Membe jiandae kisaikolojia

Alimpigania sana pale dodoma, bt timu ya mamvi ikamshinda nguvu. Bt kwa sasa bwana huyu hana nguvu yoyote nyuma yake zaidi ya wimbi kubwa la maadui wanaojifanya marafiki, hasalimiki, hasalimiki.
Nani allkwambia team mamvi Haina nguvu? Halafu km mzee wa msoga alitoshana nguvu na mtu ambae alikuwa alikuwa nje ya serikali ataweza vipi kupambana na mtu anayeiongoza serikali?

By the way magu anajua anaopambana nao kwamba sio kina membe bali ni system ya 10percent. Unafikiri atakuwa amekaa tuu anasubiri viongozi wa dini wamuombee? Wacheni kujidanganya .
 
Anapotoshwa na siasa za mitandaoni ....anapata faraja na nguvu za kijinga akiona comment za kina Salary slip anajitoa ufahamu lakn uhalisia na hulka ya kibinadamu lazima athibitishiwe kwa matendo kwamba kweli amekatwa mkia na kwa jamii za kifugaji yani kwenye zizi la Ng'ombe mnyana aliyekatwa mkia huwa na nuksi kama siyo kutengwa ....
 
Ukitaka kumpiga adui yako usimuambie kwamba utampiga, atajiandaa vizuri zaidi ili akudhibiti.

Haya unayosema usifikiri membe hayajui.
 
Kukaa kimya ni ujinga uliopitiliza!!!

Jiwe mwenyewe ana makashifa mengi tu maana na yeye ni wale wale.

Hamuwezi kuziba watu midomo kwa vitisho vya aina hii na vingine ambavyo mmekuwa mkivitumia.

Hovyo kabisa!!!
Sawa ila sio akina Membe aisee. Siwezi kushiriki kushabikia watu calibre ya akina Membe kwavile tu sikubaliani na JPM! Wengine tulichofanya mlipompokea EL tutafanya kwa Membe and a like hadi tutapokuja kupata wapinzani wa kweli bila DNA chafu kutoka Lumumba ndio tutasimama nae! Hata kama si kizazi changu basi na bora mfumo uendelee kutuletea watu wanaoona wanafaa lakini si hawa.

Tukiona nchi inataka kutwaliwa na mtandao wa mafisadi hatutakubali hata kama wapinzani ndio wanaotumika kama daraja (wao wanafikiri ni shortcut ya ikulu) Bora akina JPM kuliko watu ambao wakiongoza miaka 20 mfululizo hii nchi itakuwa either Congo au Nigeria. Never!!!
 
mi nadhani hii nchi ni huru kama membe anahisi anatosha kuwania u rais basi apambane ilimradi asivunje katiba, alikuwepo nyerere muasisi alipita mwisho wa siku vivo hivyo ata magufuli atapita kama wenzie maana nchi ni yetu sote kati ya watu mil 50 haiwezekani mwenye uwezo wa kuongoza akawa magufuli peke ake basi tutakuwa tumelaanika,...No one who is perfect nijambo la wazi huwezi pendwa au kukubalika na kila mtu ww unae ona anafaa kuongezewa muda yupo mwenzio anaetamani hata kesho atoke,...Serikali ya kina membe ndo ileile serikali ya akina magufuli wote walikuwepo kwene baraza la mawaziri.....
Huyu mkatwa mkia aliyewahi kukiri wanapishana hewani utafikiri nchi inaungua moto sijui ameingiwa na tamaa gani. Watu tunafkiria kumuongezea jiwe muda yeye analeta za kuleta
 
Kimsingi aliyeyazungumza haya anamlenga Rais aliyepita bila kujijua, maana utamzungumziaje Waziri afanye hayo kama ni kweli bila mkuu wa nchi kutoa kibali... Kimsingi mambo yenyewe hayana ukweli wowote yamejaa majungu, fitina na hayana msaada wowote kwa sasa....
 
Kwahiyo kuonyesha nia kugombea ni uhaini huko CCM sikuhizi? Siwaelewi nyie ndugu!

As per CCM constitution mtu yeyote anahaki ya kugombea katika wakati muafaka, and constitutionwise wakati muafaka ni miaka mitano, traditionally mlikuwa mnaachiana lakini it was as per utendaji, utendaji ungekuwa mbovu kama wa sasa wangetokeza wengine kugombea na kupuuza utamaduni and mind you utamaduni si Superior kwa constitution!!!

Huyo mtu wenu mnasema ni kipenzi cha watu, why worry then??? Nadhani kati ya tawala zote zilizopita hii ndio imekaa kipropaganda zaidi and inayo undeeperforf kwa kiwango kikubwa na zaidi ya yote haina uongozi shirikishi ila ina kiongozi mmoja, mtawala!!
 
Sasa unamshauri nini
 
HEBU TUPENI KWANZA FORMATION YA "CC" ILE AMBAYO HUWA INAJADILI WAGOMBEA.JE? KAMA CHAIRMAN NI MGOMBEA NA YEYE ANAKUWA MJUMBE AU ATASUBIRIA MAAMUZI YA "CC".Hivi mfano CC ikaamua kuja na MAJINA ambayo M/kiti halimo nini kitatokea?.
 
HEBU TUPENI KWANZA FORMATION YA "CC" ILE AMBAYO HUWA INAJADILI WAGOMBEA.JE? KAMA CHAIRMAN NI MGOMBEA NA YEYE ANAKUWA MJUMBE AU ATASUBIRIA MAAMUZI YA "CC".Hivi mfano CC ikaamua kuja na MAJINA ambayo M/kiti halimo nini kitatokea?.
Unaota mkuu. Inamaana Mangula, Dk. Bashiru, Makongoro Nyerere, Dk. Shein, Samia, Majaliwa wamkatae Magufuli?

Hakuna ujasiri wa hivyo mkuu.
 
Rais anatoa kibali baada ya wataalam kumshauri,na inawezekana walimshauri kipotoshaji ili wao wabenefiti(Membe).hivyo Rais aliepita hana kosa na kumbuka anakinga ,kazi kwa Membe na his allies

Dawa ya jeuri ni Kiburi,aendelee kuchongoa mdomo wake,atapata anachokitafuta,haya masuala yapo kwenye kumbukumbu,yana maana sana kwa kipindi hiki tulichonacho katika siasa nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…