Mdunguaji wa Goma

Mdunguaji wa Goma

RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SEHEMU YA KUMI NA MBILI.

Baada ya kumfahamu Papaa Deo kwa kifupi, alizitafuta picha za wapendwa wake ambao ni binti yake na kimada wake. Alipozipata alibaki akizitizama bila kupepesa.

Wote walikuwa ni warembo haswaa, ambao walionekana kuwa na asili ya kabila Wahutu.

Wakati alipokuwa akiwatizama, wazo moja lilikuwa kichwani mwake ya kuwa; wale ndiyo udhaifu wa Brigedia jenerali Deo. Aliamini alitakiwa kuanza na udhaifu ule ili kumpata Deo mwenyewe na kabla ya kumpata, alitaka kuiba kwanza mzigo ulioko kwenye nyumba ya Papaa Deo, nyumba inayolindwa kuliko nyumba zote ndani ya mji wa Goma.

“If a bullet can’t take you, will take some one you love soldier!.” Alisema huku akiufunga ukurasa wenye picha za Papaa Deo na vipenzi vyake.

Mwili ukamcheka, ubongo ukamcheza huku akifikiria namna ya kuiingia familia ile isiyoingilika kirahisi.

Mtihani!!

Alikuna kichwa kwa kufikiria mambo kadhaa, huku akijaribu kuwaza njia bira ya kutumia ili afanikishe mpango wake wa kwanza, ambao aliupa jina la KOMOA BWEGE.

Kila njia aliyoifikiria aliona haifai kutumika na, aliposhindwa kabisa kupata njia sahihi, aliamua kuachana na familia ile na, aliingia kwenye awamu nyingine ya kuwajua wahusika wengine ambao alitakiwa kuwashugulikia.

Jina la pili aliliandika kwenye kompyuta yake, kisha alisubiri kwa sekunde kadhaa na kuletewa majibu aliyoyataka.
Fredi Mutesa alikuwa ni mwanajeshi pia, ambae alikuwa na cheo cha Brigedia na alifanya kazi kwenye kambi ndogo, kwenye mpaka wa Rwanda na Goma. Wasifu wake haukuwa mrefu sana na kila alipojaribu kutafuta taarifa zaidi, alijikuta akiishia nusu ya vile alivyotaka.

Swai Makambo lilikuwa ni jina la tatu kulifanyia kazi ambapo, alikutana na wasifu uliomfanya atulie kwa umakini na kusoma taratibu sana.
Swai Makambo alikuwa ni mganga mkuu kwenye hospitali ya Dei Hospital. Hospitali kubwa kuliko zote kwenye mkoa wa Kivu ya kaskazini. Lakini kabla hajawa kwenye hiyo hospital, alikuwa ni mmoja wa matabibu wa jeshi, ambao walikuwa mstari wa mbele kuwatibu majeruhi wa vita. Lakini pia, alikuwa anaimiliki hiyo hospital kwa asilimia themanini, huku asilimia zilizosalia zikiwa zinamilikiwa na watu wengine.

Dokta Swai alikuwa na mke na mtoto mmoja ambae alikuwa ni mgonjwa wa mtindio wa ubongo na, mtoto yule alikuwa akipatiwa matibabu nyumbani, chini ya matabibu wenye uzoefu huku akiwalipa pesa nyingi ili, kumsaidia mwanae.

Jina la nne lilikuwa ni la Tatu Banenga. Huyu alikuwa ni mwanamke ambae alifanya kazi ofisi ya waziri mkuu, akiwa kama mkurugenzi wa usalama. Alipozidi kumfuatilia kwenye picha mbalimbali, aligundua ni mlinzi pia wa waziri mkuu japo alionekana mara chache kuwa nyuma yake.
Jina la tano lilikuwa ni la Jimmy Kasoki. Huyu alikuwa ni kanali mstaafu ambae amegeukia biashara za madini. Jimmy ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa ndani ya mji wa Goma, akiwa anamiliki migodi kadhaa ya dhahabu na almasi. Pia alikuwa anamiliki maduka makubwa ya nguo na majumba kadhaa ya kifahari. Alikuwa na ulinzi wake binafsi huku akiwa na gari kadhaa, ambao haziingizi risasi.

Leti Kamirimana lilikuwa ni jina la mwisho kwenye orodha. Huyu alikuwa ni mwanasiasa, japo nae aliwahi kuwa mwanajeshi mwenye cheo cha kanali.

Miguu ya kuku alifunga ukurasa wa Leti Kamarimana, kisha aliegemea kwenye sofa na kuzama mawazoni. Aliwaza namna ya kufanya kazi akiwa ugenini na namna ambavyo angeliweza kuondoka, bila kuingia kwenye vyombo vya dola.

Mji wa Goma haukuwa mgeni kwake, alifahamu maeneo mengi na alifahamu vituo vingi vya polisi na kambi za jeshi. Licha ya kufahamu yote hayo, lakini hakuwa akijua vichochoro vya msaada endapo mambo yangelikuwa magumu kwake.

Aliirudia tena kompyuta yake na kuanza kuitafuta ramani ya mji wa Goma. Mji ambao unawakazi chini ya laki tatu, ukiwa ni mji ambao unatambelewa na mvua kuanzia mwezi wa nne, hadi mwezi wa sita.

Alitabasamu baada ya kujua machache kuhusu mji huo wa kibiashara. Alitabasamu kwa kuwa alipata kazi mwezi wa nne, kuelekea mwezi wa tano. Ikiwa na maana kwamba, kilikuwa ni kipindi cha mvua kwenye wilaya ya Goma. Kwake mvua ilikuwa ni sehemu sahihi kufanyia kazi, aliamini hekaheka katikati ya mvua ni nusu ya ushindi.
Alichukua karatasi na kalamu na kuyaandika majina ya watu wote, aliotakiwa kuwashugulikia. Alipomaliza kuyaandika, alianza kupitia wasifu wa kila mmoja na kwa umakini mkubwa bila kuacha, kitu chochote ambacho kilikuwa na umuhimu kwake.

