Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?

Most media ambazo ziliikosoa serikali either zilifungiwa, kutishiwa au kuundiwa kesi
Mkuu Luse, not necessarily, japo ukosoaji unahitaji kufanywa na manguli wenye weledi wa hali ya juu mfano Ukisema Tumpinge Magufuli ni Dikiteta kwa sababu tuu amezuia mikutano ya kisiasa, utaitwa mchochezi. Lakini ukisema kuwa Magufuli ni Dikiteta, ukaonyesha vifungu vya katiba vilivyotoa haki ya kukutana, ukaonyesha jinsi Magufuli alivyovunja Katiba, ukaonyesha mipaka ya mamlaka ya rais kuwa hana mamlaka ya kwenye kinyume cha katiba, kisha ukauliza alipopiga marufuku mikutano ya siasa alitumia mamlaka gani na kumalizia kuelekeza hatua za kumchukulia rais pale anapovunja katiba, amini usiamini Magufuli angeifuta kauli yake na media ingekuwa very safe, ndio maana sisi wengine tulisupport UKUTA but conditionally.
Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA ... - JamiiForums
Paskali
 

Unachokizungumza kuhusu TBC ni mambo ambayo tungetarajia iyatende kwa umma, lakini imegeuka ni chombo cha chama fulani na serekali na sio umma. Waandishi wa habari nao ugumu wa maisha umewageuza mateka wa tumbo.
 
tulikuwa tunakutegemea wewe ila na wewe ukamezwa maana ulivyokuwa unamtetea bashite utadhani ulikuwa nae uko koromije.......................

inshort ni hakuna ata mmoja wote njaa na uwoga vimewajaa
 

Ha ha ha
 
Unlee otherwise tundu lisu atakuwa anawasumbua mahakamani kila siku
 
Ukitaka strong media tumchukue /lisu/lema/zito/lijualikali/halima mdee/ tuwapeleka journalism institute ndipo tathnia ya habari itabadilika
 
Unachokizungumza kuhusu TBC ni mambo ambayo tungetarajia iyatende kwa umma, lakini imegeuka ni chombo cha chama fulani na serekali na sio umma. Waandishi wa habari nao ugumu wa maisha umewageuza mateka wa tumbo.
TBC inapoitete serikari na chama kilichopo madarakani si ndiyo hivyo kuwatetea wananchi? Serikali ni nini? wapo kwa ajili gani? so kama TBC haiweza kusimamia misingi ya upinzani kwa kuwa upinzani unaipinga serikali na serikali inafanya kazi ya kuwatumikia wananchi... iacheni TBC ifanye kazi yake ya kuelimisha umma.
 
Mkuu Tony Antony, kwanza asante kukubali kuwa hizo strong media zipo na hao strong brave journalists pia wapo tatizo ni tumbo. Unaweza kunifafanulia unamanisha nini? .
Paskali
 

Hamna tofauti ya haki ya binadamu inayotegemea na rangi ya ngozi!

Aidha nchi ina demokrasia au haina!

There is no such thing as "African" and "non-African" democratic system.

Basic Human Rights is a UNIVERSAL right, as declared by the United Nations.

Get your facts straight, please.
 

Pascal Mayalla Shukrani sana nimesoma uzi ulioambatanisha kwa umakini sana. Kukwambia kiukweli nimehamasika na mtazamo na maono yako. Ila kuna kitu nigusie na kukufungua macho kupitia michango ya wanabodi kweye uzi ule.

Kaka yangu Paskali unachoona wewe sicho ninachoona mimi au kuna nichoona mimi na nitamani niwe wewe. Kutafuta muongozo kwenye mijadala hususani humu niwe muwazi ni kupoteza muda kwa sababu hatuko sawa.

Wakati Nokia imetawala soko la dunia Steve Jobs aliwaambia watu wake wa karibu kuwa "nakwenda kutengeneza simu so sexy kiasi watu watalamba buttons zake" na akapingwa lakini hakukata tamaa akaendelea na leo Apple Phone iko wapi???

Ukitaka kufanya mambo makubwa dont ask "the average" watakukatisha tamaa, wewe ndiye mwenye maono hivyo usiulize ushauri wa mtu wanonaje maono yako ila uliza utafikaje kule unakoona?

Usisubiri 2020 anza sasa, kwanini nasema hivyo sababu ulishawahi kuamka asubuhi ukasema sitatoa gari yangu mpaka taa zote ziwe za kijani barabarani?

Utasema resources zinakukwamisha ila unashindwa kutambua kuwa wewe ni resourceful tayari na kama hujui kuna watu wanatamani wawe wewe. Kuna watu wako tayari kufanya kazi na wewe na unataka muongozo nitakushika mkono kaka na utashangaa watavyokugombania.

Kama utaanzisha hicho kipindi kwa maslahi ya taifa utatoboa sababu ni kipindi endelevu ila hivyo tisa vingine vina time limit na hicho cha siri ya mafanikio watanzania wengi kitafanana na kipindi kama Mkasi na Vingine.

Start simple but aim Big Brother utatoboa, mfano Sporah Show started from a back room show to main stream media. Tafuta vitabu na naweza kusema be like Jeremy Pax wa tanzania in your own way unaweza Paskali. Miaka ya nyuma M.M. Mwanakijiji alikuwa na podcast zake sijui ziliishia wapi lakini kama angepata mwongozo angekuwa mbali sana.

Stop procrastinating do it now Paskali, this is your time, its a very exiting time kwa Tanzania ya leo Paskali.

N.B: Nimeandika kwa haraka sababu napeleka familia sehemu ila nitarudi hapa
 
Hii nchi ambayo Polisi wanamuua mwandishi wa Habari kwa kumpiga Bomu hadharani, Vipi mwandishi akikamatwa kwa uficho jiulize atafanywa nini?
Mkuu Bujibuji kiukweli hili tukio la kifo cha Daudi Mwangosi kiliniumiza sana hadi niliamua kuachana kabisa na hii fani ya uandishi ila kitu kikishakuwa kwenye damu kukiacha ni vigumu sana.
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!
Ni kufuatia matukio kama haya, ndio kumepelekea sheria mpya kulazimisha media kuwawekea bima ya maisha waandishi wake. Haya ni baadhi ya mambo mazuri ya sheria mpya ya Habari.

Paskali
 
Kama Strong media zenyewe ni Clouds Fm ndio iikosoe serikali basi tumeumia
Mkuu Kitumbotala, moja ya sifa kubwa ya strong media, ni zile media zinazojiendesha kwa funds kutoka vyanzo vingine ambazo hazitegemei matangazo. Clouds media sio tuu inategemea matangazo bali inajua kuzipanga vizuri na kuzicheza vizuri karata zake na mkono unaokulisha, ila kiukweli Clouds TV inafanya kazi nzuri zaidi ya ukosoaji kuliko TV nyingine yoyote kupitia kipindi chake cha 360 degrees

Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma Ujumbe Gani kwa TV yake ya TBC?!.

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa Uchochezi, Adai Rais Magufuli ni...

Pascal
 
Makala zangu kuhusu wivu wenu dhidi ya mafanikio ya Makonda ni baadhi tuu ya my pieces of literature, kama huna uwezo wa kusoma "in between the lines, you just have completely missed the point.

Pole.

Paskali

Ni Wivu gani huo juu ya alichonacho Makonda unaouzungumzia? Huyo disgraced RC Makonda ana kitu gani wanachokosa wengine hadi watu wamwonee wivu unaoupigia jaramba?
Yaani hapo ndipo unapojiingiza katika kundi la brown envelope journalists aka wachumia tumbo.
Jaribu kutafari maneno 3 katika fani ya uandishi
1. Integrity
2. Credibility
3. Objectivity

Ukiyazingatia hayo matatu yakuongoze utafanikiwa katika fani yako
Obrigado!
 
Waandishi wengi ni njaa kali na elimu za kuunga unga.
Mkuu Prishaz, japo kuna kaukweli katika hili, ila pia kuna waandishi wa aina 3.
1. Waandishi walioingia kwenye uandishi baada ya kufeli masomo, sifa za kuingia uandishi hata DIV IV ya points 31. Hivyo wameingia ili kujiokoa tuu. Hawa elimu zao ni za kuunga unga.

2. Waandishi wenye vipaji ambao wana vipaji hata kama amepata division 0 anakuwa mwandishi. Hawa elimu zao ni za kuunga unga ila wanategemea vipaji vyao.

3. Waandishi ambao wako vizuri academically wamefanya vizuri darasani na wameingia uandishi by choice for the love of it. Hawa hawana elimu ya kuungaunga.

Hivyo sio waandishi wote ni vilaza na elimu ya kuungaunga. Kuna waandishi vichwa wa ukweli.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…