SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,130
- 7,901
Baada ya mechi ya Medeama vs Yanga kumekuwa na kelele nyingi kuhusu goli la clear offside la Kibabage, ila wengi walifumbia macho matukio kadhaa ambayo refa alimezea ambayo yangewapa faida Medeama.
Kuna uzi mmoja nilisema kitendo ambacho baadhi ya watu wanasema kilistahili kadi nyekundu kilitokana na rafu kadhaa ambazo wachezaji wa Yanga walicheza dhidi ya wachezaji wa Medeama ambazo refa hakuziita. Kwa maana hiyo kile kitendo kilikuwa cha hasira ndiyo maana ukiangalia hata reaction ya wachezaji wa Yanga hawakuwa wameshangazwa kihiivyooo maana walijua ambacho walikuwa na wenyewe wamekifanya mara kadhaa kabla ya hapo.
Kwenye interview moja baada ya ile mechi, mshambuliaji wa Medeama, Jonathan Sowah akilalamika kwamba alikuwa alichezewa rafu nyingi na mbaya na mabeki wa Yanga na kwamba walinyimwa penati 3 za wazi. Na wote tulioangalia mpira tunajua alichosema ni kweli kabisa.
Ushauri wangu, Yanga wakirudia kutaka tena kucheza mpira wa nguvu na rafu katika mechi ya marudiano, utawagharimu sana. Najua mna mchezaji mmoja au wawili tu wakikosekana katika timu hamna timu tena ya ushindani.