Medard Kalemani alikuwa Mkurugenzi wa sheria Wizara ya Madini, Mikataba ilipita kwake, anaponaje?

Aisee Yaani mruma alikuwa shushushu wa rasilimali zetu enzi za kikwete????
Hii mbona kama inaleta ukakasi hivi??
hii imeniacha hoi kuwa aliulizwa kuwa kwanini ulisaini ati alisaini bila kusoma na akaingiza nchi kwenye hasara kubwa halafu anapewa hongera daah
 
hii imeniacha hoi kuwa aliulizwa kuwa kwanini ulisaini ati alisaini bila kusoma na akaingiza nchi kwenye hasara kubwa halafu anapewa hongera daah
Ajabu kabisa.....na huyu Mruma asingesaini kabla MKATABA haujapitiwa na kuandaliwa na mkurugenzi wa sheria bwana kalemani ambaye sasa ni naibu waziri nishati na madini
 
Magufuli ni mnafiki wa hali ya juu! Bado Wakolomije hataki kabisa kuwagusa pamoja na maovu tao katika nyadhifa zao. Na kauli yake FAKE "Niacheni niinyooshe nchi"

Mwana MFALME.

NCHI YA WANAFKI
 
Magufuli ni mnafiki wa hali ya juu! Bado Wakolomije hataki kabisa kuwagusa pamoja na maovu tao katika nyadhifa zao. Na kauli yake FAKE "Niacheni niinyooshe nchi"
Nchi inaenda kama gari bovu
 
Najiuliza hili swali...

Huyu mtu ni kama "anarukwarukwa" katika tuhuma hizi za Wizara ya nishati na Madini

Mkurugenzi wa sheria ndiye "mpishi wa mikataba na mshauri mkuu wa waziri na katibu mkuu" katika masuala ya sheria

Akichemka Waziri au Katibu mkuu katika masuala ya sheria, maana yake mkurugenzi wa sheria wa wizara haponi na moja kwa moja anaonyesha hafai kwa kuwa anawapotosha wakuu wake

Namshauri Kalemani ajiondoe mwenyewe katika nafasi yake, mambo yanayosumbua taifa (mikataba ya Madini) ilipita na kuandikwa mezani kwake!

Kubaki kwake Wizarani kwa hali yoyote anaweza kuingilia uchunguzi ili ajilinde, kumbuka huyu ni NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI
Mkuu uwe unaandika kulingana na kamati ilivyotoa majibu yake ,kuweka habar ambayo haikuwa kwenye taarifa juwa kuwa ni mchochezi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,
Niliwahi kujiuliza maswali mengi kuhusu Medard Kalemani-Mbunge wa jimbo la Chato na Naibu, Waziri nishati na Madini. Dr. Medard Kalemani kabla ya nafasi aliyonayo hivi sasa, alikuwa mwanasheria mkuu katika hiyo hiyo ya Nishati na Madini. Hii ina maana kwamba wakati wizara hiyo ikiongozwa na mawaziri kadhaa waliopita ( William Njeleja, Sospeter Muhongo) na ambao wametajwa kwenye ripoti mbili za makinikia pamoja na ripoti za Almasi na ile ya Tanzanite, huyu bwana alikuwa mshauri mkuu wa wizara katika masuala ya sheria. Kwa mantiki hiyo ameshiriki na kushauri mikataba yote ya madini ambayo imegundulika kuwa mibovu na haina maslahi ya taifa.

Sasa kinachoshangaza ni huyu baba kujifanya watu wanaomfahamu hawajui aliyoyafanya wakati akiwa mtumishi wa umma. Busara ndogo tu ingemshauri ajiuzulu kabla mambo hayajamfikia. Nadhani anafikiria Mkulu atamteua au kumpandisha cheo kuwa waziri kamili. Jambo analosahau ni kwamba mkulu anaona huyu baba atakuwa chanzo cha kusakamwa na balaa kila siku.

Kujiondoa serikalini kutamuongezea heshima zaidi kuliko kusubiri mpaka mambo yamfikie. Ajipime na aangalie kama bado anastahili kuwa kiongozi ndani ya serikali ya Magufuli.

Leo tumeona mpaka raisi anwaambia wakae kando watu waliotajwa kwenye ripoti ya almasi na Tanzanite.

Hivi hawa mawaziri hawajioni wenyewe kuwa wamepoteza sifa zo uongozi?

Watanzania tujifunze ustaarabu wa kujipima wenyewe.
 
Back
Top Bottom