fyddell
JF-Expert Member
- Dec 19, 2011
- 12,682
- 23,992
shukrani kudoo,kwakwel ni mtihani kwa miguu ya kukuRIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.
NA; BAHATI K MWAMBA.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA.
Ukapita ukimya mfupi, kisha Miguu ya Kuku alipata sauti kwa mara ya kwanza tangu aingie pale ndani.
“Sasa hiyo ni nyongeza au ni kazi nyingine?” Aliuliza huku akiwa anamtizama Rich'one.
“Nayo ni kazi pia.” Rich alijibu.
“Kama ni kazi ina maana nayo itakuwa na malipo tofauti pia”
“Hilo la malipo tulishalijadili hapa na tayari tunajua namna ya kukulipa kwenye hizo kazi mbili.”
“Mimi huwa malipo yangu hayajadiliwi nikiwa sipo, malipo yanajadiliwa nikiwepo na lazima mlipe kiasi ninachohitaji” Alisema Miguu ya Kuku kwa kujiamini, huku akiwaacha Boys among men wakitazamana.
“Aah,nadhani hata majadiliano yetu hayakuwa mabaya bwana Zuki”Alfa aliingilia kwa utulivu, lakini Zuki alimkatisha.
“Huwa naishi kwa misingi na kanuni zangu ambazo, kamwe sijawahi kwenda tofauti na zinavotaka na moja ya kanuni inasema:- ‘Kamwe sitapokea malipo yaliojadiliwa bila kushirikishwa'. Hiyo ni kanuni namba kumi, kati ya kanuni kumi nambili za kazi yangu. Hivyo kifupi sitaki kusikia malipo mlioyajadili, tujadili upya” Zuki Gadu p.a.k Miguu ya Kuku alizidi kushikilia msimamo wake.
Boys among men walitazamana kwa mshangao. Walikuwa wamekutana na mtu mwenye msimamo wake ambao kamwe, hauyumbi.
“Ok! Tujadili malipo kama unavyohitaji” Rich'one aliamua kurahisisha ule ubishani uliotokea.
“Hapo kila kichwa kimoja ni milioni mia” Miguu ya Kuku alisema.
“Hahaa!” Omega alicheka kibabe, kisha aliendelea..
“…Ndiyo maana tulikwambia tumeshajadili malipo yako, si unaona bado unaingia kwenye hesabu zetu!”
“Hesabu zenu zilitaka nichukue milioni mia kwa kila kichwa, ikiwa na maana kuwa mlipanga kunipa milioni mia sita?” Miguu ya Kuku aliuliza kwa upole.
“Hakika kabisa. Milioni mia sita keshi bwana mdogo” Omega alizidi kusititiza.
“Hiyo si bei yangu ndugu zangu”
“Haaa!!” Wazee walishangaa kwa pamoja.
“Ndiyo, kila kichwa ni milioni mia, lakini hapo ni kabla sijaanza kazi. Nikianza kazi na kuifanikisha vema, kila kichwa kitaongezeka bonusi ya milioni ishirini hivyo kila kichwa mtanipa milioni mia moja na ishirini na, kwa ujumla milioni mia saba ishirini.” Miguu ya Kuku alitua maelezo yake.
“Aah wapi! Pesa nyingi sana hiyo, haiwezekani aisee” Rich'one alibwata kwa hasira, huku akisimama na kuilegeza tai yake.
“Milioni mia saba ishirini! Duh, pesa kubwa sana hiyo kijana” Alfa nae aliongeza kushangaa ukubwa wa dau lililotajwa.
“I'm not cheap guys, sifanyi kazi za mia mia kama muuza karanga, nafanya kazi ya pesa kubwa kubwa tu na kama hamuwezi kunipa hiyo pesa, tafuteni mwingine. Wapo wanafanya kazi ya hata milioni ishirini wazee” Miguu ya Kuku aliendelea kuwapa maelezo yenye kujipa uthamani wa kazi yake.
“Sasa wa milioni thelathini ataweza nini?” Omega alimuuliza.
“Sasa kama huhitaji kufanyiwa kazi na majambazi, kubali kulipa pesa ya kutosha ili mamluki kama mimi, wafanye kazi yako. Tofauti na hapo agiza majambazi ya kuiba bank, yakufanyie kazi yako huko Kongo.” Miguu ya Kuku aliendelea kuwapasha.
“Ni kanuni namba tano ya kazi yangu, ambayo inanitaka kila nikua mtu, ninunue gari la bei kubwa na nibaki na pesa ya kula maisha, sasa jiulize kwa hiyo pesa nitanunua gari na kubaki na kiasi gani. Naisimamia kanuni namba tano wakubwa” Aliongeza tena.
Wazee walichoka, kila mmoja alijikuna kichwa kwa utaratibu wake. Lakini kabla mafikirio yao hayajahitimishwa, waliongezwa moto mwingine ili wajikune vizuri mvi zao.
“Na mlisema kuna kuiba viboksi viwili.” Miguu ya Kuku alinyamaza kidogo na kuwatizama wale wazee, ambao walikaa kimya tena kumsikiliza anataka kuongeza jambo gani.
Akaendelea na alilokusudia kulisema..
“Hiyo nayo ni kazi kama kazi nyingine, inaweza kubeba uhai wa mtu asiyehusika, ili mradi nipate kinachotakiwa. Mtaweka mezani milioni mia mbili, jumla itakuwa milioni mia tisa ishirini” Alitua.
“Aaah wapi weweee!! Yaani billioni kasoro senti kadhaa! Aah wewee, si utatufilisi sasa.” Omega alikuja juu huku akiwa ametoa macho, mithili ya mzee aliyesikia, korona ipo kwenye mipapai yake.
“Huwa sifanyi kazi na wabishi na huwa silegezi kamba na sishushi wala kupandisha, maana siuzi nepi mimi” Miguu ya Kuku aliongea huku akisimama kwa nia ya kuondoka, kisha akawageukia…
“Mkumbuke bado nawadai milioni kadhaa za mkoba mweusi, malizieni hizo pesa leo hii. Sitaki ifike saa kumi sijanunua pikipiki na ikifika saa kumi hamjanilipa, nitakuja kuwadai gharama nyingine mlionitumia bila kunambia. Mlinifanya Jana nimuue Kiuno cha nyoka bila malipo. Mkichelewa, nitawadai pesa yake, pia nitawadai pesa ya kuwarahisishia kumuua Tembe za chai mbele yangu. Mi naondoka” Miguu ya kuku aliunguruma kizembe, huku akiweka sawa suti yake na kuanza kupiga hatua za kuiacha ofisi ile ya madini.
Miguu ya Kuku hufanya kazi kwa sheria zake, na hayumbi hata kidogo. Kujiamini ikiwa ni silaha yake kubwa, kufanikisha mambo yake.
****
Alipotoka nje ya ofisi, Boys among men walianza kubishana wao wenyewe, huku kila mmoja akisema lake kuhusu kilichotokea.
“Huyu jamaa anadharau sana aisee, yaani anatamka pesa utadhani ni mizizi ya korosho kwamba, ukienda kusini utaiapata!” Omega'one aliunguruma kwa hasira huku akiwa ameshika nyonga zake.
“Ina maana kazi yake ina bei kubwa sana kuliko mamluki wengi hapa Afrika? Rich'one aliuliza kwa hamaki.
“Wapo professional killer’s kuliko yeye bwana, wala asitutishe. Tuanze kumsaka sasa hivi na aingie kazini” Omega aliunguruma huku akishika simu yake kubwa na ya kisasa.
“Nadhani bado tunamhitaji sana Miguu ya Kuku, kuliko muuaji mwingine yeyote hapa Afrika. Miguu ya Kuku sio rahisi kama tulivyodhani ni, wa bei mbaya lakini anaweza kuifanya kazi yake kwa usahihi mkubwa, bila kutetereka.” Alfa aliwaeleza wenzake.
“Unajua tatizo siyo ubora wake tuliouona, tatizo ni gharama zake. Haiwezekani mtu atake billion moja kasoro senti kadhaa, kuua na na kuiba mzigo hapo Congo.” Omega alizidi kushikilia msimamo wake.
“Hakuna namna, ni lazima tumtumie yeye kufanikisha hili jambo” Alfa nae aloendelea kusisitiza.
“Kwa hiyo upo tayari tumpe hizo pesa?” Rich aliuliza.
“Hakika nipo tayari apewe hizo pesa na ikibidi apewe zaidi ili ifike billion moja”
“Unakengeuka sasa!”
“Sikengeuki ndugu zangu. Hivi vile viboksi akivipata vina thamani gani ya chini kabisa?”
“Pesa nyingi sana, zaidi ya billioni mia nne hivi!”
“Kama viboksi pekee ni zaidi ya billioni mia nne, ni vipi tushindwe kumpa Billioni moja kwenye kazi mbili zenye thamani mara dufu kwetu?”
Ukimya ukapita, huku wakifikiria kile ambacho mwenzao alikuwa amewauliza.
“Tusiwe na mikono ya birika wakati ambao tunahitaji mafanikio. Toa pesa, upate pesa zaidi. Kikubwa tuombe afanikiwe kuwaangusha hao jamaa.” Alfa alizidi kuwapanga wenzake.
“Lakini unaweza kuwa sahihi bwana” Rich alijibu kinyonge.
“Ok! Apewe hizo pesa.” Omega alijibu kishingo upande.
Harakaharaka Alfa aliinyakua simu yake, kisha alimpigia Miguu ya Kuku.
“Naomba urudi tuzungumze bwana” Alfa alianza kuongea, baada ya simu yake kupokelewa.
“Huwa sirudi nilikotoka na huwa siongelei kwenye simu kuhusu uhai wa mtu. Najua unajua ni vipi unaweza kuwasiliana na mimi. Ukishindwa kabisa, weka pesa kwenye akaunti mi niende Goma kuhenyeka” Miguu ya Kuku alimjibu na kukata simu, bila kusubiri zaidi.
Alfa alishusha simu yake na kuwatazama wenzake, kisha akawambia..
“Tufanye malipo kutoka kwenye akaunti yetu ya umoja, kisha tusubiri majibu kutokea Goma nchini Congo.”
“Kwa hiyo bado anataka pesa hiyo hiyo?” Omega aliuliza.
“Mi naona tumuongezee zaidi, pesa itarudi na tutamtumia kwenye kazi zetu daima”
“Huyu hayawani anabei sana, tukizidi kufanya nae kazi ipo siku atatufilisi”
“Atafanya kazi zile ngumu tu, nyingine tutafanya wenyewe ama tutawapa wenye saizi na hizo kazi”
Boys among men walikubaliana kumpa hizo pesa na bila kuchelewa, walifanya taratibu zote za malipo na kuweka pesa kwenye akaunti ya Miguu ya kuku.
Walipomaliza kila hatua, walikubaliana kukutana baada ya Miguu ya kuku kukamilisha kazi waliomtuma. Kila mmoja alichukua uelekeo wake na kuendelea na majukumu yake na kazi iliachwa kwa Zuki Gadu p.a.k Miguu ya Kuku. Mtu mrefu na mwenye miguu myembamba.
*****
Miguu ya kuku aliwasili nyumbani kwake ikiwa ni majira ya saa mbili na nusu usiku. Siku nzima aliimalizia kwenye mizunguko yake ya hapa na pale, huku jambo kubwa likiwa ni kushugulikia tiketi ya ndege, kuelekea nchini Rwanda. Alitaka safari yake ianzie nchini Rwanda na si Congo moja kwa moja na, alikuwa na sababu zake za kufanya hivyo.
Alipoingia ndani, jambo la kwanza kwake, ilikuwa ni kuingia kwenye chumba cha mazoezi. Huko alitumia saa zima, kisha aliingia maliwatoni na kujiswafi. Alipohakikisha mwili wake upo alivyotaka, alielekea jikoni ambapo alianza kuandaa chakula cha usiku. Alihakikisha amepika chakula ambacho kingelitosheleza utumbo wake. Alipika kilo moja na nusu ya ubwabwa na kuku mzima wa kienyeji. Alipakua na kuelekea sebuleni kula.
Alitumia dakika thelathini kula na alipohakikisha ameshiba vile atakavyo, alifuata chupa ya maji ya kunywa na kunywa lita moja na nusu.
Aliweka chupa ya maji pembeni huku akibeua kwa shibe. Alikusanya vyombo vyake na kuelekea jikoni kwa mara nyingine. Alipofika jikoni alikusanya vyombo vyote vichafu na kuanza kuviosha huku akipiga mluzi usioeleweka. Alipohakikisha vyombo vimetakata, alifungua kabati na kuvihifadhi vizuri kwa kuwa alitarajia kumaliza muda mrefu, akiwa mbali na nyumba yake.
Miguu ya kuku alielekea chumbani kwake, ambapo alichukua kompyuta yake mpakato na kuiwasha. Ilipowaka alianza kazi ambayo ilimfanya aiwashe kompyuta ile.
Alianza kuingiza jina la Papaa Deo kwenye kompyuta yake na, majibu yaliokuja, yalimshangaza tofauti na alivyotarajia.
Wasifu wa Papaa Deo ulikuwa ni wasifu wenye kutia woga. Ulikuwa ni wasifu ambao ulimgandisha kwa sekunde kadhaa.
Papaa Deo alikuwa ni Brigedia Jenerali wa jeshi la Congo, huku akiwa ni kiongozi wa kambi ya jeshi ya Katindo(camp military de Katindo) iliyoko katikati ya mji wa Goma. Mbali ya kuwa mwanajeshi wa vyeo vya juu kabisa; pia alikuwa ni mtu mwenye ushawishi ndani ya mji wa Goma, akiwa ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa ambao walipewa heshima kwenye mji huo ulioko kwenye mkoa wa Kivu ya kaskazini. Ukiwa ni mji ambao ulidumu kwenye vita kwa muda mrefu na baadae, ukageuka kuwa mji wa biashara muda mfupi, tangu kumalizika kwa vita kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23, ambao walifurumushwa kwa asilimia kubwa na jeshi la Tanzania, kwenye operesheni maalumu, iliyoenda kwa jina la BEHIND THE RED SHARKS.
Papaa Deo aliheshimika sana ndani ya Goma.
Mbali na wasifu wote huo, pia alikuwa ni mtu anaelindwa kuliko hata rais wa Congo. Alikuwa analindwa na walinzi binafsi na walinzi wa serikali, huku akiwa na magari mengi ambayo hayapitishi risasi.
“Kwa nini huyu mtu anaulinzi mkubwa namna hii!” Aliwaza huku akipalaza kicharazio akiwa na lengo la kumsoma zaidi mwamba yule wa Goma.
Alikuwa anatafuta kujua kama anafamilia au la na, alipofanikiwa kujua alibaki akiwaza huku macho yake yakiwa kodo kwenye kompyuta yake.
Papaa Deo hakuwa na mke, lakini alikuwa na mtoto mmoja wa kike na kimada mmoja, ambae alimfanya kama mke wake.
Mwanae alikuwa ni mfanyakazi kwenye uwanja wa ndege wa Goma, akiwa kama mkurugenzi wa uhamiaji uwanjani pale.
Miguu ya kuku alihisi ipo sababu ya binti yule kufanya kazi kwenye uwanja ule wa ndege.
Kimada wa Papaa Deo alikuwa ni mmliki wa hoteli ya La Paix, hoteli ambayo iko kilomita chache kutoka ilipo kambi ya jeshi ya Katindo.
Baada ya kumfahamu Papaa Deo kwa kifupi, alizitafuta picha za wapendwa wake ambao ni binti yake na kimada wake. Alipozipata alibaki akizitizama bila kupepesa.
Wote walikuwa ni warembo haswaa, ambao walionekana kuwa na asili ya kabila Wahutu.
Wakati alipokuwa akiwatizama, wazo moja lilikuwa kichwani mwake ya kuwa; wale ndiyo udhaifu wa Brigedia jenerali Deo. Aliamini alitakiwa kuanza na udhaifu ule ili kumpata Deo mwenyewe na kabla ya kumpata, alitaka kuiba kwanza mzigo ulioko kwenye nyumba ya Papaa Deo, nyumba inayolindwa kuliko nyumba zote ndani ya mji wa Goma.
“If a bullet can’t take you, will take some one you love soldier!.” Alisema huku akiufunga ukurasa wenye picha za Papaa Deo na vipenzi vyake.
Mwili ukamcheka, ubongo ukamcheza huku akifikiria namna ya kuiingia familia ile isiyoingilika kirahisi.
Mtihani!!
.
.
.
.
.
ENDELEA KUWA NAMI
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

Mkwe wa papaa deoMIGUU YA KUKU ANAKWENDA KUPATA JIKO.
MAANA NJIA YA KUPATA VIBOX NI KUWA MWANA FAMILIA.