MECCO Ipo ama ilikufa?

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
15,030
10,558
Jamani nimekuwa nikitatizwa na swali hili. Kuna kampuni moja ya kizalendo iliyojulikana kama "Mwananchi Engineering and Construction Company" (MECCO). Hivi kampuni hii bado ipo ama ilikufa kama zilivyokufa nyingine?

Walikuwa wakijishughulisha sana na ujenzi wa majengo na madaraja na walishawahi kuwa na timu ya mpira wa miguu miaka ya mwishoni mwa themanini. nakumbuka walijenga jengo la benki kuu kule mkoani Mbeya miaka hiyo.

Kama kuna mwenye taarifa nitafurahi sana kuzipata.
 
MECCO kama haijafa ipo njiani kufa, kama mashirika yote ya Umma, tumeyala tumeyamaliza. Yaliyosalia, wakija wenye kuweza kuyaendesha tunalalamika, tunawaita wezi. Looh, hata sijuwi tuna-kaungonjwa gani?
 
kifo cha MECCO kinasikitisha sana............

Kama kweli imekufa, basi ni sikitiko kubwa sana, kwani hii ilikuwa ni kampuni ya wazalendo kabisa na iliyokuwa makini sana na kazi zake.
What about NEDCO? Na yenyeqwe ilikufa ama?
 
Makampuni mengi yalishajifia na kuzikwa, mengine kubinafsishwa!

Mimi nasikitika na kiwanda cha baiskeli pale mwenge, serikali ilikibinafsisha kwa AVON nao wakamuuzia/wakabinafsisha kwa shellys.

Hivi serikali ikibinasisha inabaikiwa na share? au ndio 100%.

Na vile vifaa vyetu vilivyopelekwa S.Africa kutoka KIA serikali imeshavirudisha? au bado wanachunguza?
 
Idimi,
MECCO bado ipo, bado imesajiliwa na CRB (Contractor's Registraion Board), ila imebinafsishwa kwa jamaa mmoja (ana asili ya Somalia) kwa kiasi kikubwa. Serikali ina hisa ndogo sana kwa sasa. Pia baadhi ya wafanyakazi wa zamani wana hisa chache.
Hivi sasa wanashindana kupata kazi kama makampuni mengine ila naona wanapata kazi ambazo si kubwa sana.
MECCO sio shirika la umma tena.
 
Kama kweli imekufa, basi ni sikitiko kubwa sana, kwani hii ilikuwa ni kampuni ya wazalendo kabisa na iliyokuwa makini sana na kazi zake.
What about NEDCO? Na yenyeqwe ilikufa ama?
NEDCO bado ipo inafanya kazi za kihandisi, ila nadhani si shirika la umma kabisa.
 
Nashukuru kwa Ufafanuzi Bw Roy, kidogo nimepata mwanga.
 
Back
Top Bottom