Medard Kalemani alikuwa Mkurugenzi wa sheria Wizara ya Madini, Mikataba ilipita kwake, anaponaje?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,983
20,634
Najiuliza hili swali...

Huyu mtu ni kama "anarukwarukwa" katika tuhuma hizi za Wizara ya nishati na Madini

Mkurugenzi wa sheria ndiye "mpishi wa mikataba na mshauri mkuu wa waziri na katibu mkuu" katika masuala ya sheria

Akichemka Waziri au Katibu mkuu katika masuala ya sheria, maana yake mkurugenzi wa sheria wa wizara haponi na moja kwa moja anaonyesha hafai kwa kuwa anawapotosha wakuu wake

Namshauri Kalemani ajiondoe mwenyewe katika nafasi yake, mambo yanayosumbua taifa (mikataba ya Madini) ilipita na kuandikwa mezani kwake!

Kubaki kwake Wizarani kwa hali yoyote anaweza kuingilia uchunguzi ili ajilinde, kumbuka huyu ni NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI
 
Najiuliza hili swali naomba mods Uzi huu wauache kwa kubalansi stories

Huyu mtu ni kama "anarukwarukwa" katika tuhuma hizi za Wizara ya nishati na Madini

Mkurugenzi wa sheria ndiye "mpishi wa mikataba na mshauri mkuu wa waziri na katibu mkuu" katika masuala ya sheria..........................................
mkuu tunachezeshwa ukuti ukuti tu hapa
 
Najiuliza hili swali naomba mods Uzi huu wauache kwa kubalansi stories

Huyu mtu ni kama "anarukwarukwa" katika tuhuma hizi za Wizara ya nishati na Madini

Mkurugenzi wa sheria ndiye "mpishi wa mikataba na mshauri mkuu wa waziri na katibu mkuu" katika masuala ya sheria...................................................

Huku ni kumuonea tuu, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe, na kila mtu na bahati yake ya home boy wake.

P.
 
Back
Top Bottom