Meli za mizigo zapungua bandari Dsm

Meli za mizigo zapungua bandari Dsm

Yana mwisho walijua wangeiba milele,bora tuishi na hizo chache kuliko kujaza mimeli mingi wakati serikali hakuna inachopata.

Wanaokimbia si watanzania pekee bali na wageni pia ambao hatunufaiki na kodi zao isipokuwa port charges na mengineyo so swala la kukwepa kodi hapo halipo. Usipokuwa mdau wa bandari kama mm utalichukulia hili jambo kirahisirahisi sana.

Wanachokikimbia bandarini si kodi bali ni usumbufu wa kijinga kabisa. Nitatoa mfano, walinzi kwa sasa bandarini ni polisi ambao hawafahamu chochote khs port documents. Kuna jamaa yangu walimkamata na mzigo akawapa docs za huo mzigo. Polisi wakasema wao hawawezi kuzielewa hizo docs so wanamtafuta mtu wa kuwasomea. Jamaa alistuck kwa 12 hrs ndio akawa cleared-huu kwangu ni upuuzi wala si utumbuaji wa majipu.
 
Kuna possibility kuwa:
  • unaitishia serikali ili ilegeze msimamo wake kuhusu bandari yake kutoendelea kuhujumiwa na wajanja wachache
  • hao waliohama ni wale waliozoea kutuibia sasa wanaona pamekuwa pamoto ndiyo wamekwenda hukoo, tena waambie kabisa ukiwaona, mambo ya dezo yalishaondoka na awamu ya dezo

Mkuu hilo ndilo lengo lake kuu. Majirani zetu wanao tegemea bandari ya Dar wanampongeza JPJM kwa kusafisha uhozo pale TPA na TRA halafu hapa wanajitokeza watu wanajaribu kutishia nyau!!!!
 
Hizo hizo chache zinatosha kama watalipa kodi ipasavyo.kuna haja gani ya kuzaa watoto kumi hali yakuwa 8 matahira?
 
Zije chache zenye mizigo ya watu wasiokwepa kodi.... Kutujazia mimeli lundo wakati nchi haifaidiki chochote nao ni ufala tu
 
sawa tu bora chache kuliko nyingi za wakwepa kodi

Mhhhhh, miss chaga unauhakika?. Ngoja nikupe kasiri, Forodha sio chanza kizuri cha Kodi kwa Nchi yeyote ile. Kazi yao kubwa ni ku-facilitate trade, then msisitizo wa kodi uwe kwa bidhaa zilizingizwa na kuuzwa Nchini.
Ukiwazingua sana wafanyabishara na kuairisha kuleta mizigo, mnakosa kodi zote mbili zile za ndani na za forodha. Na ndio maana kiongozi yeyote mjanja kama JK huwa wanalegeza taratibu za uingizaji mizigo ili iingie mingi Nchini, Kisha mikakati mizuri na makini hupangwa ili kukusanya kodi za mizigo hiyo ikiwa ndani(Domestic Rev.).

Tulipaswa kuwa wakali kama tungekuwa na Viwanda vya kutosha Nchini ambavyo tungetegemea wanazalisha na kuuza Nje na Ndani ya Nchi. Sisi viwanda hatuna halafu tunajifanya wajanja. Kwa stahiri hii, tutavuna tusiyoyatarajia.
 
Wanaokimbia si watanzania pekee bali na wageni pia ambao hatunufaiki na kodi zao isipokuwa port charges na mengineyo so swala la kukwepa kodi hapo halipo. Usipokuwa mdau wa bandari kama mm utalichukulia hili jambo kirahisirahisi sana.

Wanachokikimbia bandarini si kodi bali ni usumbufu wa kijinga kabisa. Nitatoa mfano, walinzi kwa sasa bandarini ni polisi ambao hawafahamu chochote khs port documents. Kuna jamaa yangu walimkamata na mzigo akawapa docs za huo mzigo. Polisi wakasema wao hawawezi kuzielewa hizo docs so wanamtafuta mtu wa kuwasomea. Jamaa alistuck kwa 12 hrs ndio akawa cleared-huu kwangu ni upuuzi wala si utumbuaji wa majipu.

Kwani documents hizo zimeandikwa kiyunani au mpaka apatikane mswahili mwenye shahada ya PhD kuitafasiri? Mbona ma clearing agents ni watu wa kawaida tu - wengi wao darasa la saba au form4 na ujanja mwingi tu wa kuwabambikia wateja kodi/charges za uongo na kweli wakitumia docoments za kughushi, unsuspecting clients wameibiwa kweli kweli na wajanja hawa.

Kwa nini wanalalamikia uwepo wa Polisi Bandarini, mtu ambaye anafanya kazi zake kihalali anawezaje kuogopa Polisi, hata kusoma documents ma Polisi wanaweza kupewa semina ekelekezi ya wiki moja tu ikawawezesha kufanya kazi za hapo Bandarini kwa ufanisi.
 
Meli idadi kama ya ile kawaida sema vijana was clearing mmebanwa kupiga madili yenu ya wizi na utapeli...
Na huko kubanwa kwenu kumeleta heshma mjini na zile mbwembwe zenu za kutapaza na kununua vindoo vya Heineken na Windhoek kwenye pubs
zote zimeisha..
Asante JPM
 
Mhhhhh, miss chaga unauhakika?. Ngoja nikupe kasiri, Forodha sio chanza kizuri cha Kodi kwa Nchi yeyote ile. Kazi yao kubwa ni ku-facilitate trade, then msisitizo wa kodi uwe kwa bidhaa zilizingizwa na kuuzwa Nchini.
Ukiwazingua sana wafanyabishara na kuairisha kuleta mizigo, mnakosa kodi zote mbili zile za ndani na za forodha. Na ndio maana kiongozi yeyote mjanja kama JK huwa wanalegeza taratibu za uingizaji mizigo ili iingie mingi Nchini, Kisha mikakati mizuri na makini hupangwa ili kukusanya kodi za mizigo hiyo ikiwa ndani(Domestic Rev.).

Tulipaswa kuwa wakali kama tungekuwa na Viwanda vya kutosha Nchini ambavyo tungetegemea wanazalisha na kuuza Nje na Ndani ya Nchi. Sisi viwanda hatuna halafu tunajifanya wajanja. Kwa stahiri hii, tutavuna tusiyoyatarajia.

Mkuu wachache sana wanalielewa hili. Wazambia, wacongo na wengineo wanakimbilia Walvis bay na Mombasa-kwani walikuwa wanalipa kodi hapa before?Jibu ni no kinachowakimbiza ni usumbufu.

Mfano kuna kipindi walisimamisha scanning so container likawa linafunguliwa moja baada ya jingine. Before wageni walikuwa wanakaa hotelini chini ya wiki moja kusubiri mizigo yao zikaongezeka na kuwa wiki 2 au zaidi- hasara yote hii waendelee kutumia Dar port ya nini wakati Mombasa within 2 days unamaliza kila kitu?
 
Mhhhhh, miss chaga unauhakika?. Ngoja nikupe kasiri, Forodha sio chanza kizuri cha Kodi kwa Nchi yeyote ile. Kazi yao kubwa ni ku-facilitate trade, then msisitizo wa kodi uwe kwa bidhaa zilizingizwa na kuuzwa Nchini.
Ukiwazingua sana wafanyabishara na kuairisha kuleta mizigo, mnakosa kodi zote mbili zile za ndani na za forodha. Na ndio maana kiongozi yeyote mjanja kama JK huwa wanalegeza taratibu za uingizaji mizigo ili iingie mingi Nchini, Kisha mikakati mizuri na makini hupangwa ili kukusanya kodi za mizigo hiyo ikiwa ndani(Domestic Rev.).

Tulipaswa kuwa wakali kama tungekuwa na Viwanda vya kutosha Nchini ambavyo tungetegemea wanazalisha na kuuza Nje na Ndani ya Nchi. Sisi viwanda hatuna halafu tunajifanya wajanja. Kwa stahiri hii, tutavuna tusiyoyatarajia.
okey
 
Kwani documents hizo zimeandikwa kiyunani au mpaka apatikane mswahili mwenye shahada ya PhD kuitafasiri? Mbona ma clearing agents ni watu wa kawaida tu - wengi wao darasa la saba au form4 na ujanja mwingi tu wa kuwabambikia wateja kodi/charges za uongo na kweli wakitumia docoments za kughushi, unsuspecting clients wameibiwa kweli kweli na wajanja hawa.

Kwa nini wanalalamikia uwepo wa Polisi Bandarini, mtu ambaye anafanya kazi zake kihalali anawezaje kuogopa Polisi, hata kusoma documents ma Polisi wanaweza kupewa semina ekelekezi ya wiki moja tu ikawawezesha kufanya kazi za hapo Bandarini kwa ufanisi.

