzania tu, tuukemee bila woga
Source : ABC HABARI
Jamaa sasa anaweka mhuri wake, hataki tena aonekane anadandia kwa wengine.

Tukipita salama kwenye uchaguzi huu na akabaki, hapo ndipo tutakapowekewa 'Nembo Mpya' ambayo bado tulikuwa hatujaiona katika miaka hii mitano inayokwisha.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,282
2,000
7 Julai 2020
Rondo, Lindi
Tanzania

’CCM ilinionya, Ukimchallenge huyu kutaka Urais utafukuzwa chamani ’ Bernard Membe

Sisi wale wa CCM ya zamani tulionekana kama kwamba hatujafanya lolote jema na hawa wanaojiita CCM Mpya.

Membe aelelezea utofauti wa aliyoiita 'CCM ya zamani' na 'CCM mpya'. Hii hapa ndio sehemu ya mazungumzo hayo.

Hapo Jana Bernard Membe,aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na kada wa muda mrefu wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM), alirudisha kadi yake ya uanachama wa CCM kitendo kilichomaanisha ukomo rasmi wa uanachama wake CCM.

Source : BBC News Swahili
Mmomonyoko rasmi umeanza...
 
kipande

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
2,002
2,000
Kama anataka urais Membe atulie sasa na aachane na mipasho. Alishafukuzwa na kilichobaki sasa ni kuchanga karata vizuri. Kuongea ongea mipasho mwishowe watu watamzoea na kumwona mlalamikaji tu na mbishi. Amekulia CCM na sasa anajifanya kama haijui CCM vizuri. Bulshit!

Start sounding presidential and leave these petty issues to the petty minded
Umeongea vizuri sana, Subira ndo iliyomgharimu membe. Inaonekana zile expectations zake za 2015 bado zilikua zinaendelea kumla ndani kwa ndani. Hakutegemea game ingebadilika vile mpaka akaporwa tonge mdomoni. Hapa ndipo naamini maneno ya Salmin Amour, kwamba U Rais unakuja kwa ridhaa za watu na idhini ya Mwenyezi Mungu. Mungu hakumpa idhini yeye kuwa Rais, ndo maana yakatokea yale yaliyotokea. Hili lazima alikubali. Kama angejifunza kwa yale yaliyomtokea Kikwete mwaka 95, pamoja na kushinda kwenye kura za maoni lakini akaambiwa kura zake hazitoshi. Lakini alivuta subira na baada ya miaka 10 kwa idhini ya M/Mungu akawa Rais.

Utamaduni huu wa chama wa kumwachia Rais aliye madarakani kumalizia muhula wa pili bila kupingwa, naye ameuishi na kuubariki akiwa ndani ya CCM tena akiwa kwenye vyombo vikuu vya maamuzi. Kama hakua anakubaliana nao, alipaswa kuupinga tokea kipindi hicho Kwanni aje kuupinga sasa wakati akiwa na maslahi yake binafsi. Matokeo yake akaanza kuleta chokochoko za kutaka kuuharibu utamaduni wa chama. Ukileta chokochoko kwenye chama lazima nawwe uchokolewe that is merely a Principal.
 
MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
581
500
Anayependwa kidemocrasia huwa pia ana uwezo mzuri uliomfanya apendwe, Nini kilitokea 2015 Democrasia ikatupwa kule? Waliosababisha vurugu, ile je wananchi wamesha-wasamehe kweli?, au wamewasahau kweli?
Hii ikikumbukwa vizuri, bado kuna wengi watagundua Vita inaendelea, watafanya walichofanya 2015.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom