SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,136
- 7,903
Wengi mmejikuta mnaangalia hatma ya Yanga kwa kuangalia tu mechi mbili za Yanga dhidi ya CRB na ile ya mwisho dhidi ya Al Ahly. Hakuna ambaye amewaza ni jinsi gani Medeama anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga.
Ukweli ni kuwa Yanga ni ngumu sana kuvuka kwa kucheza mechi zake pekee maana kama ambavyo tumejadili sana inahitaji amfunge CRB kwa tofauti ya goli 4 jambo ambalo ni gumu sana ingawa kwenye mpira lolote linaweza kutokea. Ikipata ushindi tofauti na huo Yanga inahitaji kupata angalau sare dhidi ya Al Ahly jambo ambalo nalo lina ugumu fulani.
Njia iliyo rahisi zaidi kwa Yanga ni kwa Yanga kumfunga CRB kwa ushindi wowote ule huku wakiombea Medeama ipate ushindi leo dhidi ya Al Ahly. Medeama ana nafasi kubwa ya kushinda leo kwa sababu Al Ahly bado hawako vizuri na wataendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kutokana na majeraha. Vilevile changamoto za hitilafu za ndege yao na uchovu wa safari unaweza ukawaathiri kwa kiasi fulani Al Ahly.
Matokeo ya mechi hizo mbili yakienda kama nilivyosema, kitakachobaki ni katika mechi za mwisho kwa Yanga kuiombea Medeama itoe sare dhidi ya CRB huku yenyewe haihitaji kupata sare wala ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Al Ahly.
Kwenye head to head, Yanga ina faida mbele ya Medeama kwa hiyo ikitokea wamelingana points, Yanga anafuzu.