Comment yako ipo kinadharia zaidi sitaijibu moja kwa moja. Like I said before, mm ni mdau wa bandarini nilichoeleza hapo ni kile ninachokishuhudia day in day out sijasimuliwa na mtu. It is up to you kukichukua au kukiacha. Serikali inafikiria kuwasomesha basic knowledge ya clearing & forwarding hao polisi wa ulinzi ili wajue kipi wanachoangalia kwenye hizo docs so swali lako la Phd limejibiwa na serikali si mimi.
 
Hivi kuzunguka zunguka na bill of lading TPA na TRA nako kunahitaji akili za ziada kweli? Watu wenye mizigo wanaweza kufanya kazi hiyo wakidhamilia wakalipa ushuru stahiki including wharfage charges kama kuna ulazima.

Wenye mizigo wanawapa kazi ma agent kwa kuwa hawataki usumbufu/wana shughuli nyingine za kufanya lakini sio kwamba hawana akili/uwezo wa ku clear mizigo yao bandarini.
 
Bora zipungue tu, watazoea tuu!! Ngosha chapa kazi hadi na ma clearing and forwarding uchwara waisome namba pia.. Hapa kazi tu, soon tutaheshimiana tu hapa mjini.
 
Mm nafanya ya clearing and forward nimeshughudia idadi ndogo za meli zina beth bandarini tangu wanze kutumbua majibu nchini meli ngingi zimeamia bandari ya Mombasa Kenya yaani hakuna kabisa
Bado sijakusoma vizur mkuu, hapa unamaanisha wale wachepuka kodi waruhusiwe kuendelea kuchepuka ili meli ziwe nyingi ama,,, pls explain
 
Kilichowafanya wwkimbilie mombasa nini? Kwa sababu wameambiwa walipe kodi siyo.basis waende bandari tutafugia Samaki.
 
Harbour View Plus

Leo ni tarehe 10 March ambapo ripoti ya bandari Dsm inaonyesha kuwa meli 54 zimewasili kwa mwezi wa 3(wastani wa meli 5 kwa siku) kumbuka leo ni tarehe 10 March.

Mwezi wa 2 ziliwasili meli 190(wastani wa meli 6 kwa siku), January 172(wastani wa meli 6 kwa siku).
Mwaka Jana jumla ya meli 1093 ziliwasili kwa size tofautitofauti toka januari 1 mpaka December 31,2015(wastani wa meli 3 kwa siku)
Huu nd'o uhakika..mleta uzi atakuwa ni katika wale waliotumbuliwa..
 
Bandari ya Dsm haihudumii watanzania pekee. Hili jambo si la kimzahamzaha viongozi watafute sababu kwanini meli zimepungua kiasi hiki na hatua stahiki zichukuliwe haraka sana kwani madhara yake kiuchumi ni makubwa mno. Hizo 1.6-2 tilioni wanazojisifu nazo zitayeyuka soon kwani nyingi ni arrears so hayo mapato hayakosustainable.

Kwanza ni kujua kua hii habari ina ukweli. Na mtoa mada ametoa hizo habari tika wapi? Waandishi wa habari wenyewe wako wapi wakuweza kuandika habari kama hii?
 
Mhhhhh, miss chaga unauhakika?. Ngoja nikupe kasiri, Forodha sio chanza kizuri cha Kodi kwa Nchi yeyote ile. Kazi yao kubwa ni ku-facilitate trade, then msisitizo wa kodi uwe kwa bidhaa zilizingizwa na kuuzwa Nchini.
Ukiwazingua sana wafanyabishara na kuairisha kuleta mizigo, mnakosa kodi zote mbili zile za ndani na za forodha. Na ndio maana kiongozi yeyote mjanja kama JK huwa wanalegeza taratibu za uingizaji mizigo ili iingie mingi Nchini, Kisha mikakati mizuri na makini hupangwa ili kukusanya kodi za mizigo hiyo ikiwa ndani(Domestic Rev.).

Tulipaswa kuwa wakali kama tungekuwa na Viwanda vya kutosha Nchini ambavyo tungetegemea wanazalisha na kuuza Nje na Ndani ya Nchi. Sisi viwanda hatuna halafu tunajifanya wajanja. Kwa stahiri hii, tutavuna tusiyoyatarajia.
Mbona data hazioani na maelezo yako...
http://196.43.221.2/HVPlus/Reports/VESSELCALLSPERMONTH.pdf
 
Back
Top Bottom