Makosa ya kuunganisha maneno katika lugha ya kiswahili

Oct 4, 2023
6
12
Kuna makosa mengi yanajitokeza katika uandishi ambayo ni makosa ya kuunganisha maneno kana kwamba ni neno moja ilhali ni maneno mawili tofauti na yenye uamilifu tofauti.

Mfano wa maneno hayo ni kama;

Nakadhalika badala ya Na kadhalika.
Halikadhalika badala ya Hali kadhalika.
Kwanini badala ya Kwa nini.
Kwakweli badala ya Kwa kweli
Kwasababu badala ya Kwa sababu.
Kwaajili badala ya Kwa ajili.


Maneno hayo huwezi kuyapata kwenye kamusi kwa sababu yanaundwa na maneno mawili tofauti. Mathalani neno Kwa nini lina neno "kwa" ambalo ni kibainishi na "nini" ambalo ni kiwakilishi kiulizi. Hivyo lazima kila neno lijitegemee.

Zacharia Emanuel (Swahili Linguist & Translator)
WhatsApp+255755350165
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom