Meli kubwa za mafuta supertankers zaelekea marekani kuchukua mafuta

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,716
29,071
Mzuka wanajamvi,

Baada ya Opec ikiongozwa na kushinikizwa na Russia na Saudi Arabia kupunguza uzalishaji wa mafuta ili bei ipande. Upepo umebadilika. Sasa hivi Marekani wameamua kuachia mafuta yao kuyauza kwa wingi kwenye soko la dunia.

Meli kubwa za mafuta 48 supertankers ziko njiani baharini kuelekea marekani kuchukua mafuta na kusambaza kwenye soko la dunia.

Hii number ni rekodi. Sasa hivi marekani wanazalisha mapipa million 4 kwa siku kutoka laki moja.

Na imewavutia sana makampuni ya meli za mafuta na kuanza kuelekea marekani kwani ni faida kwako.

Uchumi wa Marekani sasa hivi unazidi kukua zaidi na zaidi baada ya inflation ukilinganisha kama tarehe hizi mwaka jana.

Soma zaidi kwa Kiingereza.

Cc Proved zitto junior T14 Armata
 
Makampuni ya mafuta ya Marekani kina Conoco, Chevron na ExxonMobil huwa yanafanya timing ya bei ya mafuta soko la dunia. Marekani ndio pekee inatumia fracking technology kuchimba mafuta, teknolojia ngumu na ya gharama ila inaifanya Marekani isife njaa kirahisi ikitokea nchi zimesusa kuiuzia mafuta.

Sasa wakiona mafuta duniani yamepanda na wakizalisha kwa fracking watafika breakeven na kupata faida hata kama kidogo huwa wanazalisha. Na wakifanya hivyo wanafanya bei ya mafuta soko la dunia kushuka kiasi hivyo OPEC+ wanaitikia wanazalisha kwa wingi kufikia mahitaji ya bajeti ya nchi zao. Na hapo OPEC+ wanayatia hasara makampuni ya Marekani sababu mafuta yanashuka bei na gharama za Mmarekani hazirudi.

Ila US haiwezi zalisha kwa muda mrefu ndio maana hupendelea kununua. Hakuna haja ya kutumia gharama kubwa kuchimba wakati nchi kama Saudi Arabia ni kitendo cha kubadili flow mapipa kadhaa yakatoka. Nchi za OPEC zikiamua zizalishe kadri ya kila mmoja anavyoweza bongo tutanunua lita kwa elfu moja. Iran ndio ilikuwa inajitoa ufahamu inapump mafuta mengi. Hapa wanachofanya OPEC+ ni kuchezea supply na demand.

US hawana shida na kuuza mafuta. Wanatumia mapipa milioni 19 au 20 kwa siku na hata wakinunua yote hayo ni sawa endapo bei ya soko inaridhisha kwao. Mwenye mgahawa hatishiki na kushuka kwa bei ya mkaa hata kama ana viroba kiasi kwake, anatishika na kupande kwa bei.

Marekani ni mojawapo ya nchi zenye rasilimali nyingi sema wanajua kuzitumia. Wasiojua hudhani Marekani inategemea biashara na uzalishaji pekee. Mfano California ilijengwa kwa uchimbaji wa dhahabu na sasa dhahabu hamna ila Cali ikisimama yenyewe duniani inashindana kwa GDP na Urusi nzima. Sisi subiri dhahabu ya Shinyanga iishe uone njaa itakavyotawala maeneo yale.
 
Mkuu nakisheshimu sana kichwa chako uko vzr nakufuatilia kwa ukaribu mno
 
Back
Top Bottom