Kila alipopitia wasifu wao, alikuwa anaandika pembeni namna ya kuanza kushugulika na kila mmoja wao. Lakini licha ya kuandika baadhi ya mbinu, alishindwa kujua ataanza na yupi na kumaliza na yupi.
Aliamua kurudia tena kuwasoma mmoja mmoja na maeneo ya makazi yake, hadi anamaliza tayari alikuwa amepata wa kuanza nae na hapo alijipongeza kwa kuanzia safari yake, nchini Rwanda.

Mtu wa kwanza aliyemwekea alama alikuwa ni Bregedia Fredi Mutesa, ambae alikuwa anaongoza kikosi cha jeshi kilichokuwa mpakani mwa Rwanda na Goma, sehemu iliyoitwa Gisenyi.

Alimchagua wa kwanza kwa sababu, alikuwa mpakani na wengine wote walikuwa katikati ya mji. Aliona ni vema kuanzia mpakani, ili endapo akimaliza kazi yake katikati ya mji, iwe rahisi kuondoka, kuliko angelianzia mjini pengine asingeliweza kupata nafasi ya kupitia mpakani na kumalizia kazi. Chaguo la kwanza kwake lilikuwa ni sahihi.

Alifunga kompyuta yake na kuelekea chumbani kwake. Huko alichukua begi lake dogo la mgongoni na kulifuta vumbi, kisha alichukua nguo chache na kuziweka kwenye begi. Nguo alizochukua ni zile ambazo aliamini ni sahihi kwake kuzitumia wakati wowote. Hakuchukua silaha yoyote, hakutaka kuweka mashaka kwa mtu yeyote huko aendako.
Alichagua viatu aina ya buti, zenye ufanano na buti za jeshi. Alipomaliza kuandaa kila kitu, alifunga begi lake na kuingia kulala, huku akitarajia kuamka alfajiri ili kuwahi uwanja wa ndege, kwa ajili ya safari kuelekea Kampala, kisha ataunganisha kuelekea Kigali Rwanda.

****

Kigali, Rwanda..

Ndege ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali, ikiwa ni saa sita kasoro dakika kumi, mchana. Abiria walishuka mmoja mmoja na kufuata taratibu za kawaida, kisha waliruhusiwa kuondoka kila mmoja kuelekea aendako.

Miongoni mwa abiria hao, alikuwa ni Zuki Gadu p.a.k Miguu ya Kuku. Alifuata taratibu za ukaguzi, kisha alitoka nje ya uwanja baada ya kukamilisha taratibu zote bila kikwazo. Alipofika nje ya uwanja, alikutana na madereva taxi wengi, ambao walimlaki kwa uchangamfu, huku kila mmoja akinadi huduma yenye ubora kwa mteja wake.
Macho yake yaliokuwa yakitembea kama ya kinyonga, yalivutiwa na kijana mmoja mtanashati ambae alikuwa akijitahidi, kumuita kwa ishara bila kutoa sauti.

Alivutiwa na tabia za vijana wengi kuwa wachangamfu na si wachoyo wa taarifa, tofauti na wale wa umri mkubwa ambao mara nyingi huongozwa na hekima na usiri, kwa kuwa kwenye kazi ya usafirishaji, wamekutana na mengi ambayo huwapa funzo.

Alimfuata yule kijana na kuingia kwenye gari yake. Punde baada ya kuingia, kijana yule nae aliingia huku akitabasamu kwa amani.

“Wapi boss wangu!” Aliuliza kijana yule.

“Naelekea Gisenyi.” Miguu ya kuku alijibu.

“Gisenyi!!” Alishangaa kijana yule huku akigeuka kumtazama.

“Ndiyo Gisenyi, kwani kuna shida kuelekea huko?”
“Hapana, lakini wewe ni Mtanzania”

“Umejuaje mimi ni Mtanzania?”

“Lafudhi yako kaka.”

“Kwa nini unahofia utanzania wangu huko mpakani?”

“Huko kwa siku za hivi karubuni, kumekuwa na taarifa mbaya kuhusu vijana wa kitanzania. Nasikia wamekuwa wakipotea kwenye mazingira tata na kukutwa wakiwa wamefariki, hivyo imekuwa ni hatari kwa watanzania kupitia pale kuingia Goma”

“Kwa nini sasa inatokea hivyo?”

“Hakuna mwenye taarifa sahihi, lakini nasikia kuna mtu pale mpakani anaitwa Zibuabanda. Huyo jamaa ni kamanda wa kikosi kazi kutoka Congo, ambae anahusika kwenye ulinzi wa mpaka huo na, alitolewa kwenye jeshi la waasi wa M23, baada ya kuwa amejisalimisha kisha wakamwajiri jeshini. Sasa Zibuabanda analipiza kisasi kwa kuwa husema, jeshi la Tanzania ndilo lilowafurumusha waasi wenzake.”
“Duh! Hii ni hatari sasa…. Kwa nini viongozi hawakemei hili jambo?”

“Kwa kweli hakuna anaejua, pengine hakuna mtu ambae ameshatoa taarifa”

“Kwa hiyo huwa mnawashauri nini hao vijana?”

“Huwa tunawaomba watumie usafiri wa anga kuliko usafiri wa gari.”

“Duh!”

“Eeh, kwa hiyo ndugu yangu ni bora urudi uwanjani, utumie usafiri wa ndege hadi Goma. Ni dakika kumi au kumi na tano utakuwa umefika Goma”

“Ningeliweza kufuata ushauri wako lakini, inanilazimu kutumia mpaka wa Gisenyi, kwa kuwa kuna biashara fulani inabidi niifanye huko.”

“Duh! Haya bwana. Itabidi ulipe dola ishirini na tano”

“Hapana, naomba unipeleke kwa dola ishirini”

“Sawa” Dereva aliwasha gari na safari ya kuelekea Gisenyi ilianza,huku Miguu ya kuku akijilaza na kupitiwa na usingizi.

“Braza nikuache mpakani, au utataka twende hadi Goma?” Kijana alimstua kwa swali.

“Wewe si umesema huwa kunaogopesha huko? Mbona wataka kunisindikiza kabisa?”

