Suresawa tu bora chache kuliko nyingi za wakwepa kodi
Acha uongo weka takwimu hapa..namba hazidanganyi....FYI, basi hizo meli zimeleta bidhaa za nchi jirani..... "Statistics zipo TPA/Wizara ya uchukuzi na Wiz Fedha" waianike hapa ...hata kauchumi kamedorora ....
Mapato yaliokusnywa ni yale ya 2015 (malumbikizo ya awali) !!
new Year 2016 ni vichekesho...tu
Kweli kabisa, ila ukitizama namba zinakwenda zikishuka,Tunashukuru sana mkuu kwa kuweka Data & Numbers. Naona WAHUJUMU UCHUMI wanahaha na kutokwa makamasi kila kona.
Wee komalia takwimu..meli zinateremsha silaha za jirani.....Acha uongo weka takwimu hapa..namba hazidanganyi....
Naona ni kinyume chake, wastani wa siku 10 za mwezi huu wa tatu mwaka 2016 ni mkubwa kuliko wastani wa mwaka jana wote wa 2015. Sijui, labda kuna kitu sijaelewa, ila naona kama vile zimeongezeka.Leo ni tarehe 10 March ambapo ripoti ya bandari Dsm inaonyesha kuwa meli 54 zimewasili kwa mwezi wa 3(wastani wa meli 5 kwa siku)Mwaka Jana toka januari 1 mpaka December 31,2015 (wastani wa meli 3 kwa siku)
Chukua tano aisee, kuna watu walikuwa wanaingiza mizigo kwa kukwepa kodi afu wenzao wanalipa kodi stahiki unategemea ushindani utakuwa wa haki kweli?Sasa sisi tuliokuwa tunalipa kodi halali ndo tutaona faida, pumbavu sana watoa rushwa walikua wanatucheleweshea mizigo hadi mtu unapata hasara.
Na bado mpk maji muite mmangoja nifunge bakuli... ila magufuli katukomoa aisee...
Mm nafanya ya clearing and forward nimeshughudia idadi ndogo za meli zina beth bandarini tangu wanze kutumbua majibu nchini meli ngingi zimeamia bandari ya Mombasa Kenya yaani hakuna kabisa
SalaamNaona ni kinyume chake, wastani wa siku 10 za mwezi huu wa tatu mwaka 2016 ni mkubwa kuliko wastani wa mwaka jana wote wa 2015. Sijui, labda kuna kitu sijaelewa, ila naona kama vile zimeongezeka.
Hata wakihamia Mombasa... lazima watapita Holili au Namanga na kodi watalipa tu...
Ahsante mkuu kwa report za kitaaluma kuongezea hapo kipindi kama hiki (kuanzia february mwishoni hadi march) berth ya meli hupungua kutokana na wachina wengi wanakua kwenye sherehe za mwaka mpya wao ambazo hufanyika february kila mwaka hivyo husitisha shughuli zao ,na ukitegemea meli nyingi zinazo berth pale hutoka hasa hukoHarbour View Plus
Leo ni tarehe 10 March ambapo ripoti ya bandari Dsm inaonyesha kuwa meli 54 zimewasili kwa mwezi wa 3(wastani wa meli 5 kwa siku) kumbuka leo ni tarehe 10 March.
Mwezi wa 2 ziliwasili meli 190(wastani wa meli 6 kwa siku), January 172(wastani wa meli 6 kwa siku).
Mwaka Jana jumla ya meli 1093 ziliwasili kwa size tofautitofauti toka januari 1 mpaka December 31,2015(wastani wa meli 3 kwa siku)