Shaffin Simbamwene
JF-Expert Member
- Nov 16, 2008
- 2,156
- 1,539
Del
Delta force/Missing in Action?
Delta force/Missing in Action?
Uyu Umbwa(Mbwa) ni zaidi ya Check Norris, zaidi ya stering kipensi, zaidi ya dame marasta na dame msalabani, amekomaa zaidi ya Anodi Jenny na anody jini uji uji...
Hahaha haaaUyu Umbwa(Mbwa) ni zaidi ya Check Norris, zaidi ya stering kipensi, zaidi ya dame marasta na dame msalabani, amekomaa zaidi ya Anodi Jenny na anody jini uji uji...
Jamaa kanikumbusha Em good old days
In Vino Veritas (In Wine Lies the Truth)
Mkuu tayari nishalipa ila bado umezima data WhatsAppNimerejea mkuu, nilibanwa na majukumu tangu jana
Tayari mkuu nimeipata ahsante sanaUtakuwa hujanitext baada ya kulipa. Wengine wote wamepata. Nitext upate haki yako boss. Nitext whatsap
SawaRIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA
NA; BAHATI K MWAMBA.
SEHEMU YA KUMI NA TANO.
Alimuona akijizoazoa chini baada ya kurejewa na fahamu, alimfuata na kumtandika kichwa kizito kilichomrudisha chini Kipepeo na kupoteza fahamu tena.
“Baboon!” Alijisemea kwa hasira huku akiwafuata wenzake, ambao walikuwa bado wamelala chini bila matumaini.
“Nyanyukeni tuondoke hapa haraka” Aliwambia kwa sauti, huku akijivua suruari na kuacha kichapio nje, kisha alivuta hisia za kikojozi ndotoni na kulimwaga kojo kwenye pingu zake. Mkojo ulipokatika alirudisha kichapio chake na kuanza kuzivutavuta pingu, ili mkojo uingie vema kwenye loki zake. Alipohakikisha alichotaka kimeanikiwa, alienda kwenye gari na kugongesha kwenye chuma kwa nguvu na pingu ziliachia, akawa huru.
“Hatuna muda wa kumtafuta mwenye funguo za pingu, ambaye mkojo upo karibu akojolee hizo pingu,zitalainika na kuachia zenyewe” Aliwambia wenzake huku akielekea upande wa pili wa gari, ambako aliingia kwenye gari na kuliwasha.
“Haraka tuondokeni hapa” Alipaza sauti kuwaharakisha wenzake, ambao nao walienda upande wa mbele na kukaa kulia kwake.
“Fungeni mikanda” Aliwambia huku akiondoa gari kwa kasi na kushika njia waliotokea.
“Kuna yeyote aliyeumizwa?” Aliwauliza.
“Hapana!” Walijibu kwa pamoja huku wakimtizama kwa jicho la shukrani.
“Nitawarudisha Rwanda, mkifika huko fanyeni taratibu zenu mrudi nyumbani. Hiki kilichotokea mkiendelea kuwa Congo litawakuta jambo kubwa zaidi.”
“Tunashukuru sana kaka”
“Mtanishukuru mkifika salama” Aliwajibu huku akizidi kukanyaga mafuta kuelekea Gisenyi, Rwanda.
Wakati yeye alipokuwa akijitahidi kufuata njia walizopitishwa awali, huku nyuma Zibuabanda alikuwa analia kwa ghadhabu. Kitendo cha kupigwa busu na mwanaume mwenzake, kisha kutemewa mate na kuitwa Chick-boy, ilikuwa ni zaidi ya dharau. Hakuwahi kutegemea kutukanwa kiasi hicho, na hajawahi kudhani ipo siku atapigwa hadi kuvunjwa mkono na mtu aliyefungwa pingu.
Alilia kwa ghadhabu huku akiapa kulipa kisasi, aliapa kumtafuta mbaya wake popote duniani na kulipa kisasi. Aliapa kumlipa udhalilishaji aliofanyiwa.
Zibuabanda aliapa kulipa kisasi siku yoyote ya uhai wake.
******
Gari lao likiwa kwenye mwendo mkali na wa hatari, Miguu ya kuku alivua kibegi chake mgongoni na kumpa mmoja ya watu aliokuwa nao.
“Humo ndani kuna simu, iwashe” Alimwambia huku yeye akizidi kuwa makini barabarani.
“Tayari” Jamaa alimwambia.
“Haya ingia kwenye ramani, tafuta mtaa wa Mailimbili.” Alimwambia tena.
“Tayari”
“Angalia uko upande gani, kati ya huku tuendako, au kuelekea Goma mjini na kutoka hapa ni dakika ngapi”
“Uko kilomita mbili kabla ya kufika Goma.”
“Good” Alisema huku akikunja kona kuishika barabara kubwa ya kuelekea Gisenyi mpakani.
“Tumebakiza dakika kumi kabla ya kufika mpakani, jiandaeni kwa nitakachowaambia” Alimwambia huku akizidi kuongeza kasi na gari ile ya jeshi, ambayo aliipora kwa Zibuabanda.
“Ni bahati nzuri kila mmoja hajapokonywa vitu vyake, hivyo nitawapeleka hadi Rwanda, kisha ondokeni na msijekurejea tena Goma”
“Lakini si itabidi tukaguliwe tena ili tupite na vipi kama taarifa zetu, zimeshasambazwa?” Jamaa mmoja aliuliza kwa wasiwasi.
“Nisikilize mimi na kikubwa fuata maelekezo yangu” Alimjibu huku akitua macho miguuni kwa wale Jamaa.
Aliona bunduki mbili zikiwa zimelazwa chini.
“Hebu angalieni kama kuna risasi kwenye hizo bunduki.” Aliwambia na mmoja aliinama kuzichukua bunduki zile, aliziinua na kumwonesha.
“Sawa, zirejeshe” Alimwambia huku akitizama juu ya kichwa chake na aliweza kuona simu ya upepo, ambayo ilikuwa imeunganishwa na mfumo wa gari. Alijawa na matumaini, kwa kuwa alijua ilikuwa ni lazima ile gari iwe na simu ya dharura. Gari ya jeshi haikosi simu ya dharura.
“Waungwana, jishikeni vizuri na masikio yenu yawe tayari kupokea maelekezo yangu” Alisema huku akiongeza zaidi mwendo, baada ya kuona kizuizi cha mpaka mbele yake.
Kwa kuwa alishafahamu namna kizuizi kilivyokuwa kimekaa, haikumpa shida kujua namna atakavyopita bila kungoja foleni.
Mbele yake aliona gari chache zikiwa zimewekwa foleni, kulikuwa na gari zilizokuwa zikielekea Rwanda na gari zilizokuwa zikielekea Goma. Aliachana na barabara hizo mbili, macho yake yalihamia kwenye njia ya wapita kwa miguu, haraka aliingiza gari kwenye hiyo njia, ambayo haikuwa na watu usiku huo.
Kitendo cha gari kuhamia kwenye njia ya wapita kwa miguu, kiliwafanya walinzi wa pale mpakani kukaa sawa, huku taa za ulinzi zikihamia kwenye hiyo njia na kumulika.
Miguu ya kuku hakujali akilizidi kuongeza kasi huku akipiga honi mfululizo kuwachanganya walinzi ambao hadi wakati huo, hakuwa wanajua kitakachotokea.
“Fungueni mikanda!” Aliwambia wenzake, ambao hawakuwa wanajua alichopanga.
Walipomaliza kujifungua mikanda, aliwapa maelekezo mengine tena.
“Fyatua kabali ya huo mlango!”
“Heh!” Jamaa mmoja alishangaa bila kuchukua hatua.
