Membe: Kuna CCM Mpya na CCM ya Zamani

Nasikia harufu ya mzee wa Msoga kwa mbali akipiga jaramba chini kwa chini.

Waandishi mnaoendelea kumuhoji, muwe macho hii nchi ishabadilika.

Huu ubaguzi haujaishia kwa wapinzani tu, sasa umejikita mpaka kwenye chama chao!

Sasa mtaanza kuyaelewa maneno ya Lissu kwa vitendo.
hapo mstari wa mwisho umeongea point..kuna machalii wangu huku nilipo huwa nawakumbusha sana hayo maneno ya lissu.. "Wakimalizana na sisi....................
 
think differently mkuu!! you sound like them old and wrong thinkers!! ni ngumu kwa nyani kuona kundule! Maembe anataka nayeye kugombea urais na sheria ya chama ilimruhusu kosa lake nini?lets all choose CCM Academia!! Lets us all live in modernity! Lets us stand in the truth! mimi si shabiki wa Maembe ni shabiki wa Mkulu but sikubaliani na CCM walichomfanyia Membe!!

Sote tunajua Mkulu hana mpinzani ila sheria za members kugombea zifuatwe sio kanuni kuwa hakuna kumchallenge Rais alie madarakani, mi sielewi, mtu anaetaka kupimana ubavu na Mkulu katiba ya chama imeruhusu kwanini Maembe kazuiwa? huo ni ujuha ni vizuri chama kiondoe hiyo fursa kabisa ndio sawa!!

The strongest man is the one who stands alone!! Maembe is the strongest man. He deserves to contest against Mkulu if he gets Arab money and ACT back up! He can think to contest for presidency consecutivelly kwa fifteen years ( longterm plan) labda Allah will grant him his wishes!! Asiende chadema inajifia!!
Mbona hakuchukua fomu awamu ya pili, ya mzee Mkapa?, mbona hakuchukua fomu awamu ya pili ya mzee Kikwete? Iweje sasa ndo aone utaratibu wa CCM ni mbaya ili Hali alishiriki kuujenga? Membe kachanganyikiwa sio bure
 
Jenerali Ulimwengu - Kila ajaye ana jipya, hatuendi kokote



source
: Jenerali Online


Katika makala yangu ya mwisho, wiki mbili zilizopita, nilionyesha jinsi ambavyo wakuu waliostaafu wanvyolalamikia mambo ambayo wao wenyewe waliyasababisha walipokuwa madarakani kwa kutotaka kusikiliza kilichokuwa kikisemwa na wengine, wakidhani kwamba maoni ya mkuu ni bora kuliko ya wale wasio na ukuu.

Marais wastaafu wawili walikuwa wametoa maoni yao kuhusu mporomoko wa viwango vya elimu, wakisema kwamba hili ni janga la taifa. Ni kweli kwamba elimu yetu imeporomoka kwa kiasi cha kutisha, kama ambavyo tafiti zetu zinavyoonyesha. Lakini hao wawili walikuwa madarakani wakati fulani, na kila aliyejaribu kuwaambia hayo ambayo wanayasema leo walimuona kama mwendawazimu, punguani, muongo au ‘mvivu wa kufikiri.’

Nachelea kufikiri kwamba mkuu tuliye naye sasa, kwa kufuata mfano wao, anaweza kuwaita hao watangulizi wake majina hayo. Natumai hatofanya hivyo bali atajifunza kutokana na kasoro zao ili naye asije akaanza kulalama baada ya kutoka madarakani kuhusu mambo ambayo alikuwa na uwezo nayo alipokuwa madarakani lakini akawabeza waliotaka kumshauri.



Tukumbushane akili: Serikali ina wajibu wa kutawala, na katika shughuli hiyo, ni serikali pekee yenye wajibu huo. Hakuna chombo kingine chenye wajibu wa, au haki ya, kutawala isipokuwa serikali. Minajili ya kufanya kazi hiyo, serikali imepewa vyombo vya utekelezaji, kama vile utawala wa raia, pamoja na asasi za kimabavu, kama vile majeshi, idara za upelelezi na ujasusi, vitengo vya makachero na wachunguzi.

Lakini, pamoja na nguvu zote hizo ilizopewa serikali kwa ukiritimba, haiwezekani serikali yo yote ikatamba kwamba ina ukiritimba wa akli, maono ama ujuzi katika mambo yote. Idadi yote ya watu waliomo serikalini katika ngazi ote ni ndogo mno, na uwezo wa kila mmoja wao kumiliki akili, maono, taarifa na weledi ni huo anaoweza kuwa nao mtu mmmoja, na uwezo wao wote ukichanganywa pamoja bado utakuwa ni kidogo ukilinganishwa na uwezo wa pamoja wa raia wa nchi husika.

Ndiyo maana ni hatari kwa watawala kudhani kwamba wanao uwezo wa utambuzi na uelewa kuwazidi wananchi wao. Na ndiyo maana, baada ya karne nyingi za mapambano baina ya matabaka hasimu, wenzetu walioendelea walitambua kwamba hawana budi kujenga mifumo na michakato inayotambua upungufu wa uwezo wa watawala, na kuweka utaratibu wa kurutubisha uwezo huo kwa kuukutanisha na uwezo unaopatikana miongoni mwa wananchi wasio na dhima ya kutawala.



Kutokana na kutambua hivyo, wenzetu waliweka utaratibu kama vile uwakilishi katika halmashauri na mabunge ambamo wawakilishi wao walipeleka hoja zao na kuzishindanisha, maslahi ya hawa yakikinzana na maslahi ya wale, huku pande zote zikizingatia maslahi ya pamoja ya kitaifa. Miundo na mifumo hiyo tulirithishwa na wakoloni wakati wakiondoka, na hadi sasa tunayo, hata kama tumeifanya ni kama mazindiko hasi yasiyokuwa na faida yo yote kwetu.

Lakini wenzetu wamekuwa wakiendelea na mifumo na michakato yao, ambayo wameipa uzima na kuifanya hai. Mabunge yao yanafanya kazi ya kuzikosoa, kuzielekeza na kuzidhibiti serikali zao. Halmashauri zao zinafanya vivyo hivyo. Inapofikia kwamba watawala wameonekana hawana usikivu, mabunge haya na halmashauri hizi inao uweo wa kuwaondoa madarakani.

Kwetu sisi tumebaki na mabunge na halmashauri magarasa, mapambo ambayo yanapendeza kuyaangalia na kumuonyesha mgeni, lakini huwezi kuyatuma sokoni. Ni mpangilio ulio ghali mno, lakini ambao hautuzaliii matunda tuliyotaraji.



Hata hivyo, hali kama tuliyo nayo, kimsingi siyo ya kwetu peke yetu. Wakati katika historia ya binadamu kumekuwapo na misuguano baina ya matabaka mbali mbali, au makundi mbali mbali, kila moja likipigana ili kuongeza manufaa yake, lakini kila muhula wa mapambano hayo hulizipeleka jamii husika katika ngazi mpya juu ya pale zilipokuwa awali.

Sisi tunaelekea kuwa tofauti. Ni kama vile tunatembea kinyumenyume. Mahali ambapo tulikwisha kupitia jui ndiko tunakotaka kurejea leo. Ni mithili ya watu wazima wanaotaka kunyonya vidole, kama watoto. Hatuelekei kama watu wanaojua hatua za kihistoria walizozipitia.

Mojawapo ya matatizo yanayotukwaa ni kutokuwa na utaratibu unaoeleweka na unaoufuatwa wa kupokeana utawala (achana na uongozi kwa sasa). Alipoondoka Julius Nyerere na kumwachia urais Ali Hassan Mwinyi, kwa miaka mitano Mweinyi alionekana akifanya kazi nzuri mno, kwa sababu, kimsingi, Nyerere alikuw ahajaondoka moja kwa moja.

Kwanza Nyerere ndiye alikuwa bado mwenyekiti wa chama-tawala. Maamuzi yote yalipitia mikononi mwachama kabla hayajatekelezwa serikalini. Lakini pia, waziri mkuu wa Mwinyi alikuwa Joseph Warioba, ambaye mtazamo wake ulifanana sana na ule wa Nyerere, hata kama alikuwa hapokei maelekezo yo yote toka kwa Mzee. Muhula wa wa pili wa Mwinyi ukaja kuwa tofauti kabisa na ule wa kwanza kwa sababu, kwanza Nyerere aliachia uenyekiti na Warioba akaondolewa kwenue uwaziri mkuu, na hapo ndipo tukaziona sura halisi za Mwinyi.



Tangu hapo tunachoshuhudia ni kila anayekuja kuja na lake, na hakuna mwendelezo way ale aliyoyakuta. Wakati mwingine wakuu wanatoa taswira kama vile utawala mpya umeingia kwa kuupindua utawala uliopita, au kama vile chama kipya (kilichokuwa upinzani) kimeingia madarakani. Kila anayeingia anaingia na timu yake ambayo lengo lake kuu ni kufutilia mbali yale yote yaliyofanywa na mtangulizi wake.

Katika awamu inayoitwa ya tano (binafsi naona awamu imekuwa ni moja tu tangu 1961), mambo mengi makuu ya ‘awamu’ ziliopita yametupwa nje, hata yale yenye manufaa ya dhahiri, kwa sababu wakuu wapya wana upendeleo kwa mambo mengine tofauti. Najiulia iwapo ‘awamu’hii itakapopita hakutakuja wengine naao wakayatupilia mbali haya tunayoyaona yakifanyika hivi sasa? Hili nitalieleza kwa kina huko mbele.

Kwa jinsi hii, hatuendi ko kote, kwa sababu hatulimbikizi matendo, ujuzi, uzoefu na manufaa; kila siku sisi ni watu wa kuanza upya.
Source : Kila ajaye ana jipya, hatuendi kokote
 
Nasikia harufu ya mzee wa Msoga kwa mbali akipiga jaramba chini kwa chini.

Waandishi mnaoendelea kumuhoji, muwe macho hii nchi ishabadilika.

Huu ubaguzi haujaishia kwa wapinzani tu, sasa umejikita mpaka kwenye chama chao!

Sasa mtaanza kuyaelewa maneno ya Lissu kwa vitendo.
Mzee GSM hausik na huu uchu wa Membe. Kwanza mzee wa GSM anamuogopa Magu kama moto, hawezi kudiriki kumchokonoa
 
KUSADIKIKA by Shabaan Robert

Mvutano katika jamii, usiotaka fikra tofauti tofauti

Mapitio mafupi ya ktk kijitabu hiki chenye kurasa takriban 40 chenye simulizi ya riwaya hekaya ya Kisa cha Bwana Karama vs Bwana Majivuno na umuhimu wa kusikiliza fikra mbadala na kujifunza ili kuchukua ushauri mwema wa ndani na nje

Source : Jenerali Online
 
Kama Ben Membe anataka kuwa Rais wa nchi hi, angetulia tu na kuomba msamaha kwa CCM. 2025 wangemfiria. Kwa sasa ndio basi tena hadi kufa. Ni kama maalim Seifu. Angetulia na kuomba msamaha kwa sasa wangekuwa Rais wa Zanzibar
 
10 Julai 2020
Dodoma, Tanzania
BREAKING: RAIS MAGUFULI ATANGAZA MEMBE KUFUKUZWA CCM, AMTUMIA UJUMBE KINANA



Source : Millard ayo
 
Back
Top Bottom