PIcha hizi zilipigwa mapema na abiria aliyekua angani kwenye ndege baada ya pilot kuspot hiyo meli
Mh jana niliona taarifa ya habari kuwa ilivutwa sasa kama ilianza tena safari leo, watakuwa wamefanya makusudi kabisa .
Tajiri na wahusika wa meli hii ni wazi watakuwa na kesi ya kujibu ya mauaji ya makusudi.
Nimesikia pia, na inasemekana ilikuwa na abiria zaidi ya hao. Hakuna nchi ya ajabu kama Tanzania, tuna laana ya kuchagua chama chenye laana, ajali hizi zinatokea hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kuzuia ajali hizi, na kwa hakika chini ya serikali hii tutakufa kama njugu kama tusipojisalimisha chini ya mwenyenzi MUNGU.
KUMBE MELI YENYEWE ILIKUA MBOVU MBOVU TOKEA ZAMANI.... Soma hiyo iliyotokea tarehe 12/05/2012:
Mv. Seagull yazima moto ikiwa safarini kuelekea Pemba
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 13/05/2012 // Habari // 5 Comments
Salma Said,
ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi.
Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea.
Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine.
Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele alisema Masoud.
Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake.
Awali abiria walisema kuwa katika hekaheka na upepo mkali meli ilipoteza muelekeo na kuelekea upande wa Tanga, kabla ya mafundi kufanikiwa kutengeneza.
Safari ya meli hiyo ilianza baada ya matengenezo yalichukua muda wa zaidi ya masaa mawili majini na kutarajiwa kufika bandari ya zanzibar ambapo ilitarajiwa ifike saa 10 jioni.
Hadi tunakwenda mitamboni meli hiyo haijafika zanzibar. Na hakuna taarifa zozote kutoka mamlaka zinazohusika kuhusiana na suala hilo licha ya wananchi kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka hizo. wakizungumza na gazeti hili wananchi mbali mbali wamesema bado serikali haijapata funzo kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali mbaya iloiyotokea mwaka jana ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
wamesema ni jambo la kushangaza kwa serikali iliyo makini kushindwa kutafuta usafiri wa uhakika na badala yake kuwaacha wananchi wake wakitumia usafiri usio na uhakika jambo ambalo wananchi wengi wanasafiria boti hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda ndege.
Ingekuwa tuna ndege basi tungekuwa tunasafiri kwa ndege maana usafiri wa baharini imeshakuwa ni kifo sasa lakini kwa kuwa sisi ni masikini hatuna budi kucheza bahati nasimu na maisha yetu kwa sababu ndio usafiri wa watu wanyonge tutafanya nini? alihoji Haji Hamadi Mkaazi wa Mwembetanga Unguja.
Hii ni mara ya nne katiak kipindi cha wiki moja kutokea misukosuko kama hiyo inayohusu meli hiyo hiyo ya Seagul na Sea Express ambapo wananchi wamekuwa na khofu ya usafiri wa Unguja na Pemba kutokana na meli nyingi zinzofanya safari za visiwa hivyo kutokuwa na uhakika wa usalama majini.
Milango ya saa sita na nusu mchana wa leo, palitokea a freak storm, upepo usio wa kawaida kabisa ulioambatana na vumbi hapa jijini Dar es salaam.Nilisikia ktk TV, kabla ya tukio hili, kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitoa hadhari khs hali ya hewa ya leo, lkn cha ajabu hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuzuia vyombo vya majini kusafiri au kwenda kufanya shughuli nyingine baharini, km uvuvi.
Mkuu Mv Seagual ndiyo imezama leo na Mv Karama ilizima juzi usiku mbona imetangazwa na ITV jana.
mara mv seagul mara mv karama....ni meli ipi hasa imezama?
Mkuu kwa nini unasema hii ni breaking news wakati huna taarifa kamili???? Subiri ukishakuwa na taarifa kamili ndo uanzishe uzi.
aisee kumbe kuna nyingine ilipiga mzinga juzi!!!....basi bwana..
Ni ya abiria au mizigo?