“Aah.. Naweza kuwa msaada kwako nikikupitisha, kwa sababu mimi Mtutsi hivyo ubaya wowote kwangu, utaamsha vuguvugu mpakani. Kwa hiyo wanaogopa kutudhuru pia ni Watutsi wenzengu.”

“Hapana! Siku huwa hazifanani na sitaki kukuingiza matatizoni”

“Mh! Sawa bwana mkubwa” Kijana alijibu huku akiendelea kuongeza kasi ya gari lake.

****

Saa tatu baadae, walikuwa wanaingia wilayani Gisenyi karibu na mpaka wa Rwanda na Congo.

“Tumefika kaka mkubwa” Kijana alimuamsha Miguu ya kuku.

Miguu ya kuku aliamka na kuangaza huku na huko, kisha akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa dola ishirini na, kumpa yule kijana. Kisha alipiga hatua na kuelekea sehemu ya ukaguzi huku akipokea kheri ya safari, kutoka kwa dereva aliyemfikisha pale.

Alivuta hatua zake kama mlevi, huku akijaribu kuangaza huku na huko. Kwa harakaharaka aliweza kuwaona wanajeshi wa Rwanda wakiwa na silaha zao, wakidumisha usalama upande wao. Kulikuwa na maofisa kadhaa wa uhamiaji na wale wa polisi, ambao nao walikuwa pembeni ya ofisi za ukaguzi.

Alipiga hatua na kuelekea upande wa wapita kwa miguu, huko alipanga foleni na kusubiri zamu yake ifike akaguliwe. Alijiamini kwa kuwa alikuwa anafuata taratibu bila kukwepa.

Zamu yake ilifika na alikaguliwa na kuulizwa maswali machache, kisha Hati zake za kusafiria zilipigwa mhuri na aliruhusiwa kuingia upande wa pili, ambao ni Goma, Congo.

--- 2----

Goma, Congo…

Miguu ya kuku aliweka vema begi lake mgongoni, kisha alianza kupiga hatua kuelekea upande ambao kulikuwa na daladala, ambazo zilikuwa zinafanya safari zake kutoka Goma hadi Gisenyi, lakini hazikuruhusiwa kuingia Rwanda.

Alipiga hatua zake kivivu huku akishuhudia baadhi ya gari zikiondoka kuelekea Goma. Aliifikia gari ambayo ilikuwa inajiandaa kuondoka, alipanda na safari ilianza. Abiria wenzake walikuwa ni watu wenye kuongea lugha moja, na yeye pekee ndiye hakuelewa kilichokuwa kinazungumzwa.

Alikaa kimya na kuanza kuhesabu miti iliyokuwa inarudi nyuma kwa kasi.

Baada ya dakika kumi za safari yao, gari ilianza kupunguza mwendo na alipojaribu kutizama mbele, aliona kizuizi na wanajeshi wakiwa na silaha za moto.

“Jamani abiria wageni wekeni karatasi zenu karibu.” Dereva alipaza sauti kuwambia abiria wake.

Taarifa ile iliyotolewa, ilifanya watu wote wamtazame Miguu ya kuku, nae bila kujiuliza, alijua yeye ndiye mgeni na wenzake ni wenyeji. Lakini ni kwa vile aliamua kujipa jibu la kwa nini anatizamwa, lakini kama angeliwauliza, wangelimpa jibu tofauti na alilokuwa akiwaza.

Wao walimtizama kwa kuwa walijua pale ni mwisho wa safari yake, walijua kwa sababu walishajua anatokea nchi gani na walijua mbele yao, kulikuwa na vijana wa Zibuabanda.

Yes, Zibuabanda asiyewapenda watanzania
.
.
.
.
.
ENDELEA KUWA NAMI
Hii hatari hii,
Miguu ya Kuku nakuaminiaa

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
MUENDELEZO MDUNFUAJI WA GOMA

Baada ya raiabwotevkwenye gari kuendelea kumtolea macho miguu ya kuku aka mzee baba mivuu ya kuku akawa ashasoma nyuso zao.Akawa anaendelea kutabasam bila kutoa chochote.Manake alijua vijana wa zuba sio watu wazur ni manyangau. Vijana walifika mpaka pale wakakagua gari bila kujua kuna mgeni kule gari ikaruhusiwa kupita bila kikwazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
(

Kwa hiyo akabatasamu kwa kitutsi wakajua ni mwenzao bangi hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SEHEMU YA KUMI NA TATU.

Baada ya dakika kumi za safari yao, gari ilianza kupunguza mwendo na alipojaribu kutizama mbele, aliona kizuizi na wanajeshi wakiwa na silaha za moto.

“Jamani abiria wageni wekeni karatasi zenu karibu.” Dereva alipaza sauti kuwambia abiria wake.

Taarifa ile iliyotolewa, ilifanya watu wote wamtazame Miguu ya kuku, nae bila kujiuliza, alijua yeye ndiye mgeni na wenzake ni wenyeji. Lakini ni kwa vile aliamua kujipa jibu la kwa nini anatizamwa, lakini kama angeliwauliza, wangelimpa jibu tofauti na alilokuwa akiwaza.

Wao walimtizama kwa kuwa walijua pale ni mwisho wa safari yake, walijua kwa sababu walishajua anatokea nchi gani na walijua mbele yao, kulikuwa na vijana wa Zibuabanda.

Yes, Zibuabanda asiyewapenda watanzania.

Foleni ya magari ilizidi kusogea taratibu, huku baadhi ya watu wakitolewa kwenye magari na kuwekwa pembeni, kisha magari waliokuwemo yakiruhusiwa kuendelea na safari.

Gari alilopanda Miguu ya kuku lilifikiwa, kisha lilizungukwa na wanajeshi watatu ambao walikuwa na silaha mikononi mwao. Mwanajeshi mmoja aliyekuwa na cheo cha Sajenti, alilisogelea gari lile, huku nyuma yake kukiwa na wanajeshi wengine wawili wakimpa ulinzi.

Mwanajeshi yule aliamuru milango ifunguliwe na abiria wageni watoe nyaraka zao. Wenyeji walibaki kimya kwenye gari, huku mgeni pekee akihangaika kufungua begi lake, ili atoe nyaraka za kusafiria.

“Naomba utoke na nyaraka zako bwana mkubwa” Sajenti alimwambia kwa lugha ya kifaransa.

Miguu ya kuku alishuka huku akiwa ameshika Hati za kusafiria, ambazo zilimruhusu kuingia nchini Congo. Sajenti alizichukua na kuzitizama.

“Wewe ni Mtanzania!?” Sajenti aliuliza.

“Ndiyo ni Mtanzania”
“Goma unaenda kufanya nini?”

“Mimi ni mfanyabiashara wa nguo na naenda kutafuta soko la nguo”

“Lakini inaonekana si mara yako ya kwanza kuja Goma. Je, kipindi hicho hukuona hilo soko?”

“Kipindi hicho nilikuja kufungua duka langu la simu.”

“Ulifungulia mtaa gani?”

“Mtaa wa Nduguwatwana, karibu na kanisa la CBCA Katoyi.”

“Sawa! Lakini matajiri wenzio huwa wanatumia usafiri wa ndege, kwa nini wewe unatumia magari?”

“Nilikuwa na shughuli fulani hapo Gisenyi, hivyo niliona bora nitumie usafiri wa gari.”

“Sawa bwana mdogo, lakini itabidi ulale chini ya uangalizi kwa siku ya leo, kisha kesho utaendelea na safari yako”

“Lakini sijavunja sheria yoyote, huoni kama huko ni kunipotezea muda bila sababu?”

“Hakuna namna, inabidi utii sheria bila shuruti.”

“Sheria nimetii na ndiyo sababu nimepita hapa nikiwa na kila kitu kinachohitajika”

“Bahati mbaya Sajini Kipepeo huwa sibishani na watu” Aliongea Sajini ambae alijiita kipepeo, huku akipiga hatua kuondoka.

Miguu ya kuku alishangaa akidakwa kwa nyuma, kisha alifungwa pingu harakaharaka bila kupenda. Alishindwa cha kufanya kwa sababu hakuwa ametegemea kufanyiwa vile na wanajeshi wale, japo alikuwa na tahadhari ila si ya tukio lile.

Alivutwa kuelekea kwenye karandinga ya jeshi, aina ya Iveco12 ambayo ilikuwa na wanajeshi wengine ndani yake.
Alipokelewa jujuu kama mwizi wa dagaa mwaloni, kisha aliamuliwa kukaa kitako ndani ya gari ile ya jeshi. Harakaharaka aliwahesabu wanajeshi waliokuwa pale ndani na, idadi yao ilikuwa ni sita. Mbali ya wanajeshi hao, kulikuwemo watu wengine wawili ambao nao walikuwa wamefungwa pingu.

“Poleni” Aliamua kuwambia wale wahanga wenzake, ambao aliwakuta ndani ya gari chini ya ulinzi.

“Pole na wewe” Alijibiwa kwa kiswahili kilichonyooka, kumaanisha walikuwa ni Watanzania wote.

“Na…” Kabla hajamalizia kauli yake, alitandikwa konde zito usoni, ambalo lilimpeleka chini bila kutarajia.

“Ukiwa chini ya ulinzi, hutakiwi kuzungumza” Mwanajeshi aliyemuadhibu alimkoromea huku akiweka bunduki yake sawa, kwa hatua itakayofuata endapo ingelihitajika.

Miguu ya kuku alijizoazoa na kuamka huku akimtizama mwanajeshi yule, alimkariri bila kusema neno.

Dakika chache baadae, Sajenti Kipepeo alipanda kwenye gari na kuamuru iondolewe, huku Miguu ya kuku na wenzake wakifunikwa nyuso zao.

Kwa Miguu ya Kuku ilikuwa ni sawa na kumfunika mtu mdomo asipumue, huku akiachiwa pua wazi. Kwake ni heri angelifunikwa masikio na kumuacha akiwa anatizama. Masikio yake yalisikia na kila kitu na kuhifadhi kumbukumbu bila kusahau. Hivyo masikio yake yalikuwa wazi kufuatilia mwenendo wa safari yao, alikariri kila uchochoro walioupita. Hivyo alijua wameelekea upande gani na wametumia muda gani na wamechepuka njia ngapi.

Walisafiri zaidi ya dakika thelathini kisha gari ilisimama na wakaamriwa kushuka. Walishuka na kufunuliwa vitambaa nyusoni mwao. Macho yao yalikutana na nyumba nzuri ambayo ilionekana kulindwa sana, kulikuwa na wanajeshi zaidi ya saba ambao walikuwa na silaha za moto mikononi mwao.

Miguu ya kuku na wenzake, waliingizwa ndani ya nyumba ile na kupelekwa kwenye chumba kimoja ambacho kilijaa giza nene, huku kukiwa na harufu mbaya ya uvundo.

Walimriwa kukaa chini, kisha taa zikawashwa na mwanga ukasambaa chumba kizima. Macho yao yalikutana na damu mbichi zilizokuwa zimetapakaa ukutani, huku chini kukiwa na vidole vya watu ama kucha zikiwa mbali na vidole na, haileweki watu wenye vile viungo walikuwa wapi kwa wakati huo.

Wale jamaa wawili walianza kulia kwa woga, miili yao ilikuwa imejawa na ubaridi wa kutisha.

“Punguzeni hofu, tumuombe Mungu atutoe hapa salama” Miguu ya kuku aliwambia wenzake, huku yeye akijaribu kukichunguza kile chumba kwa umakini usio tia shaka. Kwa harakaharaka aliweza kuona meza na kiti kimoja, ambavyo alijua vilitumika kuwaweka mateka wakati wa mahojiano. Kulikuwa na kidirisha kidigo upande wa kulia wa kile chumba. Macho yake yaliwaona walinzi wawili waliokuwa mle ndani, walikuwa wamebeba silaha zao wakiwa na umakini usioyumba.

Wakati akiendelea kukikagua kile chumba, mlango ulifunguliwa na aliingia Sajenti Kipepeo akiwa ameongozana na wanajeshi wawili, ambao walikuwa wamebeba sanduku la chuma.

“Hapa kuna maswali machache mnatakiwa kuyajibu, mwenye kuyajibu vema ataruhusiwa kuendelea na safari yake.” Sajenti Kipepeo alisema huku akimfuata jamaa mmoja aliyekuwa chini akitetemeka.
Alimnyanyua na kumpeleka kwenye kiti na kumkaliza.
Alitoa picha mbili na kumuonesha yule jamaa.

“ Hawa jamaa unawajua?” Kipepeo aliuliza.
Yule jamaa alichukua sekunde kadhaa kuzitizama zile picha, kisha aliinua uso wake na kujibu..

“Hapana siwafahamu kabisa”

“Wewe ni Mtanzania kweli?”

“Ndiyo ni Mtanzania, lakini siishi Tanzania kwa muda mrefu sasa.”

“Ooh, vizuri sana. Sasa wewe nadhani hufai kuhojiwa hapa.” Kipepeo alisema na kumpa ishara kijana wake mmoja, ambae alimchukua yule jamaa na kuondoka nae nje ya kile chumba.

Baada ya kusalia wawili, Sajenti Kipepeo alimwinua mwingine na kumkalisha kwenye kiti, kisha alimwonesha zile picha.
Yule jamaa alizitizama kwa sekunde chache na jibu lake likawa, hawafahamu wale watu walioko kwenye zile picha.

“Makazi yako ni wapi?” Kipepeo alihoji.

“Tanzania…” Jamaa alijibu.
“Kwa nini huwajui hawa jamaa na upo nao nchi moja?”

“Pengine siishi nao mkoa mmoja, ama kulingana na watu wengi nchini ni vigumu kuwatanbua watu wote”

“Upo mkoa gani?”

“Makazi yangu ni Mwanza”

“Sawa, tunakuhamishia sehemu ya pili” Alisema Kipepeo huku akimpa ishara kijana mwingine na, yule jamaa nae aliondolewa kwenye kile chumba.
Kipepeo alibaki na Miguu ya Kuku kwenye kile chumba, huku kukiwa na vijana wengine wawili wakiwa kimya kabisa.

Kipepeo alimfuata na kumuinua, kisha alimkalisha kwenye kiti na kumuonesha zile picha. Miguu ya kuku alizitizama kwa sekunde chache na kuinua uso wake, kisha akasema..

“Nawafahamu”

Kipepeo alibaki akiwa ameganda kama aliyeingizwa kijiti cha masikio, alimtizama pasipo kuamini alichokisikia..

.
.
.
.
. ENDELEA KUWA NAMI
 
Mkuu hongera kwa utunzi mzuri.

Japo naomba Leo uongeze kipande kingne

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu asanteh
Itapendeza zaidi leo ukitupa viwili!
 
RIWAYA; MDUANGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SEHEMU YA KUMI NA NNE.

Wakati akiendelea kukikagua kile chumba, mlango ulifunguliwa na aliingia Sajenti Kipepeo akiwa ameongozana na wanajeshi wawili, ambao walikuwa wamebeba sanduku la chuma.

“Hapa kuna maswali machache mnatakiwa kuyajibu, mwenye kuyajibu vema ataruhusiwa kuendelea na safari yake.” Sajenti Kipepeo alisema huku akimfuata jamaa mmoja aliyekuwa chini akitetemeka.
Alimnyanyua na kumpeleka kwenye kiti na kumkaliza.
Alitoa picha mbili na kumuonesha yule jamaa.

“ Hawa jamaa unawajua?” Kipepeo aliuliza.
Yule jamaa alichukua sekunde kadhaa kuzitizama zile picha, kisha aliinua uso wake na kujibu..

“Hapana siwafahamu kabisa”

“Wewe ni Mtanzania kweli?”

“Ndiyo ni Mtanzania, lakini siishi Tanzania kwa muda mrefu sasa.”

“Ooh, vizuri sana. Sasa wewe nadhani hufai kuhojiwa hapa.” Kipepeo alisema na kumpa ishara kijana wake mmoja, ambae alimchukua yule jamaa na kuondoka nae nje ya kile chumba.

Baada ya kusalia wawili, Sajenti Kipepeo alimwinua mwingine na kumkalisha kwenye kiti, kisha alimwonesha zile picha.
Yule jamaa alizitizama kwa sekunde chache na jibu lake likawa, hawafahamu wale watu walioko kwenye zile picha.

“Makazi yako ni wapi?” Kipepeo alihoji.

“Tanzania…” Jamaa alijibu.
“Kwa nini huwajui hawa jamaa na upo nao nchi moja?”

“Pengine siishi nao mkoa mmoja, ama kulingana na watu wengi nchini ni vigumu kuwatanbua watu wote”

“Upo mkoa gani?”

“Makazi yangu ni Mwanza”

“Sawa, tunakuhamishia sehemu ya pili” Alisema Kipepeo huku akimpa ishara kijana mwingine na, yule jamaa nae aliondolewa kwenye kile chumba.
Kipepeo alibaki na Miguu ya Kuku kwenye kile chumba, huku kukiwa na vijana wengine wawili wakiwa kimya kabisa.

Kipepeo alimfuata na kumuinua, kisha alimkalisha kwenye kiti na kumuonesha zile picha. Miguu ya kuku alizitizama kwa sekunde chache na kuinua uso wake, kisha akasema..

“Nawafahamu”

Kipepeo alibaki akiwa ameganda kama aliyeingizwa kijiti cha masikio, alimtizama pasipo kuamini alichokisikia..

“Hili sanduku hapa pembeni linazana za kutesea, lakini lisikutishe. Wenzako nimeona wamesema kweli na wameondolewa hapa bila kuguswa, hivyo usiogope.”

“Ni kweli nawafahamu” Miguu ya kuku aliendelea kusisitiza.

“Huu ni mwaka wa nne, hajawahi kutokea mtu akasema anawafahamu hawa jamaa. Hakika leo ni siku njema sana.” Kipepeo aliinuka huku akitabasamu, alimwinua Miguu ya kuku na kuanza kutoka nae nje ya kile chumba kilichokuwa kimejaa damu za watu.

Walitembea korido kadhaa na kuingia kwenye chumba kingine, ambacho kilionekana kuwa kama ofisi. Miguu ya kuku akikalishwa kwenye kiti na kuachwa peke yake pale ofisini.

Kama kawaida, macho yake yalifanya utalii kwenye ile ofisi kwa kasi ya ajabu. Aligundua ofisi ile haikuwa na mpangilio maalumu na bila shaka ilipangwa na mwanaume, kiasi alishindwa kupanga vema ikawa na mwonekano wa kuvutia. Ukutani aliona picha nusu ya mtu ambae alikuwa amevaa gwanda la jeshi. Mtu yule alionekana kuwa na nyota mbili mabegani mwake. Sura ya yule mtu haikuwa ya kuvutia hata kidogo, ilikuwa ni sura yenye kutangaza hatari na ugomvi wakati wote. Akiwa bado anaitafakari picha ile, mlango ulifunguliwa na mwenye picha aliingia.

Alikuwa ni mwanaume mrefu aliyejaa kimazoezi, ngozi nyeusi mithili ya koboko, macho mekundu kupita kiasi, alikuwa na alama ya kukatwa na kitu chenye ncha kali, pembeni kidogo ya jicho lake la kushoto. Mikono yake pia ilikuwa na alama nyingi za kukatwakatwa. Mtu yule alimtizama Miguu ya kuku kwa macho yake makali, huku akienda kukaa kwenye kiti chake na kutazamana na mgeni wake.

“Naitwa kamanda Zibuabanda” Jamaa alijitambulisha.

“Naitwa Zuki Gado”

“Good!” Jamaa alisema huku akipekuapekua makabrasha yalioyokuwa pembeni yake. Alipomaliza kuyapekua aliyatupa pembeni huku mkononi, akiwa na picha moja. Picha ile aliiweka mbele ya Miguu ya kuku.

“Bila shaka ni wewe uliyesema unawafahamu hao jamaa” Zibuabanda alisema.

“Ndiyo, nawafahamu”

“Kwa sasa wanashugulika na nini huko kwenu?”

“Ni wafanyabiashara wakubwa tu”

“Bado wapo jeshini au wametaafu?”
“Bila shaka watakuwa wamestaafu hivi sasa”

“Biashara gani wanafanya hivi sasa?”

“ Wanauza madini”

“ Mara nyingi huwa wako wapi?”

“Arusha na Dar Es laam.”

“Kwa nini unawafahamu sana hawa jamaa?”

“Kwa sababu nafanya nao biashara.”
“Unayafahamu makazi yao?”

“Hapana siyafahamu”

“Good!” Zibuabanda alisema huku akinyanyua simu ya mezani na kupiga sehemu fulani.

“Naomba kuongea na Brigedia tafadhali…. Amekwenda wapi?.... Kwa mkewe yupi wa Mailimbili au Gisenyi?... Mailimbili eeh… sawa akija mwambie tarifa za awali zipo kuhusu mbwa wa Tanzania, mtoa taarifa anaingia hatua inayomhusu….OK.” Zibuabanda aliweka simu chini na kumtazama Miguu ya kuku ambae alikuwa kimya muda wote.

Walitazamana.

“Nashukuru kwa maelezo yako. Sasa itabidi tukusindikize hadi Goma usiku huu” Zibuabanda aliongea huku akitungua koti lake kwenye msumari uliyokuwa umegongwa kwenye kabati la kutunza Nyaraka.

“Nashukuru sana kamanda” Miguu ya kuku alijibu huku akiamini hakukuwa na usalama wowote, hakuona kama kuna nafasi ya kusindikizwa kama alivyoahidiwa.

Zibuabanda alimuongoza kutoka nje ya nyumba ile, huko alikutana na wale jamaa wawili ambao alikuwa nao kwenye chumba cha mahijioano. Waliongozwa kuingia kwenye gari huku kukiwa na ulinzi wa kutosha, askari sita nyuma yao akiwemo Sajenti Kipepeo.

Safari ilianza huku Zibuabanda akiwa amekaa mbele kwa dereva.

Miguu ya kuku bado fikra zake hazikumpa imani kuwa, kuna usalama na kuhitimisha fikra zake, bado mikononi mwao kulikuwa na pingu, kitu pekee kilichokuwa kimebadilika ni kuwa, wakati huu hawakuwa wamefunikwa chochote nyusoni mwao na pengine ni kwa sababu, kulikuwa na giza la saa moja jioni.

Zuki Gado alizungusha macho yake taratibu na kuwatizama walinzi waliokuwa wanalinda, wote walikuwa ni wanajeshi na walikuwa na silaha za moto. Kufungwa pingu kwake halikuwa tatizo, tatizo lilijitokeza alipoanza kuwafikiria wenzake ambao aliamini anahitajika kuwasaidia.
Tofauti na walivyoahidiwa kupelekwa Goma, gari lilikuwa linachukua uelekeo mwingine na lilizidi kuelekea porini zaidi.

Miguu ya kuku aligundua hilo, baada ya kuhisi gari linapita uelekeo tofauti na ule wa awali, waliopita wakati wakienda kwenye nyumba ya mahojiano.

Wasiwasi ulizidi kujijenga moyoni mwake. Wenzake hakuona kama walikuwa wamebahatika kuhisi chochote, kwa sababu walikuwa wakitabasamu kama vile hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea. Nyuso zao zilijawa matumaini makubwa tofauti na alivyowaona awali.

Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, gari ilisimama na harakaharaka wanajeshi watano walishuka, akiwemo Sajenti Kipepeo. Walipofika chini walijadiliana kidogo, kisha waliwaamuru watu wao washuke kwenye gari.

Miguu ya kuku alikuwa wa mwisho kushuka, ambapo aliweza kuwaona wenzake walivyopigwa na butwaa kwa kile walichokiona.
Wanajeshi watano walikuwa wamesimama mstari huku wakiwa wamebeba silaha zao mikononi, japo hawakuonekana kutaka kuzitumia.

Miguu ya kuku alielewa ni kitu gani kilitarajia kufuata, hivyo alihitaji kufanya maamuzi ya haraka kujiokoa, hakutaka kufa kizembe.
Haraka macho yake yalimuona Sajenti Kipepeo akimfuata Zibuabanda upande wa mbele wa gari na, kuwaacha wenzake watano ambao walikuwa wamejipanga mstari, kutoka kushoto kwao kuelekea kulia.

Alipiga hesabu zake haraka kabla mambo hayajaharibika, alijua itawahitaji sekunde kumi hadi kumi na tano; kuziweka silaha zao sawa ili kushambulia. Pia ilingelicbukua sekunde hizohizo kuweza kumtoa Zibuabanda kwenye gari hadi chini, au Kipepeo kurudi na kuwafikia pale walipokuwa.

Yeye ilingelimchukua sekunde sita pekee kuwafikia wale jamaa wenye bunduki, lakini ingelimchukua sekunde thelathini kuweza kuwadhibiti. Aliwatizama wenzake ambao bado walikuwa wamebutwaika na wasijue la kufanya, pori liliwatisha na dhahiri hawakuona usalama mbele yao.

“Mkiona nafanya tukio lolote, hakikisheni mnalala chini haraka iwezekanavyo. Hawa jamaa wanatutoa kafara hapa msituni.” Aliwambia wenzake kwa sauti ndogo ambayo aliamini walimsikia vema kabisa.

Hakutaka kungoja majibu yao, alianza kupiga hatua kuwafuata wale jamaa ambao walikuwa wamejipanga mstari na silaha zao.

Hatua zake ziliwastua na kufanya wamtazame kwa pamoja.

“Simama hapo wewe Kenge” Mmoja alisema huku akipiga hatua kumguata.

Aliyemfuata alikuwa anamrahisishia kazi aliyotarajia kuianza na, ili iwe rahisi zaidi, aliamua kumtia hasira zaidi.

“Kenge mwenyewe!” Alisema kwa sauti na kuwafanya watu wote wamtazame yeye. Kitendo cha kurudishia tusi, kilimpandisha hasira yule mwanajeshi aliyetukana. Alizidi kupiga hatuakubwakubwa ili amfikie Miguu ya kuku na kumuadhibu, lakini hakujua miguu ya kuku alikuwa anamuwazia nini.
Kabla hajafikiwa na yule mwanajeshi mwenye hasira za mkizi, alitanua miguu yake mirefu, kisha akapiga hatua ndefu na kujifyatua akitanguliza miguu yake, ambayo ilienda kutua kifuani kwa yule mwanajeshi. Kabla yule mwanajeshi hajafika chini, tayari miguu ya kuku alikuwa ameshatangulia chini na kumpokea kifuani mwake na kufamnya ngao, ili asipatwe na risasi ambazo zilianza kurindima kumfuata.

Mbali na kumfanya ngao, pia alichomoa bastola iliyokuwa kiunoni mwake na kuishika kwa mikono yake miwili, ambayo ilikuwa imefungwa pamoja kwa pingu.

Kutokea pale chini, aliweza kuwaona vema wale wanajeshi wanne, ambao walikuwa wanashambulia hovyohovyo bila mpangilio kwa kuwa walivurugwa na tukio lile la ghafla.
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa, Miguu ya kuku alitumia bastola mkononi mwake, kuwatungua watu zaidi ya wawili. Shabaha yake haijawahi kukosa kichwa cha mtu, hivyo kila risasi ilitua vema kwenye miili ya wale askari, huku yeye akimsukuma kando askari aliyekuwa kifuani kwake, kisha alibiringita upande na kuzikwepa risasi za mwanajeshi mmoja aliyekuwa amesalia, baada ya wenzake kwenda chini.

Haraka alijinyanyua kwa kasi kubwa, kisha akaenda hewani kama anarukia embe. Aliposhuka alitanguliza guu lake la kulia, ambalo lilienda kutua kifuani kwa yule mwanajeshi aliyesalia, kisha akamsindikiza na risasi ya kichwa ili aanguke vizuri.

Macho yake yaliyokuwa yakitembea mithili ya bundi, yaliwaona Kipepeo na Zibuabanda wakimfuata kwa kasi na bastola zao, alipojaribu kuwalenga, risasi kwake zilikuwa zimekishwa na asingeliweza kutumia AK47 zilizokuwa pale chini, kwa sababu mikono yake bado ilikuwa imefungwa.

Kama kawaida yake, alichanua miguu kama anajiandaa kuchuchumaa, kisha alianza kuwafuata kwa kasi kubwa, akiwa anakimbia zigizaga ili kuwanyima shabaha. Hatua sita zilitosha kumkutanisha na Kipepeo, akiwa kwenye kasi ileile, alimtandika teke la mbavu na, kumuongezea teke lingine lililomuinua na kumtupa chini huku bastola ikienda chini na kujifyatua risasi bila mpangilio.

Miguu ya kuku alitaka kumvamia Zibuabanda, lakini alikuwa amechelewa. Alitandikwa ngumi nzito katikati ya kifua na, kabla hajajua cha kufanya alijikuta akidakwa mikono yake na kuzungushwa kiustadi, huku akisindikizwa na ngumi ya ubavu.

Miguu ya kuku alijikuta akienda chini bila kupenda, huku akihisi pumzi zinamkimbia. Alijua ni nini kingelimtokea, endapo angeruhusu kuendelea kulala chini huku akimwacha mpinzani wake aamue cha kumfanya.

Alijiinua chini taratibu huku akiwa na mchanga mkononi mwake. Alianza kuumwaga chini ule mchanga hadi aliposalia na vipande sita vya mchanga mkononi mwake. Aliangusha kipande kimoja na kusalia na vipande vitano.

Baada ya kusimama alimuona Zibuabanda akijiandaa kumvamia, haraka alichanua miguu yake na kuwa kama anataka kucheza mieleka ya Kijapani. Hasimu wake hakujua lengo la mkao ule na laiti angelijua, hakika asingelimfuata.