“Fyatuaaa!” Alifoka kwa hasira huku akishika vema usukani wa gari na kuongeza gia nyingine.
Dakika moja iliyofuata, gari ilikuwa inalipitia geti la wapita kwa miguu, kisha alishika breki kwa nguvu huku akikunja kona upande wake wa kushoto kwa kasi ileile. Gari liliserereka huku tairi zikusuguana na lami na kutoa sauti ya kulalama. Kitendo alichokifanya alijua matokeo yake ni nini, baada ya gari kusimama.
Gari ilifanikiwa kusimama kama alivyotaka; kibini ilikuwa upande wa Rwanda na bodi ilikuwa upande wa Congo, hivyo hakuna ambae angelimshambulia kwa risasi na, yeyote ambae angelishambulia angeliharibu uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.
Kitendo kile kiliwafanya wanajeshi wa pande mbili zote, kubaki wakiwa wameshika silaha zao na wasijue wazitumie kwa lipi.
“Shukeni haraka!” Aliwafokea wale jamaa, ambao bado walikuwa wanatetemeka kwa kitendo kilichotokea.
“Mkishuka chini inueni mikono juu na mpige magoti” Aliwalekeza huku yeye akianza kupangua gia ili arejeshe gari upande wa Congo.
Alianza kugeuza gari kwa fujo, kiasi kwamba iligeuka kuwa kelele pale mpakani, alipiga honi hovyo huku akikanyaga mafuta kwa fujo.
Dakika moja baadae alikuwa amefanikiwa kuirejesha gari upande wa Congo, huku Watanzania wenzake akiwa amewaacha upande wa Rwanda ambako aliamini amewaacha kwenye mikono salama na watarudi nyumbani salama.
Kitendo cha kuigeuza gari kilifanya wale maofisa wa Congo wazubae na, silaha zao. Walishindwa kushambulia kwa sababu gari ilikuwa ni ya jeshi lao. Kitu walichokifanya haraka ni kutumia vipaza sauti, kumtaka aliyekuwa ndani ya gari ashuke. Lakini ilikuwa ni kama kumuuliza mbuzi tarehe. Aliyekuwa kwenye gari hajuwajali na badala yake, alizidi kuchochea gia na kuwaacha solemba wasijue kinachoendelea.
****
Baaada ya kuwatoka maofisa wa mpakani, huku akiwa na uhakika wa usalama kwa ndugu zake aliowapeleka Rwanda, Miguu ya kuku alivuta bunduki na kuziweka kando yake, kisha alivuta simu ya upepo ambayo ilikuwa na usawa wa kichwa chake na kubonyeza kitufe cha kutafuta mawimbi. Baada ya dakika moja aliunganishwa…
“Niunge na Brigedia Fredi Mutesa.” Aliongea kwa lugha ya Lingala ambayo alisikia wakipenda kuitumia.
“Nani anazungumza” Iliunguruma sauti nzito ambayo bila shaka ilikuwa ni ya Brigedia Fredi Mutesa.
“Sajenti Kipepeo, kuna tatizo huku mpakani unaombwa msaada mkuu”
“Kwani Zibuabanda yuko wapi?”
“Simu zake hazipokelewi kabisa”
“Sawa nakuja!” Brigedia alijibu na kutoka hewani.
Miguu ya kuku alipiga usukani kwa furaha baada ya mpango wake kutimia. Aliamua kumtoa Brigedia Fredi Mutesa huko alikokuwa, ambapo ni kwa kimada wake. Alijua hivyo baada ya kumsikia Zibuabanda akizungumza kwenye simu, wakati alipokuwa nae ofisini kwake.
Kutoka pale alipokuwa hadi mtaa wa Mailimbili, kulikuwa na umbali wa kilomita sita na kwa kasi aliyokuwa anatumia, ingelimchukua dakika zaidi ya kumi na mbili. Kwake huo mwendo hakuwa akiuhitaji, hivyo alipunguza mwendo akiwa na lengo la kukutana na msafara wa Brigedia njiani.
