Nini ni tofauti ya 'Mdomoni' au 'Kinywani'?

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,863
Nini tofauti kati ya neno 'mdomo' na 'kinywa'? Maneno hayo mawili jinsi watu wanavyoyatumia yamekuwa yananipa taabu. Nadhani kuna tatizo la kisarufi.

Je, kunatofauti kati ya 'kuweka kitu mdomoni' na 'kuweka kitu kinywani'?
 
Hamna tofauti, ni mambo ya lahaja tu, ukishangaa mdomoni na kinyani utaona kanwani, which means the same thing.
 
Hamna tofauti, ni mambo ya lahaja tu, ukishangaa mdomoni na kinyani utaona kanwani, which means the same thing.

Ahsante Mkuu, lakini je mtu ana midomo miwili na kinywa kimoja?
 
Kinywa ni sehemu ya kunywea (kupitisha kimiminika kwenda tumboni). Mdomo ni ujumla wa shughuli zote zinazohusika mfano kula, kunywa, kucheka na kuongea bila kusahau kuhema na kutoa makohozi n.k.
 
Mi nilidhani kwamba mdomo ni 'lip'.....yaani utasema amepata rangi midomo yake.
Na kinywa ni 'mouth'?
 
lip=midomo? sidhani kama ni sahihi? wala sijui lip kiswahili chake sahihi ni nini though.
 
Swahili translation ya Lip kumbe ni midomo. Okay.

Kwa nilivyoelewa mimi 'Lips = Midomo' and therefore 'Upper lip = mdomo wa juu' and 'Lower lip = mdomo wa chini'.

'Mouth = Kinywa' . Mouth (kinywa) is intangible while lips (midomo) are tangible.

Lakini pia nimeshawishika na hoja ya mchangiaji ambaye amelipa neno 'mdomo' maana pana zaidi kwa kujumuisha kinywa,meno, ulimi nk. Katika lugha mara nyini neno moja linaweza kuwa na maana nyini kutegemeana na watumiaji. Kwa mfani neno "mzee" kwa desturi limekuwa likimaanisha " - enye umri mkubwa", lakini leo hii neno mzee linafungamanishwa zaidi na jinsia ya kiume (eg Mzee Makamba, Mzee Mkapa) na si ya kike (huwezi kusema 'Mzee Anna Abdala', bali unasema 'Bi Anna Abdala').
 
Kimsingi naungana mkono na mchangiaji aliyesema kwamba kinywa ni sehemu ya mdomo na kwamba mdomu ni mjumuiko wa vitu vingi kama alivyovitaja. Naongeza mifano kuthibitisha
1: Fulani ananuka mdomo-Ikimaanisha anapumua hewa chafu
2: Fulani ana mdomo mchafu-Ikimaanisha kutokuwa na kauli nzuri
3: Fulani ana kidomodomo-Ikimaanisha uharaka wa kuongea
4: Kumziba mtu mdomo-mojawapo ya maana ni kutomfanya mtu kusema tena

Hata hivyo, unaweza kuweka kitu mdomoni iwapo umefunga mdomo na kuwa umelala chali au umeelekeza mdomu juu. Lakini huwezi kuweka kitu kinywani bali kitu hutiwa kinywani. Kwa maana nyingine unaweza kutia au kuweka kitu mdomoni. Mto akisema anakula haina maana kwamba anaweka chakula mdomoni/kinywani bali anakitia mdomoni/kinywani
 
Kinywa ni sehemu ya kunywea (kupitisha kimiminika kwenda tumboni). Mdomo ni ujumla wa shughuli zote zinazohusika mfano kula, kunywa, kucheka na kuongea bila kusahau kuhema na kutoa makohozi n.k.

Sikubaliani na maana uliyoitoa ya kinywa kwamba ni sehemu ya kunywea(kupitishia kimiminika) hii ni moja ya kazi za kinywa pamoja na kwamba ni kweli neno kinywa limetokana na kunywa.
Kinywa ni sehemu ya Uwazi uliyo baina ya koo na midomo ikiwa na kazi nyingi ikiwemo ya kuweka chakula kwa ajili ya kukichanganya na mate, kukisaga kwa meno na kukiaanda kumeza( nisemapo chakula namaanisha kikiwa ni kimiminika(maji pia) na hata kikiwa kigumu.
Neno Mdomo humaanisha sehemu ya nje ambayo inakazi ya kufumba na kufungua kinywa. japo kutokana na kuwa sehemu hii ndio iliyo njee na ambayo tunaiona mara nyingi, hivyo imechukua umaarufu zaidi ni kutumika neno la ujumla linalo jumuisha kunywa meno ulimi na koo kwa pamoja.
 
Kwa hiyo lips tutasema vipi ktk kiswahili fasaha maanake sijaona kitu ambacho kina maana mbili toka sehemu moja..
 
Kwa hiyo lips tutasema vipi ktk kiswahili fasaha maanake sijaona kitu ambacho kina maana mbili toka sehemu moja..

Lips ni midomo, Mdomo wa juu = Upper lip, Mdomo wa chini = Lower Lip
Kinywa ni sehemu ya ndani inayochukua ujazo. ila mara nyingine mdomo humaanisha kinywa kwa kua kinywa kimo ndani na hakionekani mara zote inayoonekana ni midomo hivyo huchukua jina la jumla ikimaanisha vyote kwa ujumla wa kinywa meno ulimi na midomo yenyewe. natumai nimeeleweka vizuri.
 
Last edited:
Back
Top Bottom