Zibuabanda akiwa ni mwingi wa hasira, alimfuata huku akiunguruma mithili ya beberu, alipomfikia alirusha ngumi tatu za harakaharaka, lakini zote ziliambulia patupu na alipojaribu kurusha teke, alijikuta akienda chini baada ya kulambwa mtama safi na kwa ufundi mkubwa. Alipotaka kunyanyuka, alijikuta akichezea makofi ya miguu kama mzaha vile na kila alipojaribu kupangua, alijikuta akiloa teke za mbavu.

Zibuabanda hakutaka kukubali, alirudi nyuma kwa kasi, na kujiweka mbali na balaa la Zuki Gado. Alipohakikisha amejiweka mbali, alijipanga upya huku mwili mzima akihisi maumivu yasiyokifani.

Alimfuata tena huku akiwa amejipanga kutumia mtindo wa Marsh-up, mtindo ambao ukipiga unawahi kujiweka kando. Alienda na kurusha konde, huku akiwahi kujiweka kando.

Mbinu yake ilifanikiwa, kwani ngumi tatu za mwanzo zilimwingia Miguu ya kuku, lakini ghafla kibao kilibadilika; alipopeleka ngumi, alijikuta akikutanisha na ugoko wa mguu chuma wa Miguu ya kuku.

‘Kaah!!’ Ilisikika sauti ya mvunjiko mithili ya ukuni uliyopitiwa na tairi ya trekta.
Zibuabanda alipiga yowe kubwa mithili ya mtu aliyeibiwa suti ya sikukuu.

Wakati yeye akiungulia maumivu ya kuvunjika mkono, mwenzake alimsogelea na kuanza kumwadhibu kwa mateke yasiyo na idadi, hadi alipoishiwa pumzi na kuanguka chini, akiwa ametota damu usoni mwake.
Miguu ya kuku alibaki akiwa amesimama huku akimshuhudia Zibua banda akiwa anagalagala chini, mithili ya chatu aliyekatwa kichwa.

Alimuainamia na kumpiga busu kwa dharau, kisha alisema…

“Huwa sipambani na watoto kwenye mapigano, mimi nizaidi ya jeshi lako… Chick-boy!” Alimalizia na kumtemea mate kwa dharau, huku macho yake yakielekea alikokuwa ameangukia Sajenti Kipepeo.

Alimuona akijizoazoa chini baada ya kurejewa na fahamu, alimfuata na kumtandika kichwa kizito kilichomrudisha chini Kipepeo na kupoteza fahamu tena.

“Baboon!” Alijisemea kwa hasira huku akiwafuata wenzake, ambao walikuwa bado wamelala chini bila matumaini.

“Nyanyukeni tuondoke hapa haraka” Aliwambia kwa sauti, huku akijivua suruari na kuacha kichapio nje, kisha alivuta hisia za kikojozi ndotoni na kulimwaga kojo kwenye pingu zake. Mkojo ulipokatika alirudisha kichapio chake na kuanza kuzivutavuta pingu, ili mkojo uingie vema kwenye loki zake. Alipohakikisha alichotaka kimeanikiwa, alienda kwenye gari na kugongesha kwenye chuma kwa nguvu na pingu ziliachia, akawa huru.

“Hatuna muda wa kumtafuta mwenye funguo za pingu, ambaye mkojo upo karibu akojolee hizo pingu,zitalainika na kuachia zenyewe” Aliwambia wenzake huku akielekea upande wa pili wa gari, ambako aliingia kwenye gari na kuliwasha.

“Haraka tuondokeni hapa” Alipaza sauti kuwaharakisha wenzake, ambao nao walienda upande wa mbele na kukaa kulia kwake.

“Fungeni mikanda” Aliwambia huku akiondoa gari kwa kasi na kushika njia waliotokea.

“Kuna yeyote aliyeumizwa?” Aliwauliza.

“Hapana!” Walijibu kwa pamoja huku wakimtizama kwa jicho la shukrani.

“Nitawarudisha Rwanda, mkifika huko fanyeni taratibu zenu mrudi nyumbani. Hiki kilichotokea mkiendelea kuwa Congo litawakuta jambo kubwa zaidi.”

“Tunashukuru sana kaka”

“Mtanishukuru mkifika salama” Aliwajibu huku akizidi kukanyaga mafuta kuelekea Gisenyi, Rwanda.

Wakati yeye alipokuwa akijitahidi kufuata njia walizopitishwa awali, huku nyuma Zibuabanda alikuwa analia kwa ghadhabu. Kitendo cha kupigwa busu na mwanaume mwenzake, kisha kutemewa mate na kuitwa Chick-boy, ilikuwa ni zaidi ya dharau. Hakuwahi kutegemea kutukanwa kiasi hicho, na hajawahi kudhani ipo siku atapigwa hadi kuvunjwa mkono na mtu aliyefungwa pingu.

Alilia kwa ghadhabu huku akiapa kulipa kisasi, aliapa kumtafuta mbaya wake popote duniani na kulipa kisasi. Aliapa kumlipa udhalilishaji aliofanyiwa.

Zibuabanda aliapa kulipa kisasi siku yoyote ya uhai wake.

.
.
.NB; KWA WALE WANAOIULIZIA, RIWAYA HII ITAANZA KUUZWA KESHO KWA BEI YA TSH2500/=.

NAMBA ZA MALIPO NI. 0656741439.TIGOPESA
0658564341.TIGOPESA(WHATSAPP)
0624155629. HALOPESA.
0758573660.MPESA(WHATSAPP).

.
.
.
.ENDELEA KUWA NAMI.
 
Hiyo Tigopesa whatsapp na Mpesa whatsapp ndio inakuaje?

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Hiyo Tigopesa whatsapp na Mpesa whatsapp ndio inakuaje?

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Anamaanisha mbali na kutumia namba hizo kwa huduma hizo za kifedha unaweza wasiliana nae pia kupitia whatsapp katika namba hizo
 
Back
Top Bottom