Aliamini kama angeliendelea na mwendo wake, angeliwahi kufika kabla ya windo lake halijatoka kwa mchepuko wake.
Kupunguza kwake mwendo ilikuwa ni sahihi zaidi, licha ya kutokuwa na imani na usalama wake, kwa sababu aliamini muda mfupi mbele, angelifuatwa nyuma na majeshi ya Zibuabanda.
Simu ya upepo ilianza kuleta majibu aliyoyategemea, mawasiliano yalianza kufanyika pande mbalimbali kutarifiana kuhusu kilichotokea, kisha alisikia namba za gari alilokuwamo zikitajwa na namna ambavyo mgawanyo wa kumfukuzia ungelifanyika.
Miongoni mwa vitu alivyohitaji ni kusikia sauti ya Brigedia. Haikuchukua muda kuisikia ikitoa maagizo kwenye vikosi vilivyokuwa barabarani na vile vilivyokuwa kambini, huku yeye akisema yupo njiani kuelekea huko.
“Yes!” Alijikuta akisema kwa furaha baada ya mbinu zake kuzaa matunda. Lengo lake la kuomba kuunganishwa simu yake lilikuwa limetimia, aliweza kubaki ameunganishwa huku tayari akiwa amewasiliana na Fredi Mutesa.
Kuendelea kuunganishwa kulimwezesha kusikia mawasiliano yote ambayo yaliunganishwa na Brigedia. Kwake huo ulikua ni ushindi uwanjani na, aliuhitaji huo ushindi usiku huo.
Baada ya kujua tayari windo lake lipo njiani, alichukua bunduki moja na kuikoki, kisha alilenga kioo cha mbele cha gari alilokuwemo na kukifyatulia risasi mbili, ambazo zilienda kukisambaratisha na kubaki wazi.
Alipohakikisha kila kitu kipo kama alivyokusudia, aliongeza mwendo wa gari lake huku akizima taa za gari na kuendesha kwa kukadiria njia.
Kwa mtu mwingine ile ilikuwa ni hatari kubwa kuendesha bila kuwasha taa, lakini kwake ulikuwa ni mchezo wa kawaida kabisa ambao haukumpa shida kuucheza.
Akiwa amebakiza kilomita mbili kuufikia mtaa wa Mailimbili, macho yake yaliweza kuona gari mbili kwa mbele yake, mita kama mia sita hivi. Gari lililokuwa limetangulia lilikuwa na kimulimuli juu, huku likipiga ving'ora na likiwasha taa za kuashiria hatari. Gari la nyuma lenyewe lilikuwa linatembelea kasi ileile iliyotembelewa na gari la mbele yake.
“Kumekucha!” Alijisemea huku akiongeza kasi na kuhamia upande ambao, gari za mbele yake zilipita na kuwachanganya zaidi, alichukua bunduki na kuachia risasi kadhaa bila mpangilio, kisha alivuta begi lake na kulivaa huku usukani akiwa ameuachia na gari likiwa kwenye kasi ile ile
.
.
.
.NB; SASA UNAWEZA KUIPATA RIWAYA HII IKIWA HADI MWISHO KWA BEI YA TSH 2500/
NAMBA ZA MALIPO...
0656741439.Tigopesa.
0658564341.Tigopesa(WhatsApp)
0758573660.Mpesa.(WhatsApp)
0624155629.Halopesa.
NAMBA ZOTE JINA NI, BAHATI K MWAMBA.
UNAWEZA KUTUMA PESA UKIWA POPOTE DUNIANI.
.
.
.
ENDELEA KUWA NAMI.
Alisema ataimalizia inbox hii ilikua ni intro tu uhondo kamili lipia ili zije nyingine nyingi.Mkuu Kudo hii riwaya utaimalizia hapahapa au utahamia inbox ikihusisha mapene?