nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,613
ni wa nyumbani...
Game overWakuu,
Niliwahi kujiuliza maswali mengi kuhusu Medard Kalemani-Mbunge wa jimbo la Chato na Naibu, Waziri nishati na Madini. Dr. Medard Kalemani kabla ya nafasi aliyonayo hivi sasa, alikuwa mwanasheria mkuu katika hiyo hiyo ya Nishati na Madini. Hii ina maana kwamba wakati wizara hiyo ikiongozwa na mawaziri kadhaa waliopita ( William Njeleja, Sospeter Muhongo) na ambao wametajwa kwenye ripoti mbili za makinikia pamoja na ripoti za Almasi na ile ya Tanzanite, huyu bwana alikuwa mshauri mkuu wa wizara katika masuala ya sheria. Kwa mantiki hiyo ameshiriki na kushauri mikataba yote ya madini ambayo imegundulika kuwa mibovu na haina maslahi ya taifa.
Sasa kinachoshangaza ni huyu baba kujifanya watu wanaomfahamu hawajui aliyoyafanya wakati akiwa mtumishi wa umma. Busara ndogo tu ingemshauri ajiuzulu kabla mambo hayajamfikia. Nadhani anafikiria Mkulu atamteua au kumpandisha cheo kuwa waziri kamili. Jambo analosahau ni kwamba mkulu anaona huyu baba atakuwa chanzo cha kusakamwa na balaa kila siku.
Kujiondoa serikalini kutamuongezea heshima zaidi kuliko kusubiri mpaka mambo yamfikie. Ajipime na aangalie kama bado anastahili kuwa kiongozi ndani ya serikali ya Magufuli.
Leo tumeona mpaka raisi anwaambia wakae kando watu waliotajwa kwenye ripoti ya almasi na Tanzanite.
Hivi hawa mawaziri hawajioni wenyewe kuwa wamepoteza sifa zo uongozi?
Watanzania tujifunze ustaarabu wa kujipima wenyewe.
Mi sijui Mkuu....?Unajua maana ya WA KUNYUMBA ?
Kwanini hakujizulu,hawa ni watu hatari sana,ndumila kuwili.Mbona ripoti imeanisha kabisa wao ndio waliomshauri waziri asisaini lakini waziri akasaini,sasa kosa lake lipo wapi kutoa ushauri wa kutokusaini kwa kuwa kampuni haijulikani ama vipi?
Nyani Haoni..........!Hili jipu liko usoni mkuu
Mbona ripoti imeanisha kabisa wao ndio waliomshauri waziri asisaini lakini waziri akasaini,sasa kosa lake lipo wapi kutoa ushauri wa kutokusaini kwa kuwa kampuni haijulikani ama vipi?
Hivi mnajua kazi ya kitengo kweli ninyi,mengine mwachieni Rais,he is in control.Mnataka mkaange mpaka pilipili hoho,nyanya na vitunguu?Najiuliza hili swali...
Huyu mtu ni kama "anarukwarukwa" katika tuhuma hizi za Wizara ya nishati na Madini
Mkurugenzi wa sheria ndiye "mpishi wa mikataba na mshauri mkuu wa waziri na katibu mkuu" katika masuala ya sheria
Akichemka Waziri au Katibu mkuu katika masuala ya sheria, maana yake mkurugenzi wa sheria wa wizara haponi na moja kwa moja anaonyesha hafai kwa kuwa anawapotosha wakuu wake
Namshauri Kalemani ajiondoe mwenyewe katika nafasi yake, mambo yanayosumbua taifa (mikataba ya Madini) ilipita na kuandikwa mezani kwake!
Kubaki kwake Wizarani kwa hali yoyote anaweza kuingilia uchunguzi ili ajilinde, kumbuka huyu ni NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI
Mtoto Akililia Wembe...........!Hivi mnajua kazi ya kitengo kweli ninyi,mengine mwachieni Rais,he is in control.Mnataka mkaange mpaka pilipili hoho,nyanya na vitunguu?