Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Nadhani ifike mahali tukubali kama taifa kuwa tulijikwaa pakubwa (tulikosea sana) kumuondoa Mhe. Dkt. Medard Kalemani MB toka kwenye Baraza la Mawaziri na Wizara ya Nishati.
Hali tuliyo nayo ya nishati ya umeme Tz ni wazi kuwa hatuwezi kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi tu ya uwekezaji mdogo mdogo wa wanyonge.
Ukitathmini tija ya Mhe. Dkt. Kalemani, ya Mhe. January Makamba na ya Mhe. Dkt. Dotto Biteko NWM unaweza kujuwa uamue nini kwa maslahi ya taifa.
Ni wazi utagundua kwamba rekodi ya Mhe. Dkt. Kalemani MB inamsemea bila kuhitaji msaada.
Mhe. David Cameron waziri mkuu mstaafu amerudi kwenye Baraza la Mawaziri la Mhe. Rishi Sunak (PM) akiwa kama Waziri wa Mambo ya Nje.
Mhe. Vladmir Putin aliwahi kuwa waziri, rais, waziri mkuu, rais tena.
Mhe. Dkt. Medard Kalemani MB ni nani kulinganisha na Putin na Cameron hadi tupate shida kumrejesha nishati!?
Tutakapogundua kwamba kumbe tunahitaji zaidi umeme kwa maendeleo ya taifa badala ya kuhitaji mbwembwe za teuzi zisizo makini tutakuwa tumesalimisha taifa.