Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,408
Sabato Njema!
Waafrika wengi ni rahisi kuwaonea na kuwadhulumu kwa sababu hawana umoja. Hawapendani. Uoga mara nyingi husababishwa na kutokuwa na upendo wa dhati.
Kama Watanzania wangekuwa wanapendana Kwa dhati yote. Kusingekuwa na msamiati watu wasiojulikana.
Watu wasiojulikana ni matokeo ya Jamii kutokupendana.
Hakuna adui yoyote anayoweza kuishinda jamii inayopendana. Jamii yenye umoja inakuwa na nguvu.
Sio ajabu wazungu watano tuu walitosha kuwaswaga waafrika maelfu na maelfu.
Kuna Clip moja kipindi Fulani niliiona ikimuonyesha Mchina Mmoja akitandika waafrika mbele ya waafrika wenzao.
Jambo Hilo huwezi kulisikia likifanyika kwenye Jamii zingine. Yaani wewe muafrika uende China au Arabuni au uhindini ukawapige huko alafu wakuangalie. Hiyo haiwezekaniki.
Suala la wasiojulikana kwa sasa limeota mizizi. Na kiukweli sio kwamba hawajulikani. Wanajulikana. Serikali IPO, imeajiri maelfu ya vijana wa kulinda usalama wa watanzania. Gharama kubwa zinatumika kwenye ulinzi na usalama. Hao wasiojulikana wanatokea wapi? Kwamba hakuna jeshi, vyombo vya dola KAZI take ni ipi haswa.
Mtanzania anatekwa, watu kimya. Ingawaje wapo wachache wanapiga kelele lakini bado haitoshi.
Husikii serikali yake ya mtaa ikiwajibika.
Mjumbe, sijui mwenyekiti, sijui mbunge. Kimya.
Ni kwa sababu hawana upendo, na mtu asiye na upendo mara nyingi hukosa ujasiri. Hawezi kuwa mtenda HAKI.
Hata Kuku ukienda kuchukua kifaranga chake hupambana. Kuku anatushinda?
Kanisa analosalia Mdude au waliotekwa wengine yapo Kimya.
Waumini wapo Kimya. Alafu wanasema wanamuabudu Mungu. Kweli?
Hii inawapa nafasi viongozi wasio waadilifu waliopo serikali kutumia vibaya madaraka yao.
Najua wapo viongozi waadilifu hukohuko serikalini lakini uadilifu wao unakosa mashiko na nguvu kutokana na tabia watanzania na waafrika kwa ujumla.
Tusitegemee hata siku moja wazungu au watu wa jamii nyingine watatuokoa kutoka hapa tulipo. Watatufanya tupendane.
Umoja wetu upo kati yetu. Unatoka kwetu na sio kwa watu wa jamii zingine.
Tupendane, kwa maana huo ndio uzalendo. Huko ndio kuipenda Nchi kwa sababu nchi ni watu.
Huwezi sema unaipenda nchi yako, ati wewe ni mzalendo alafu unakaa kimya pale unapoona mambo mabaya yanafanyika kwenye nchi yako.
Kukemea mabaya ndio uzalendo wenyewe. Ndio kutaka maendeleo ya taifa lako. Maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiteknolojia n.k.
Tusiishi kwa kuviziana.
Tusiishi kwa hofu.
Watawala kuwahofia wananchi hupelekea ukatili. Kwamba mtawala anahofia maslahi yake yapo mashakani .
Na wananchi kuihofia serikali huondoa uwajibikaji na kukuza dhulma.
Ukweli utatuweka Huru
Haki itatupa Amani ya kweli
Upendo utatupa Furaha
Akili na Maarifa vitatupa maendeleo
Acha nipumzike.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam